Sifa na Bei ya Galaxy S10e Toleo la Bei Rahisi la Galaxy S10

Eti!!.. hii ndio simu ya bei rahisi kutoka Samsung
Sifa na bei ya Galaxy S10e Sifa na bei ya Galaxy S10e

Kama uliangalia uzinduzi wa Galaxy S10 hapo jana basi lazima utakuwa unajua kuwa uzinduzi huo jana ulikuwa ni uzinduzi wa simu tano mpya kutoka Samsung. Tayari tumeshangalia sifa na bei ya Galaxy S10 na Galaxy S10, pia tumesha angalia sifa na bei ya Galaxy Fold simu inayojikunja kutoka Samsung, na sasa tuangalie sifa na bei ya Galaxy S10e toleo la bei rahisi la Galaxy S10.

https://tanzaniatech.one/finder/specs/samsung-galaxy-s10e/

Kwa kuanza Galaxy S10e inakuja na kioo cha inch 5.8 chenye resolution ya 1080 x 2280 pixels pamoja na teknolojia ya Dynamic AMOLED. Kioo hicho kwa mbele kinakuja na kamera moja ya Selfie yenye uwezo wa Megapixel 10. Huku kwa nyuma simu hii inakuja na kamera mbili, moja ikiwa na Megapixel 12 na nyingine inakuja na Megapixel 16.

Advertisement

Galaxy S10e inaendeshwa na processor ya Exynos 9820 Octa (8 nm) – EMEA au Qualcomm SDM855 Snapdragon 855 (7 nm) kwa simu za marekani pamoja na China. Processor hiyo inasaidiwa na RAM ya GB 8 au GB 6, pamoja na ukubwa wa ndani ROM ya GB 128 au GB 256, vilevile unaweza kuongezea ukubwa huo kwa kutumia memory card ya hadi GB 512. Sifa nyingine za Galaxy S10e ni kama zifuatazo.

Sifa za Samsung Galaxy S10e

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.8 chenye teknolojia ya Dynamic AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16, pamoja na resolution ya 1080 x 2280 pixels.
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie) yenye mfumo wa One UI
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.7 GHz Mongoose M4 & 2×2.3 GHz Cortex-A75 & 4×1.9 GHz Cortex-A55) – EMEA au Octa-core (1×2.8 GHz Kryo 485 & 3×2.4 GHz Kryo 485 & 4×1.7 GHz Kryo 485) kwa nchini China pamoja na Marekani.
 • Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 9820 Octa (8 nm) – EMEA au Qualcomm SDM855 Snapdragon 855 (7 nm) – USA/LATAM, China.
 • Uwezo wa GPU – Mali-G76 MP12 – EMEA.
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja ikiwa na GB 256 na nyingine ikiwa na GB 128 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
 • Ukubwa wa RAM – Ziko za aina mbili GB 8 au GB 6.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 10 yenye, f/1.9, Dual Pixel PDAF Huku ikisaidiwa na Dual video call, Auto-HDR.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja inakuja na Megapixel 12, yenye uwezo wa f/1.5-2.4, 26mm (wide), 1/2.55″, 1.4µm, Dual Pixel PDAF, OIS, nyingine inakuja na  Megapixel 16 yenye f/2.2, 12mm (ultrawide). Huku zote zikiwa na uwezo wa kurekodi video za 2160p@60fps, 1080p@240fps, 720p@960fps, HDR, dual-video rec.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3100 mAh yenye teknolojia ya Fast Charging.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE
  na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO na USB ya 3.1, Type-C 1.0 reversible connector; magnetic connector.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi sita za Prism White, Prism Black, Prism Green, Prism Blue, Canary Yellow, Flamingo Pink.
 • Mengineyo – Haina Radio FM (Radio ipo kwa simu za USA na China), inatumia laini mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack. Inayo teknolojia ya kuzuia maji na vumbi, IP68 dust/water proof (up to 1.5m for 30 mins), Inayo teknolojia ya kuchaji vifaa vingine kwa kutumia Wireless.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass, barometer, heart rate, SpO2.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa pembeni).

Bei ya Samsung Galaxy S10e

Kwa upande wa bei ya Galaxy S10e, simu inatarajiwa kuingia sokoni mwezi ujao huku simu hiyo ikitarajiwa kuanzia dollar za marekani $750 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 1,748,000 bila kodi. Kumbuka bei ya simu hii inaweza kubadilika kutokana na kodi pamoja na viwango vya kubadilisha fedha. Kama hii ni simu ya bei rahisi kwako basi karibu kwenye ulimwengu wa smartphone…!

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use