Nokia Yazindua Simu Mpya za Nokia 3.2, 4.2 na Nokia 1 Plus

Fahamu sifa kamili pamoja na bei za simu mpya za Nokia
Nokia Yazindua Simu Mpya za Nokia 3.2, 4.2 na Nokia 1 Plus Nokia Yazindua Simu Mpya za Nokia 3.2, 4.2 na Nokia 1 Plus

Mkutano wa MWC 2019 bado unaendelea huko nchini Barcelona ambapo kampuni mbalimbali zipo tayari kuonyesha bidhaa zake mpya. Moja ya kampuni ambayo tayari imeonyesha bidhaa zake ni pamoja na kampuni ya Nokia ambayo inaendeshwa na kampuni ya HMD Global.

Hivi karibuni kampuni hiyo ilizindua rasmi simu mpya ya Nokia 9 Pureview, simu ya kwanza kutoka kampuni ya Nokia kuwa na kamera tano kwa nyuma. Lakini kama haitoshi kupitia mkutano huo kampuni ya Nokia pia imezindua simu mpya nyingine za Nokia 3.2, Nokia 4.2, Nokia 1 Plus pia bila kusahau aina mpya ya simu ya kitochi ya Nokia 210.

Simu hizi mpya za Nokia hazina tofauti sana kimuundo na simu nyingi za Nokia ambazo tayari ziko sokoni, utofauti wake mkubwa uko kwenye sifa ambazo tunaenda kuzingalia moja kwa moja bila kupoteza muda.

Advertisement

Sifa za Nokia 3.2

Nokia 3.2

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.2 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1520 pixels.
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie).
 • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM429 Snapdragon 429.
 • Uwezo wa Processor (CPU) – Quad-core 1.8 GHz Cortex-A53.
 • Uwezo wa GPU – Adreno 504.
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja ikiwa na GB 16 na nyingine ikiwa na GB 32 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 400.
 • Ukubwa wa RAM – GB 3 au GB 2
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 5.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 huku ikiwa na uwezo wa kurekodi video za 1080p@30fps, kamera hiyo pia inakuja na Flash ya LED.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4000 mAh Battery.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 3.1, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Black, Steel.
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Aina za Sensor – Fingerprint, accelerometer, proximity
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma) kwa toleo lenye GB 32 na RAM GB 3.

Bei ya Nokia 3.2

Nokia 3.2 inategemewa kuingia sokoni mwezi wa nne mwaka huu 2019, Simu hii inatarajiwa kupatikana kwa dollar za marekani $139, ambayo ni sawa na Tsh 326,000 bila kodi kwa toleo lenye ukubwa wa GB 16, Kwa toleo lenye ukubwa wa GB 32 likitarajiwa kupatikana kuanzia dollar $169, ambayo ni sawa na Tsh 396,000 bila kodi.

Sifa za Nokia 4.2

Nokia 4.2

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.71 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1520 pixels.
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie).
 • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM439 Snapdragon 439.
 • Uwezo wa Processor (CPU) – Octa-core (2×2.0 GHz Cortex-A53 & 6×1.45 GHz Cortex A53).
 • Uwezo wa GPU – Adreno 505.
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja ikiwa na GB 16 na nyingine ikiwa na GB 32 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 400.
 • Ukubwa wa RAM – GB 3 au GB 2
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 5.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Inakuja na kamera mbili kwa nyuma, kamera moja inakuja na Megapixel 13 yenye f/2.2, 1/3″, 1.12µm, PDAF na nyingine inakuja na Megapixel 2 yenye depth sensor, kamera zote zikiwa na uwezo wa kurekodi video za 1080p@30fps, kamera hiyo pia inakuja na Flash ya LED.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3000 mAh Battery.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 3.1, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Black, Pink Sand.
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Aina za Sensor – Fingerprint, accelerometer, proximity
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Nokia 4.2

Kwa upande wa bei ya Nokia 4.2, kama ilivyo Nokia 3.2 simu hii pia inatarajiwa kuingia sokoni kuanzia Mwezi wa nne huku bei ya Nokia 4.2 yenye GB 16 ikianzia dollar za marekani $199 ambayo ni sawa na Tsh 466,000 bila kodi. Toleo lenye GB 32 linatarajiwa kuuzwa kuanzia dollar za marekani $169 sawa na Tsh 396,000 bila kodi.

Sifa za Nokia 1 Plus

Nokia 1 Plus

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.45 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 480 x 960 pixels.
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie) Go edition
 • Aina ya Processor (Chipset) – Mediatek MT6739WW (28 nm).
 • Uwezo wa Processor (CPU) – Quad-core 1.5 GHz Cortex-A53.
 • Uwezo wa GPU – PowerVR GE8100.
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja ikiwa na GB 8 na nyingine ikiwa na GB 16 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
 • Ukubwa wa RAM – GB 1.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 5.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 8 yenye uwezo wa kurekodi video za 720p@30, kamera hiyo pia inakuja na Flash ya LED.
 • Uwezo wa Battery – Battery inayotoka ya Li-Ion 2500 mAh Battery.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 3.1, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Red, Blue.
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Aina za Sensor – accelerometer, proximity
 • Ulinzi – Haina Fingerprint.

Bei ya Nokia 1 Plus

Nokia 1 Plus inakuja rasmi sokoni kuanzia mwezi wa nne na toleo lenye GB 16 litauzwa kwa dollar $89 ambayo ni sawa na Tsh 210,000 bila kodi.

Sifa za Nokia 210

Nokia 210

Kwa upande wa simu mpya ya kitocho ambayo hii ni Nokia 210 yenyewe inategemewa kuwa na sifa zinazo karibiana sana na Nokia 3310, Kama unataka kujua sifa za simu hii mpya unaweza kusoma hapa.

Na hizo ndio simu mpya za Nokia ambazo zimezinduliwa kwenye mkutano wa MWC 2019, Kama unataka kujua habari zaidi za mkutano huu tembelea ukurasa wetu maalum hapo chini utapa habari zote kuhusu MWC 2019.

MWC 2019

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use