Bando Linaisha Haraka ? Elewa Zaidi Kuhusu Data Roaming

Fahamu kuhusu gharama zinazoletwa kwa kutumia sehemu ya Data roaming
Data roaming Data roaming

Ukweli ni kwamba kila mtu kwa wakati wake ameshawahi kukutana na adha ya kuona bando linaisha kwa haraka bila kutumia au bila sababu, well moja kati ya sababu za muhimu kuhusu tatizo hili ni sehemu ya Data roaming.

Leo tutenda kuangalia zaidi kuhusu sehemu hii ya Data roaming na jinsi gani inafanya kazi, pia mwisho nitaenda kukwambia ni mahali gani muhimu kutumia sehemu hii ya Data roaming, pamoja na jinsi ya kuzima na kuwasha sehemu hii kwenye simu yako. Bila kupoteza muda twende tukajifunze zaidi.

Data Roaming ni nini ?

Data roaming ni aina ya mpangilio ambao unakuruhusu kutumia Internet ya mitandao mingine ya simu hata kama (uko nje ya mtandao wako) huja jisajili na mitandao hiyo. Kwa mfano kama wewe unatumia laini ya simu ya Vodacom ni lazima utakuwa unatumia huduma za internet za Vodacom, lakini sasa kwa kutumia mpangilio wa Data roaming unaweza kuendelea kutumia huduma za internet za Tigo kwenye laini yako ya Vodacom hata bila kuwa na laini ya Tigo kwenye simu yako.

Advertisement

Kutokana na kampuni zinazotoa huduma ya Internet kutofautiana miundombinu na gharama za Internet, basi lazima utaona ongezeko la Speed ya Internet kwenye simu au kifaa chako, pia lazima utaweza kuona ongezeko la gharama za matumizi ya Internet kwenye simu yako.

Kwa nini utumie Data Roaming ?

Data Roaming imewekwa kwaajili ya kusaidia usiweze kukosa internet hata kama uko nje ya mtandao wako (Nje ya nchi au Mji), mara nyingi sehemu hii inasaidia sana endepo upo eneo ambalo mtandao wako unaotumia kwenye eneo hilo hauna internet nzuri. Kwa mfano labda umenda kwenye kijiji fulani, kwenye kijiji hicho unajua kabisa mtandao wa Airtel upo kwenye kijiji hicho lakini wewe unatumia Vodacom au Tigo, kwa kuwasha sehemu ya Data roaming utaweza kutumia internet kwa speed nzuri kwani sasa utakuwa unatumia Internet kutoka kwenye mtandao wa Airtel ambao unapatika eneo ulilopo.

Kwanini usitumie Data Roaming ?

Kila kizuri hakikosi kasoro na kwa sababu Data roaming hutegemea zaidi miundombinu ya makampuni mengine basi ni wazi kuwa hapa kuna gharama za ziada kutumia sehemu hii.

Kutumia Data Roaming kuna hitaji uangalifu sana kwani gharama zinaweza kuwa kubwa sana hasa kwa wale wanaotumia huduma za malipo ya baada ya matumizi, vilevile pia kwa wale wanaotumia huduma za malipo kabla ya matumizi, wanaweza kuona tatizo la data kuisha kwa haraka pamoja na matatizo mengine kama salio kutumika wakati unacho kifurushi cha data.

Utajuaje kama unatumia Data Roaming ?

Mara nyingi simu nyingi zinakuja zikiwa sehemu ya Data Roaming inakuwa ON, sehemu hii inawashwa kwa sababu ya kukupa urahisi wa kupata huduma ya Internet kila mahali unapokuwa hata unapo kuwa sehemu isiyokuwa hakuna huduma za Internet za mtandao unaoutumia.

Lakini pia inawezekana kujua kama unatumia sehemu ya Data Roaming kwani simu nyingi za Android pamoja na iPhone huonyesha ishara juu ya kioo kama unatumia sehemu hiyo. Mara nyingi ishara hiyo inakuwa na herufi “R” lakini kwa muundo inaweza kutofautiana kwenye kila simu au kifaa. Kwa mfano unaweza kuona alama kama hiyo hapo chini.

Bando Linaisha Haraka ? Elewa Zaidi Kuhusu Data Roaming

Kuepuka Gharama za Data Roaming

Ukweli ni kwamba Data roaming ni sehemu muhimu sana kuongeza kasi ya Internet yako, lakini pia ni chanzo cha data kwenye simu yako kuisha haraka pamoja na kupotea kwa senti kadhaa kwenye salio lako la kawaidia.

Unaweza kuzima sehemu hii kwenye simu yako kwa kufuata hatua hizi. Kama unatumia simu ya Android ingia kwenye Settings > Connections > Mobile networks > Kisha zima sehemu ya Data Roaming. Kama unatumia iPhone unaweza kuingia sehemu ya Settings > Mobile Data > Mobile Data Options kisha hakikisha sehemu ya Data roaming imezimwa. Pia kumbuka kama utakuwa sehemu ambayo haina Internet vizuri unaweza kuwasha sehemu hiyo ya Data roaming kwa kufuata hatua kama hizo hapo juu.

Hitimisho

Kwa ufupi kabisa hiyo ndio sehemu ya Data roaming, kujua zaidi kuhusu sehemu hii hakisha unaongea na watoa huduma wa mtandao wa simu unaotumia pia hakikisha kuwa unazima sehemu hii endapo upo eneo lenye uhakika wa Internet.

Kama una maswali au kuna mahali ujaelewa basi unaweza kuandika swali lako kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kwa uchambuzi zaidi kuhusu maswala mengine ya Teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use