Zifahamu kwa Undani Sifa za Simu Mpya ya Tecno Camon CX

Kwa wapenzi wa simu za Tecno wanaojiandaa kupata toleo jipya la Tecno Camon
Tecno Camon CX Tecno Camon CX

Kwa wapenzi wa Tecno huu ni wakati mwingine tena kwani kampuni ya Tecno Mobile sasa iko tayari kutoa toleo lake jipya la simu za Tecno Camon, simu hizo mpya za Tecno Camon CX pamoja na Camon CX Air zimepangwa kuzinduliwa rasmi kwa hapa Tanzania siku ya Jumamosi tarehe 8 Aprili.

Simu hizi mpya za Tecno Camon CX pamoja na Tecno Camon CX Air sasa zinakuja zikiwa zime-tengenezwa maususi kabisa kwa wale wanaopenda picha maarufu kama selfies. Tukirudi kwenye sifa za simu hizi Tecno Camon CX inakuja na Processor ya Media Tek MT6750T yenye uwezo wa 1.5GHz ikiwa pamoja na RAM ya GB 2 pamoja na Ukubwa wa ndani wa GB 16, simu hii vilevile inakuja na toleo jipya la Android Nougat au Android 7 huku ikiwa inaendeshwa na Battery yenye uwezo wa 3200 mAh ikiwa imewezeshwa kwa teknolojia ya Li-Po (Lithium polymer battery) ambayo ina uwezo wa kudumi na chaji kuanzia masaa 22 na kuendelea.

Advertisement

Kwa upande wa kioo simu hii ina kioo cha size ya inch 5.5 ikiwa na teknolojia ya IPS display chenye resolution ya 1080 X 1920 pixel, simu hizi pia zime tengenezwa na uwezo wa 3G pamoja na 4G zote zikiwa zinauwezo huo. Tukiangalia upande wa kamera Tecno Camon CX inakuja na kamera ya Mbele na nyuma zote zenye uwezo wa 16 Megapixel huku kwa mbele kamera yake ikiwa na teknolojia ya dual-LED flash pamoja na uwezo wa Auto Focus kwa kamera zote mbili ya mbela na nyuma.

Kwa kifupi hizi ndio sifa za simu mpya za Tecno Camon CX pamoja na Tecno Camon CX Air

  • 5.5-inch IPS Display, 1080 x 1920 pixels (400ppi)
  • 1.5GHz octa-core Mediatek CPU with 2GB RAM
  • Android 7.0 (Nougat) with HiOS
  • 16GB Storage with support for memory card up to 128GB
  • 16MP Rear Camera and 16MP Front Camera
  • 4G LTE (up to 150Mbps)
  • Fingerprint Sensor (Rear)
  • 3200 mAh Battery with Fast Charging

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use