Sehemu Muhimu ya Galaxy S8 Kutoku Fanya Kazi Vizuri

Kama ulikua unategemea kuipata Samsung Galaxy S8 hivi karibuni basi soma hii
galaxy s8 simu galaxy s8 simu

Kwa wapenzi wa simu mpya ya Samsung Galaxy S8 jana walipokea taarifa ya kushtua kidogo kiasi cha kuanza kutengeneza majadiliano kadhaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii. Taarifa hizo ambazo zilikua zinausisha kutokufanya kazi vizuri kwa sehemu muhimu ya simu hiyo mpya.

Taarifa hizo zilikua zikisema kuwa, sehemu hiyo maarufu kama Bixby au Voice Assistance kama ilivyo programu ya SIRI sasa haito fanya kazi vizuri mpaka hapo itakapo tangazwa na Samsung. Simu hiyo itaendela kutoka kama kawaida kuanzia  April 21 huku sehemu za programu hiyo ya Bixby kama vile Vision, Home na Reminder zikifanya kazi kama kawaida lakini sehemu ya Bixby Voice haitoweza kufanya kazi mpaka hapo itakapo tangazwa na kampuni Samsung.

Habari hizo zimekuja kwa kushtua wakati watu wakiwa wana tegemea kununua simu hiyo kutokana na sehemu hiyo ambayo ilitangazwa kwenye uzinduzi wa Simu hiyo hapo March 29.

Advertisement

Haya hivyo ndio taarifa yenyewe kumbuka sio kwamba simu hiyo itakuwa haifanyi kazi bali ni sehemu hiyo ndio itakuwa haifanyi kazi vizuri na kizuri zaidi sehemu hii ni software au programu hivyo basi baadae Samsung itatoa update ambazo zitawezesha sehemu hiyo kufanya kazi vizuri kama kawaida.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja yote ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use