Kampuni ya Lenovo Yazindua Simu Mpya Tatu Nchini China

Hivi ndivyo kampuni ya Lenovo ilivyorudi kwa mwaka huu 2018
Kampuni ya Lenovo Yazindua Simu Mpya Tatu Nchini China Kampuni ya Lenovo Yazindua Simu Mpya Tatu Nchini China

Baada ya kuwa kimya kwa takribani mwaka sasa, kampuni ya lenovo imerudi tena na mwaka huu imezindua simu zake mpya tatu huko nchini China. Simu zilizo zinduliwa ni pamoja na Lenovo S5, Lenovo K5 pamoja na Lenovo K5 Play.

Kwa kuangalia muonekano simu hizi ni simu nzuri sana kwa muonekano, huku zikiwa na rangi nzuri za kuvutia. Japokua simu hizi zote zimetoka ndani ya simu moja lakini zinakuja na sifa tofauti. Kuzijua zaidi hizi hapa ndio sifa kamili za simu hizo tukianza na simu mpya ya Lenovo S5.

Sifa za Lenovo S5

Advertisement

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.7 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolutiion ya 1080 x 2160 pixels, 18:9 ratio (~424 ppi density)
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android Oreo 8.0
 • Uwezo wa Processor – Octa-core 2.0 GHz Cortex-A53
 • Uwezo wa GPU – Adreno 506
 • Ukubwa wa Ndani – GB 128, GB 64 na GB 32 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa Memory card hadi ya GB 128
 • Ukubwa wa RAM – Ziko za aina mbili moja ina GB 3 na nyingine GB 4
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16 yenye f/2.4, 1/5″ sensor size, 1.12 µm pixel size, pamoja na uwezo wa kuchukua video za 2160p@30fps, 1080p@30fps
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili zenye Megapixel 13 yenye f/2.2, pamoja na teknolojia za phase detection autofocus, na LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3000 mAh battery
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bletuooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go
 • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Night Black na Flame Red
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by)
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint kwa nyuma

Simu hii inategemewa kunza kuuzwa kwa dollar za marekani $157.74 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 360,000 kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania.

Sifa za Lenovo K5

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.7 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolutiion ya 720×1440 pixels, 18:9 ratio (~424 ppi density)
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 Nougat
 • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.5 GHz MediaTek MT6750V
 • Uwezo wa GPU – Mali T860
 • Ukubwa wa Ndani – GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa Memory card hadi ya GB 128
 • Ukubwa wa RAM – GB 3
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye f/2.0
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ina  Megapixel 13 na nyingine ina Megapixel 5 moja ikiwa na f/2.0 na nyingine f/2.2 pamoja na teknolojia za phase detection autofocus, na LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3000 mAh battery
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bletuooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go
 • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Elf Blue, Space Grey na Star Black
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by)
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint kwa nyuma

Simu hii ya Lenovo K5 inategemewa kuingia sokoni kwa dollar za marekani $141.93 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 322,000 kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania.

Sifa za Lenovo K5 Play

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.7 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolutiion ya 720×1440 pixels, 18:9 ratio (~424 ppi density)
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 Oreo
 • Uwezo wa Processor – 8 Core 1.4 GHz
 • Uwezo wa GPU – Adreno 505
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko za aina mbili moja ina GB 32 na nyingne GB 16 ikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa Memory card hadi ya GB 128
 • Ukubwa wa RAM – GB 3
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye f/2.0
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ina  Megapixel 13 na nyingine ina Megapixel 2 moja ikiwa na f/2.0 na nyingine f/2.4 pamoja na teknolojia za phase detection autofocus, na LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3000 mAh battery
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bletuooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go
 • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Jazz Blue, Modern Gold na Punk Black
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by)
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint kwa nyuma

Lenovo K5 Play inategemewa kuuzwa kwa dollar za marekani $110.35 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 250,000. kumbuka bei za simu zote ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo na bei inaweza kubadilika kutokana na kodi. Simu hizi kwa sasa zinapatikana nchini china pekee na inawezekana kuzipata kwa hapa Tanzania kwa siku za karibuni.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use