Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Simu Mpya Zinazo Tarajiwa Kuzinduliwa Leo Tarehe 27/3/2018

Simu mpya zilizo zinduliwa leo au zitakazo zinduliwa leo
Simu Mpya Xiaomi-Mi-Mix-2 Simu Mpya Xiaomi-Mi-Mix-2

Siku ya leo kunafanyika uzinduzi wa simu mbalimbali ikiwa pamoja na kufanyika kwa tamasha la Apple ambalo nalo litafanyika siku ya leo huku tukitegemea kuona baadhi au vifaa vipya kutoka kampuni ya Apple. Sasa kurahisisha mambo nimeona nikulete hii list ili uweze kujua simu zitakazo zinduliwa au zilizo zinduliwa siku ya leo.

Huawei P20 inatarajiwa kuzinduliwa leo na tutakuwa Live tukionyesha uzinduzi huo mubashara kabisa. Simu hii inatarajiwa kuja na kamera tatu zenye ukubwa wa MP 40, MP20, pamoja na MP 8. Usikioze kuangalia uzinduzi ili kujua zaidi.

Advertisement

  • Xiaomi Mi Mix 2S

Simu nyingine ambayo tayari mpaka sasa imeshazinduliwa ni Xiaomi Mi Mix 2S, hii ni toleo jipya la simu ya Xiaomi Mi Mix 2 ambalo lilitoka mwezi September. Simu hii inakuja na muundo wa kisasa pamoja na sifa nzuri zaidi kuliko simu ya Xiaomi ya mwaka jana, Japo kuwa simu hii kufika Tanzania itakuwa ngumu kidogo lakini tutakuletea sifa zake kamili ili pale unapokutana nayo iweze kukusaidia kujua sifa zake.

Vilevile inasemekana leo kuwa Apple itazindua iPad mpya ambayo itakuwa maalum kwa ajili ya wanafunzi, iPad hiyo inategemewa kuja ikiwa na bei rahisi tofauti na iPad iliyoko sasa sokoni. Bado haijajulikana iPad hiyo itakuja na sifa gani zingine lakini tutawaletea habari zaidi pale tutakapo zipata. Kuhusu kuonyesha uzinduzi huu mubashara, kwa bahati mbaya Apple haitakuwa live kuonyesha uzinduzi huo lakini tutawaletea habari zote pindi tutakapo zipata.

Na hizo ndio simu mpya ambazo zitakuja au zitazinduliwa siku ya leo, endelea kutembelea Tanzania Tech tutakupa taarifa zaidi pale tutakapo zipata. Pia usisahau kuangalia mubashara uzinduzi wa Huawei P20 unakuja hivi punde.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use