Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Samsung Yazindua Galaxy J4 Core Simu Mpya Yenye Android Go

Samsung imekuja tena na simu yake nyingine inayotumia Android GO
Samsung Yazindua Galaxy J4 Core Simu Mpya Yenye Android Go Samsung Yazindua Galaxy J4 Core Simu Mpya Yenye Android Go

Kampuni ya Samsung inaendelea na jitihada za kupambana na kampuni kama Tecno na Infinix kwa kuja na simu za bei nafuu ambazo zinaweza kutumiwa na wananchi wa hali ya chini, Sasa katika kufanya jitihada hizo, kampuni ya Samsung imetangaza kuja na simu yake ya pili inayo tumia mfumo wa Android Go, mfumo wa Android ambao umetengenezwa maalum kwa simu zenye uwezo wa RAM hadi GB 1.

Simu hii mpya ya Samsung Galaxy J4 Core inakuja na kioo cha inch 6.0 ambacho kina resolution ya 720 x 1480 pamoja na teknolojia ya High Definition HD. Kwa upande wa processor Galaxy J4 Core inakuja na processor ya Exynos 7570 Quad SoC yenye uwezo wa quad-core Cortex-A53 CPU yenye speed ya 1.4 GHz.

Advertisement

Processor ya Simu hii inasaidiwa na RAM ya GB 1, pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 16 huku ukubwa huo ukiwa na uwezo wa kuongezewa na Memory Card hadi ya GB 512. Tukiamia kwenye upande wa kamera, Galaxy J4 Core inakuja na kamera moja kwa nyuma yenye uwezo wa Megapixel 8 yenye f/2.2 lens. Kwa mbele simu hii inakuja na kamera moja ya selfie yenye Megapixel 5 ambayo inauwezo wa f/2.2 aperture. Sifa nyingine za Samsung Galaxy J4 Core ni kama zifuatazo.

Sifa za Samsung Galaxy J4 Core

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.0 chenye teknolojia ya LCD IPS capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1480 pixels, na uwiano wa 18.5:9 ratio (~274 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo Go)
  • Uwezo wa Processor – Quad-core 1.4 GHz Cortex-A53.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm MSM8917 Snapdragon 425 (28 nm) Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 308.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card ya hadi GB 512.
  • Ukubwa wa RAM –  RAM ya GB 1
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 5
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 8 yenye HDR, panorama na LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery Inayotoka ya Li-Ion 3300 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 b/g/n, Wi-Fi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. micro USB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Blue, Black, Copper.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Accelerometer, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Haina Fingerprint.

Bei ya Samsung Galaxy J4 Core

Kwa upande wa bei ya Samsung Galaxy J4 Core, bado hakuna ripoti zaidi kuhusu bei ya simu hii, ila tegemea kupata simu hii kwa makadirio ya Tsh 200,000 hadi Tsh 350,000 pamoja na kodi. Endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza zaidi kuhusu simu hii ikiwa pamoja na mahali pakununua simu hii.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use