Habari Njema Kwa Watumiaji wa Tecno Camon X na Camon CM

Watumiaji wa simu hizo kuweza kupata simu mpya za Camon 11 kwa urahisi
habari njema watumiaji wa camon cm na camon x habari njema watumiaji wa camon cm na camon x

Kama tulivyo weza kuona hivi karibuni kampuni ya Tecno imezindua simu zake mpya za Tecno Camon 11 pamoja na Tecno Camon 11 Pro, simu hizi zinakuja na maboresho makubwa sana kuanzia muundo mpaka kwenye sifa zake.

Kama ulikuwa hujui, Tecno Camon 11 na Camon 11 Pro ni simu za kwanza kabisa kutoka kampuni ya Tecno ambazo zinakuja na ukingo wa juu maarufu kama notch, na pia simu hizi ni simu za kwanza kabisa kutoka Tecno kuja na mfumo wa AI au Artificial intelligence moja kwa moja kwenye kamera zake.

Sasa katika kusherekea mwisho wa mwaka 2018, kampuni ya Tecno inakuja na ofa kabambe kwa wateja wake wanaotumia simu za Tecno Camon CM, Tecno Camon X pamoja na Camon X Pro, ofa hiyo itakuwa inawapa urahisi watumiaji wa simu hizo kuweza kupata simu mpya za Tecno Camon 11 au Camon 11 Pro kwa urahisi zaidi.

Advertisement

Kwa mujibu wa ripoti maalum, Kampuni ya Tecno hapa Tanzania itakuwa inatoa ofa ya kubadilisha simu hizo za zamani za Camon X na Camon CM kwa wateja wake wote watakao kidhi vigezo na masharti na kuweza kuwapa simu mpya za Tecno Camon 11 pamoja na Camon 11 Pro. Hata hivyo bado hakuna ripoti kamili za vigezo na masharti hayo ila ni wazi kuwa simu zitakazo kubalika kwenye ofa hiyo ni zile simu ambazo zitakuwa kwenye hali nzuri yaani zitakuwa nzima kwa asilimia 100.

Mbali na hayo pia inawezekana simu zitakazo kubaliwa kwenye ofa hiyo ni zile simu ambazo zitakuwa hazina muda mrefu sana toka zinunuliwe. Hivyo basi, kama ulikuwa umepanga kununua simu mpya ya Tecno Camon X au Camon CM basi hakikisha unafanya hivyo sasa kwani unaweza kupata simu mpya ya Camon 11 na Camon 11 Pro kwa bei nafuu zaidi.

Unaweza kupata Tecno Camon X kwa punguzo la hadi Tsh 400,000 na Camon X Pro kwa hadi punguzo la Tsh 495,000. Pia unaweza kupata Tecno Camon CM kwa punguzo la hadi Tsh 299,000. Kwa habari zaidi kuhusu ofa hii hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use