Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Simu Bora za Infinix za Chini ya TZS 300,000

Simu hizi zimetoka hivi karibuni lakini zinapatikana kwa bei nafuu
Hizi Hapa Simu Bora za Infinix za Chini ya TZS 300,000 Hizi Hapa Simu Bora za Infinix za Chini ya TZS 300,000

Kampuni ya infinix imezidi kuboresha simu zake kadri muda unavyokwenda, siku za karibuni tumeona kampuni hiyo ikizindua simu mpya ya Infinix S5, simu ambayo inakuja na aina mpya kabisa ya kioo ambacho kina tundu la kamera ya mbele juu ya kioo na pia simu hii inakuja na kamera nne kwa nyuma.

Hizi Hapa Simu Bora za Infinix za Chini ya TZS 300,000

Advertisement

Ukijaribu kuangalia simu hiyo utaona kuwa kampuni ya Infinix inajitahidi sana kuendana na kasi ya teknolojia kwa kuja na simu bora lakini pia ambazo zinapatikana kwa bei nafuu ambayo watanzania wengi pamoja na waafrika kwa ujumla wanaweza kununua.

Sasa kuliona hilo leo nimekuletea list ya simu bora za infinix ambazo unaweza kupata hapa Tanzania kwa bei ya chini ya shilingi za kitanzania TZS 300,000. Kumbuka bei za simu hizi zinaweza kutofautiana kulingana na sehemu unayo nunulia simu hiyo hivyo neno langu sio sheria. Basi baada ya kusema hayo moja kwa moja twende tuka angalie list hii.

Infinix Hot 8 – TZS 280,000

Hizi Hapa Simu Bora za Infinix za Chini ya TZS 300,000

Infinix Hot 8 ni moja kati ya simu bora sana kwa sasa hasa kama wewe ni mmoja wa watu wanaopenda simu zinazo dumu na chaji, simu hii ni bora sio kwa upande wa chaji tu pali pia simu hii inakuja na muonekano mzuri na pia simu hii inakuja na mfumo mpya wa Android 9.0 (Pie) pamoja na mfumo wa infinix wa XOS 5.5.

  • CPU: Octa-core 2.0 GHz
  • RAM: 4 GB
  • Storage: 64 GB
  • Display: IPS LCD 6.5 Inch
  • Camera: Triple 13 MP, 2 MP, 2MP
  • OS: Android 9.0 (Pie)

Infinix Hot 8 Lite – TZS 260,000

Hizi Hapa Simu Bora za Infinix za Chini ya TZS 300,000

Tofauti kidogo na Infinix Hot 8, infinix Hot 8 Lite nayo ni simu nzuri sana ambayo inapatikana kwa bei nafuu chini ya TZS 300,000. Simu hii ni bora sana kwa wale ambao wanataka simu nzuri ya kisasa yenye uwezo wa kawaida. Simu hii inakuja na mfumo wa Android Go, mfumo ambao ni maalum kwa simu zenye uwezo wa RAM chini ya GB 1.

  • CPU: Quad-core 1.3 GHz
  • RAM: 1 GB
  • Storage: 32 GB
  • Display: IPS LCD 6.6 Inch
  • Camera: Dual 8 MP, QVGA
  • OS: Android 8.1 Oreo (Go edition)

Infinix Smart 3 Plus – TZS 280,000

Hizi Hapa Simu Bora za Infinix za Chini ya TZS 300,000

Kama wewe ni mpenzi wa simu ya infinix yenye muonekano bora na sifa za nzuri simu hii ya infinix smart 3 Plus ni simu bora sana kwako. Simu hii kama simu zilizopita kwenye list hii ni simu bora sana ambayo unaweza kupata kwa bei nafuu chini ya Shilingi za kitanzania TZS 300,000.

  • CPU: Quad-core 2.0 GHz Cortex-A53
  • RAM: 2/3 GB
  • Storage: 16/32 GB
  • Display: IPS LCD, 6.2 inches
  • Camera: Triple 13MP, 2MP, QVGA
  • OS: Android 9.0 (Pie)

Infinix Smart 3 – TZS 260,000

Hizi Hapa Simu Bora za Infinix za Chini ya TZS 300,000

Kama ilivyo infinix hot 8 lite, infinix smart 3 ni toleo la bei rahisi zaidi kwenye simu hizi za Smart 3, simu hii pia ni simu ambayo unaweza kupata kwa bei rahisi na ni moja kati ya simu ambazo zina muonekano mzuri pamoja na sifa nzuri pia. Simu hii pia inakuja na mfumo wa Android 9.0 (Pie) Go mfumo ambao ni maalum kwa simu zenye RAM chini ya GB 1.

  • CPU: Quad-core 2.0 GHz Cortex-A53
  • RAM: 2 GB
  • Storage: 16 GB
  • Display: IPS LCD, 5.5 inches
  • Camera: Dual 13MP, 2MP
  • OS: Android 9.0 (Pie) Go Edition

Na hizo ndio baadhi ya simu za infinix ambazo unaweza kupata kwa bei rahisi chini ya Shilingi za kitanzania TZS 300,000 kwa hapa Tanzania. Kumbuka bei ya simu hizi zinaweza kubadilika kulingana na mahali ambapo nunua simu hizi, bei zilizoandikwa ni kwa mujibu wa kampuni mbalimbali za kuuza simu hapa nchini Tanzania. Kama unataka kujua simu nyingine bora za Infinix na mahali unapoweza kununua unaweza kusoma makala nyingine hapa.

4 comments
  1. Asante sana kwa kutuhabarisha ila naomba kujua kazi ya kamera 2,3,4 mfano za nyuma kwenye simu moja. Make kuna siku nilifanya utafiti wa hizo kamera kwa kuziba kamera moja moja nilichogundua ni kamera moja tu iliyokuwa inafanya kazi kwa kuonesha kwenye screen kwamba ipo active. Sa hizo nyingine zina kazi gani?

  2. Safi sana nitaitaji infinix hot 8. Siku za baadae. Mimi nimtumiaji wa infinix. Japo nipo mkoa wa bukoba inakuaje kupata?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use