Galaxy J2 Core Simu ya Kwanza ya Samsung Yenye Android Go

Hizi hapa ndio sifa pamoja na bei ya Samsung Galaxy J2 Core
Sifa na Bei ya Samsung Galaxy J2 Core Sifa na Bei ya Samsung Galaxy J2 Core

Mpaka sasa kampuni ya Samsung ilikuwa haina simu yoyote yenye kutumia mfumo wa Android Go, mfumo wa Android ulio tengenezwa kwaajili ya simu zenye uwezo mdogo wa RAM. Galaxy J2 Core ndio simu ya kwanza kabisa kutoka Samsung yenye mfumo huo na imezinduliwa rasmi hapo siku ya jana.

Simu hii ya Samsung Galaxy J2 Core inakuja ikiwa na kioo cha inch 5 chenye teknolojia qHD screen, Processor ya Exynos 7570 chipset yenye uwezo wa CPU ya 1.4GHz Cortex-A53 cores, na kama unavyojua kuhusu mfumo wa Android Go, Galaxy J2 Core inakuja na RAM ya GB 1 na ukubwa wa ndani wa GB 6 yenye uwezo wa kungezewa na Memory Card. Sifa nyingine za Galaxy J2 Core ni kama zifuatazo.

Sifa na Bei ya Samsung Galaxy J2 Core

Advertisement

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.0 chenye teknolojia ya HD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 540 x 960 pixels, na uwiano wa 116:9 ratio (~220 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo Go)
  • Uwezo wa Processor – Quad-core 1.4 GHz Cortex-A53.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 7570 Quad Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali-T720.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 8 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card ya hadi GB 256.
  • Ukubwa wa RAM –  RAM ya GB 1
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 5
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 8 yenye HDR, panorama na LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery Inayotoka ya Li-Ion 2600 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 b/g/n, Wi-Fi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. micro USB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Gold na Blue
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Accelerometer na proximity.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Haina Fingerprint.

Bei ya Samsung Galaxy J2 Core

Simu hii ya Galaxy J2 Core kwa sasa itapatikana nchi mbalimbali ikiwa pamoja na chini india ambapo itapatikana kwa rupee ₹5,499 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 180,000. Kwa sasa bado simu hii haijatangazwa kuja hapa Tanzania lakini tegemea kuipata hapa Tanzania siku za karibuni, kumbuka bei inaweza kubadilika kutokana na kodi na viwango vya kubadilisha fedha.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use