Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Sony Xperia XZ3

Kampuni ya Sony imezindua simu yake mpya ya Sony Xperia XZ3
Sifa na Bei ya Sony Xperia XZ3 Sifa na Bei ya Sony Xperia XZ3

Mkutano wa IFA 2018 bado unaendelea uko nchini ujerumani, ndani ya mkutano huu kampuni mbalimbali za kieletroniki zinafanya uzinduzi mbalimbali za bidhaa mpya, Kampuni ya Sony nayo iko moja kati ya kampuni hizo na hivi leo kupitia mkutano huo Sony imezindua simu mpya ya Sony Xperia XZ3.

Simu hii ukweli kabisa inakuja na muonekano mzuri sana tofauti na simu nyingine za Sony Xperia ambazo zimezinduliwa miaka ya karibuni. Sony Xperia XZ3 inakuja na kioo cha inch 6.0 ambacho ni curved OLED, HDR display ambacho kina uwiano wa 18:9 pamoja na ulinzi wa Gorilla Glass 5.

Advertisement

Kama unavyojua kuhusu ubora wa kamera za Sony, Sony Xperia XZ3 nayo haiko nyuma, simu hii inakuja na uwezo wa kurekodi video za 4K HDR, huku ikiwa ndio simu ya kwanza kabisa kuweza kuchukua video za uwezo huo. Kuwezesha kuchukua video hizo, Sony Xperia XZ3 inakuja na kamera ya nyuma yenye Megapixel 19 yenye f/2.0, 25mm, 1/2.3″, 1.22µm, predictive PDAF & laser AF, huku kwa mbele simu hii ikiwa inakuja na kamera ya selfie ya Megapixel 13.

Kwa upande wa processor simu hii inakuja na processor ya Snapdragon 845 chipset, ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 64. Kwa upande wa GPU simu hii inakuja na uwezo wa Graphics ya Adreno 630 ambayo hii inauwezo wa kufanya kazi vizuri sana kwenye game zenye uwezo mkubwa kama vile Fortnite na nyingine kama hizo.

Mbali na hayo Sony Xperia XZ3 inakuja na vikorobwezo kadhaa kama vile uwezo wa kuzuia maji na vumbi IP65/IP68 dust/water proof (kwenye maji ya mita 1.5 kwa dakika 30), pia inakuja na uwezo wa kufungua app mbalimbali kwa kubofya kwenye ukingo wa simu hiyo, pamoja na teknolojia mpya ambayo itakusaidia kupiga picha kwa urahisi zaidi pale unapotoa simu yako mfukoni. Sifa nyingine za Sony Xperia XZ3 ni kama zifuatazo.

Sifa za Sony Xperia XZ3

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.0 chenye teknolojia ya P-OLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1440 x 2880 pixels, na uwiano wa 18:9 ratio (~537 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.7 GHz Kryo 385 Gold & 4×1.7 GHz Kryo 385 Silver).
 • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 Chipset.
 • Uwezo wa GPU – Adreno 630.
 • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
 • Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 4
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 13 yenye f/1.9, 23mm, 1/3″, 1.12µm) yenye uwezo wa kuchukua video za 1080p@30fps (5-axis gyro-EIS).
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 19 yenye f/2.0, 25mm, 1/2.3″, 1.22µm, predictive PDAF & laser AF, ambayo pia inakuja na panorama, HDR na uwezo wa kuchukua Video za 2160p@30fps, 1080p@30/60fps (5-axis gyro-EIS), 1080p@960fps, HDR. Kamera hii inasiaidwa na Flash ya LED.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3300 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging (Quick Charge 3.0).
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, aptX HD, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO. USB ya Type-C 3.1 reversible connector, USB On-The-Go.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Black, Silver White, Forest Green na Bordeaux Red
 • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na uwezo wa kuzuia maji na vumbi (IP68 dust/water proof (maji ya urefu wa 1.5m kwa dakika 30), pia Inakuja na ukingo wa pembeni unao bonyezeka.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, barometer, compass na color spectrum.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Sony Xperia XZ3

Simu hii mpya ya Sony XZ3 inatarajiwa kuingia sokoni mwishoni mwa mwezi ujao na kuhusu bei simu hiyo inatarajiwa kuuzwa kwa Euro € 800 ambayo ni sawa na Shilingi za kitanzania Tsh 2,128,000 bila kodi. Kumbuka kwa Tanzania bei hii inaweza kuongezeka kutokana na kodi na viwango vya kubadilisha fedha.

1 comments
 1. Habali ya asubuhi nimesoma na kuangalia aina ya simu sony z3 na z5 4k ukweli zipo vizuli ila bei ndo shida je? Kwa mtu wa hali ya kawaida yani hana pesa ya kiwango nilicho kisoma kwenye maelezo je mtamsaidiaje ili apate simu ynye uwezohuo?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use