Samsung Yazindua TV Zenye Uwezo wa Kufanana na Ukuta

TV hizo mpya hazita onyesha kioo cheusi zikiwa zimezimwa
TV mpya za Samsung QLED TV mpya za Samsung QLED
<a href="https://www.cnet.com/" rel="nofollow" target="_blank"><span style="font-size: x-small;">Photo by Sarah Tew/CNET</span></a>

Kama ilivyo tangazwa Kampuni ya Samsung jana ilizindua TV zake mpya za mwaka 2018 zenye teknolojia ya QLED pamoja na 4K huko New York City nchini Marekani. Bado Samsung imendelea kuwa kiongozi wa kutengeneza TV bora huku kwa mwaka huu ikiwa imekuja na TV zenye maboresho zaidi pamoja na mfumo wa usaidizi wa sauti (Voice Assistance) maarufu kama Bixby.

Mbali na kuweka mfumo huo kwenye TV hizo, Samsung pia imefanya maboresho makubwa ya picha kwenye TV zake huku ikiwezesha TV hizo kuendesha vifaa vyake vya nyumbani maarufu kama Samsung’s SmartThings smart home platform. TV zilizo zinduliwa hapo jana ni pamoja na Samsung QLED Q9, Samsung QLED Q8, Samsung QLED Q7, pamoja na Samsung QLED Q6.

TV zote hizi zinakuja na teknolojia mpya inayoitwa Ambient Mode, Ambient Mode hii ni teknolojia inayo ruhusu TV yako kuweza kulingana na mazingira ya ukuta wako pale inapokuwa imezimwa. Yaani kwa kutumia simu yako unatakiwa kupiga picha TV yako mahali ilipo, hii ikiwa pamoja na mazingira ya ukuta TV yako ilipo, kisha TV hizi za Samsung zitatumia picha hiyo kuweza kutengeneza Wallpaper au picha ambayo itafanana na ukuta wako kwa asilimia 100.

Advertisement

Mbali na sehemu hiyo kuweza kufanya TV yako kufanana na ukuta, sehemu hiyo pia inauwezo wa kuonyesha vitu mbalimbali kwenye TV yako kama vile utabiri wa hali ya hewa, habari na mambo mengine ya muhimu. Kumbuka yote hayo uweza kufanyika wakati TV yako imezimwa hivyo hutaweza kutaona kioo cheusi wakati umezima TV yako, bali sasa Ambient Mode itasaidia TV yako kuvutia zaidi pale inapokuwa imezimwa.

TV hizi mpya zinakuja kwa ukubwa tofauti kwa kila kila toleo huku Toleo la Q9 Series likiwa na TV zenye ukubwa wa inch 75 na inch 65 wakati toleo la Q8 Series litakuwa na TV zenye ukubwa wa inch 75, inch 65 pamoja na inch 55. Huku kwa upande wa Q7 Series zitakuja TV zenye ukubwa wa inch 75, inch 65 pamoja na inch 55 na toleo la mwisho la Q6 Series litakuja na TV zenye ukubwa wa inch 82, inch 75, inch 65, inch 55, pamoja na inch 49.

TV zote hizi zinategemewa kuingia sokoni siku za karibuni, huku Samsung bado ikiwa haijatangaza rasmi bei ya TV hizi.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use