LG Yazindua TV Mpya ya Inch 88 Yenye Spika Kwenye Kioo

LG yaonyesha baadhi ya teknolojia zake mpya zitakazokwepo CES 2019
TV za LG 2019 TV za LG 2019

Mkutano wa CES 2019 umebakiza siku moja kuweza kuanza rasmi na kama kawaida kampuni ya LG hupenda kuanza mapema. Mwaka huu LG imeendeleza teknolojia yake ya mwaka 2017 ya kutengeneza TV zenye uwezo wa kutoa sauti kupitia kioo au unaweza kusema Crystal Sound screen technology.

LG imetangaza maboresho ya TV ya Inch 88 (ilizinduliwa mwaka jana) yenye teknolojia hiyo pamoja na teknolojia ya 4K huku ikisemekana kuwa na sauti nzuri sana inayotolewa kwa channel ya 3.2.2 Dolby Atmos audio. Kwa mtu unaejua maswala ya audio basi utajua sauti hii ni nzuri sana hasa ikichanganywa na teknolojia ya Dolby Atmos audio.

LG Yazindua TV Mpya ya Inch 88 Yenye Spika Kwenye Kioo

Advertisement

Mbali na hayo LG imetangaza kuwa inatarajia kuzindua TV mpya za inch 65 zenye teknolojia ya 8K ambazo pia zitakuwa za bei nafuu zaidi. Kama unavyo jua kwa sasa TV zenye teknolojia ya 8K zinauzwa bei ghali sana lakini LG inatarajia kubadilisha hilo mwaka huu 2019.

Vilevile kwenye mkutano huu wa CES 2019, LG imeonyesha sanaa kwenye TV zake kwa kuja na mpangilio mpya wa TV zilizopagwa kama MAUA, LG imesema mpangilio huo umetengenezwa kwa TV za inch 64 zenye teknolojia ya Ultra HD OLED displays, Huku LG ikidai lengo la kuonyesha sanaa hiyo ya kupanga TV kwa mfumo huo ni kuonyesha jinsi TV hizo zina vyoweza kufanya kazi vizuri zikiwa zote kwa pamoja bila kupoteza ubora, (Angalia Picha Hapo Chini).

LG Yazindua TV Mpya ya Inch 88 Yenye Spika Kwenye Kioo

Mbali na hayo LG inatarajia kuzindua TV nyingine ambazo zinajikunja ambazo tuliona mwaka jana kwenye mkutano wa CES 2018. Pia tegemea kuona mpya za inch 27 kutoka LG, hizi zinaitwa Art portable display ambazo nazo zitazinduliwa hivi karibuni kupitia mkutano huu wa CES 2019.

Kwa ufupi kabisa hayo ndio mambo ambayo LG imeweza kuyataja kwa siku ya jana, lakini mambo yote yana anza kesho hivi hakikisha una tembelea Tanzania Tech kujua mambo yote yanayojiri kwenye mkutano wa CES 2019 na yote yatakayojiri.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use