TV 5 Zenye Ving’amuzi Vinavyo Onyesha Chaneli za Ndani Bure

Hizi hapa TV 5 za bei nafuu zenye ving’amuzi vya kuonyesha chaneli za bure
TV zenye ving'amuzi TV zenye ving'amuzi

Hivi karibuni hapa Tanzania kumekuwa na sintofahamu baada ya baadhi ya ving’amuzi kuacha kuonyesha chaneli za ndani kutokana na kutii sheria au maagizo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Sasa kutokana na kutii sheria hii watu wengi kwa sasa hawaoni chaneli za ndani kutokana na ving’amuzi hivyo kusitisha kuonyesha Chaneli hizo.

Sasa leo hapa Tanzania Tech tumekuleta makala hii ambayo itakufahamisha aina za TV ambazo hizi utaweza kuzitumia kuweza kuona chaneli za ndani bure kabisa bila kulipia au bila kuhitaji Ving’amuzi. TV hizi nyingi au zote zinapatikana hapa Tanzania na unaweza kuzipata kwenye maduka mbalimbali yanayo uza TV kwenye mkoa uliopo, basi bila kupoteza muda Twende tukangalie TV hizi.

1. LG 32LF5100

TV hii ni moja kati ya TV nzuri sana na ambazo zinaweza kuonyesha chanel za ndani bila kuwa na ving’amuzi. TV hii kwa sasa inapatikana kwa bei nafuu sana kupitia maduka ya Game. TV hii ya inch 32 inapatikana kwa makadirio ya Tsh 700,000 hadi Tsh 599,000.

Advertisement

2. LG 43LH576T

TV hii ya LG ni moja kati ya TV ambayo inapatikana sana hapa Tanzania, mbali ya kupatikana kwake TV hii ni nzuri kwa sura na inauwezo wa kuonyesha Chanel zote za ndani bure kabisa bila kingamuzi, unacho hitaji ni antenna ya nje kisha tafuta chaneli na utaona chaneli zote za ndani. TV hii inauzwa kwa makadirio ya Tsh 1,000,000 hadi 900,000 kwa inch 43.

3. Samsung J4303

Samsung J4303 ni moja kati ya TV ya bei nafuu kutoka Samsung, TV hii ni Smart TV na inauwezo wa kuonyesha chaneli zote za ndani bila kulipia au bila kuitaji kuwa na king’amuzi. TV hii inapatikana sana kwenye maduka mbalimbali hapa Tanzania na inapatikana kwa makadirio ya Tsh 800,000 hadi Tsh 700,000 kwa TV ya inch 32.

4. Sony Bravia R330B

Sony Bravia R330B ni moja kati ya TV nyingine nzuri sana kuwa nayo na ya bei nafuu, TV hii pia inauwezo wa kuonyesha Chanel zote za ndani bila kuwa na kingamuzi, TV hii kwa sasa inapatikana kwa bei nafuu kwa makadirio ya Tsh 700,000 hadi Tsh 650,000. Unaweza kuipata TV hii kwenye maduka mbalimbali ya TV hapa Tanzania.

5. LG 32LJ52

TV Hii ni moja kati ya TV nzuri sana na ya bei nafuu ambayo itakuwezesha kuangalia chaneli zote za ndani bila kulipia au kuwa na king’amuzi. TV hii inapatikana kwenye maduka mbalimbali hapa Tanzania  na unaweza kuipata kwa bei ya makadirio kuanzia Tsh 700,000 na Tsh 600,000.

Na hizo ndio TV ambazo unaweza kuzipata hapa Tanzania kwa bei nafuu ambazo zitakuwezesha kuangalia chaneli za ndani bila kulipia. Kumbuka ni muhimu kuuliza kabla ya kununua TV au ikiwezekani omba kujaribisha na utafute chaneli za ndani kabla ya kununua hii itakupa urahisi hata pale utakapo enda kutumia kwa mara ya kwanza.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use