Wote tunajua kuwa uzito ukizidi ni tatizo kubwa sana lakini kuna wakati hatuwezi kuzuia kuongezeka kutokana na aina ya kazi au hata maisha yetu kwa ujumla, lakini kwa namna moja ama nyingine kama umekua ukishndwa kupunguza uzito wako basi makala hii itakusaidia.
Kwa ufupi kabisa hii ni list ya programu bora au Apps ambazo zitakusaidia kupunguza uzito na kuweka maisha yako kwenye afya inayotakiwa, ni vizuri ukitumia apps hizi uku unafanya mazoezi ambayo ni muhimu sana hasa kwenye swala zima la kujenga afya bora.
10. Calorie Counter – MyNetDiary
Hii ni moja kati ya App ambazo ni bora sana hasa kwenye swala zima la kupunguza uzito, App hii ni rahisi sana kutumia kwani inahitaji tu uweke data zako za ulaji wako, uzito wako pamoja na uzito ambao unataka kupunguza na app hii itakusaidia kukupa ushauri pamoja na kukumbusha juu ya ulaji wako.
9. Charity Miles Walk&Run Tracker
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao unapenda kusaidia wengine huku ukiweka afya yako sawa basi app hii ni bora sana. App hii inafanya kazi tofauti kidogo kwani inakupa uwezo wa kusaidia watu mbalimbali kwa kutembea yaani pale unapotembea umbali ulio tembea unageuzwa kuwa pesa ambazo zitaenda kusaidia watu mbalimbali.
8. My Diet Coach – Weight Loss
App hii itakusaidia kupunguza uzito kwa haraka kwa kuweka uzito unaotaka kuufikia na app hii itakuwa iki kukumbusha kufanya mambo mbalimbali ya kuweza kukusaidia kupunguza uzito wa mwili wako.
7. 8fit – Workouts, Meal Planner & Personal Trainer
8fit ni programu nyingine ambayo inaweza kukusaidia kupunguza uzito wako wa mwili, app hii itakupa ushauri wa aina ya mazoezi ya kufanya pamoja na uwezo wa kukupa mazoezi marahisi ambauo unaweza kufanya popote ili kupunguza uzito wa mwili wako kwa haraka.
6. Fitbit
Fitbit ni app maarufu sana kwa kuangalia umbaili ambao unatembea huku ikikupa data mbaimbali ambazo zinaweza kukusaidia sana kuweza kupunguza uzito wa mwili wako, app hii ni moja kati ya app bora sana ijaribu sasa.
5. MyPlate Calorie Tracker
App hii ni moja kati ya app 5 bora zilizo baki kwenye list hii app hii inatengezwa na wataalamu wa afya ambao wanaendesha tovuti ya Livestrong.com tovuti maarufu kwa afya na kujenga mwili. App hii itaweza kukusaidia kuangalia chakula unacho kula pamoja na kukusisitiza unywaji wa maji ambao utakusaidia kupunguza uzito.
4. Lose It! – Calorie Counter
Hii ni app nyingine ambayo ni bora sana kwa kupunguza uzito, app hii ni moja kati ya app ambazo zinakusaidia kupunguza uzito huku unafurahia kwani app hii inakupa uwezo wa kuandika kiasi cha uzito unachotaka alafu app hii itakusaidia njia za kupunguza uzito.
3. YAZIO – Calorie Counter
Yazio ni moja kati ya app bora sana inauwezo mkubwa sana wa kukusaidia kupunguza uzito, unachotakiwa kufanya ni kujaza baadhi ya data ambazo ni muhimu ambazo zitasaidia app hiyo kuweza kufanya kazi jinsi inavyotakiwa.
2. Calorie Counter by FatSecret
Hii ni kati ya programu ambazo zimesha saidia watu wengi sana, app hii inauwezo wa kutambua chakula kwa kutumia kamera na kuonyesha kiasi cha lishe kilichoko kwenye chakula hicho pamoja na kukupa mpangilio wa nini ule na nini usile na kwa wakati gani.
1. Calorie Counter – MyFitnessPal
Kwenye namba moja hii ni moja kati ya app zenye uwezo mkubwa sana wa kukusaidia kiafya app hii ina uwezo wa kujua aina ya chakula huku ikiwa na uwezo wa kukupa ushauri wa chakula mazoeizi pamoja na mengine mengi.
Na hizo ndio programu ambazo ukizingati ushauri unapatika kwenye app hizo basi na uhakika utaweza kupunguza uzito wako kwa haraka sana, app hizi pia zinapatikana kwenye mifumo ya iOs cha msingi ingia Apple Store kisha tafuta jina na angalia picha ya app wakati unataka kudownload ili kupata uhakika.
Kujua app zingine zinazoweza kukusaidia kwenye afya yako tembelea ukurasa huu endelea kutembelea Tanzania Tech kujua zaidi, pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka zaidi.