WhatsApp Kuleta Sehemu Mpya ya “Share Live Location”

Sasa WhatsApp na Facebook zote zinayo sehemu ya Share Live Location
WhatsApp Share Live Location WhatsApp Share Live Location

Hivi karibuni watumiaji wa programu ya WhatsApp wataweza kushirikiana sehemu walizopo mubashara kabisa kupitia kwenye ramani ndani ya programu WhatsApp.

WhatsApp imetangaza rasmi hapo jana kuwa sehemu hiyo mpya itawawezesha watumiaji kuweza kushirikiana sehemu walizopo kwenye ramani kwa kutumia sehemu hiyo mpya ambayo itapatikana kwenye sehemu ya attachment (ile sehemu kama unataka kutuma picha) na kama utakuwa ume update app yako utaona sehemu mpya ya “Share Live Location”.

Tofauti na sehemu iliyoko kwenye programu ya Facebook, Sehemu hii mpya ya “Live Location” itakuruhusu kushirikiana sehemu uliyopo kwenye ramani kwa muda wa masaa 8 na vilevile Mtumiaji wa sehemu hiyo ataweza kuchagua ni muda gani anataka kuonekana kwenye ramani pamoja na idadi ya watu unaotaka waone mahali ulipo kwenye ramani.

Advertisement

Sehemu hiyo inakuja hivi karibuni na tayari imesha anza kutoka kwenye baadhi ya nchi, kama bado hujapata sehemu hii kwenye programu ya WhatsApp hakikisha una-angalia update za programu hizo kupitia Play Store kwa Android na App Store kwa iOS.

Kwa habari zaidi za Teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech nasi tutakujuza yote mapya kwa upande wa teknolojia, pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote kwa haraka zaidi.

Chanzo : TechCrunch

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use