Ukweli : Njia za Kupata Pesa Kupitia Google Adsense (Tanzania)

Unataka kuanza kutengeneza pesa kupitia Google Adsense, soma hapa
Ukweli : Njia za Kupata Pesa Kupitia Google Adsense (Tanzania) Ukweli : Njia za Kupata Pesa Kupitia Google Adsense (Tanzania)

Ni wazi kuwa siku hizi vijana hasa hapa kwetu Tanzania wameamka na wanapambania fursa mbalimbali kwa umakini wa hali ya juu. Fursa hizo ni pamoja na biashara mtandaoni au kama ambavyo wengi wetu hupenda kusema pesa mtandaoni.

Kwa wengi wenu najua unaposikia neno pesa mtandaoni au biashara mtandaoni basi lazima utawaza baadhi ya huduma kama vile YouTube, au Kuwa na Programu ya iOS na Android au pengine tovuti (Website) ambayo unaweza kuweka matangazo ya Google na kuendelea kutengenza pesa mtandaoni, lakini yapo mambo mengi sana yanayoweza kukusaidia kutengeneza pesa mtandaoni zaidi ya hayo.

Lakini hebu tufanye hiyo ni topic ya siku nyingine na leo hebu tuongele kidogo kuhusu njia za kutengeneza pesa mtandaoni kupitia Google Adsense. Bila kupoteza muda hebu twende moja kwa moja kwenye makala hii.

Advertisement

Google Adense ni nini

Kwanza tuanzie mbali kidogo, kama wewe ni mgeni lazima unajiuliza Google Adsense ni nini..? Adsense au Google Adsense hii huduma ambayo inatolewa na Google kwajili ya wabunifu wa mauthui mtandaoni pamoja na wabunifu wa programu na tovuti kuweza kupata pesa kutokana na kazi zao. Hapa napo sema kazi na maana kutengeneza video, kutengeneza makala au kutengeneza programu mbalimbali zenye maudhui.

Huduma za Google na Google Adsense

Kama tunaongelea maswala ya pesa mtandaoni basi ni vyema kujua huduma za Google ambazo zinaweza kukusaidia kupata pesa mtandaoni kupitia Google Adsense, huduma hizi zipo tofauti lakini zote zimeunganishwa na huduma ya Google Adsense, hivyo haijalishi utachagua huduma gani kati ya hizo zote ni huduma zilizo unganishwa na Google Adsense.

  • YouTube
  • Blogger
  • Google Admob
  • Google Ads (Tovuti Binafsi)

Kama unavyoweza kuona, njia zote hizi ni tofauti lakini zote zinakuhitaji kuwa na akaunti ya Google Adsense hivyo ni muhimu sana kuwa na akaunti ya Ansense kabla ya kuanza kufanya hatua za kupata pesa mtandaoni kupitia huduma yoyote kati ya hizo, baadae nitakwambia ni kwanini.

YouTube

Sasa labda tuanze na YouTube, Youtube ni sehemu ambayo inakuruhusu kuweka video zenye maudhui ambayo yanakubalika na jamii ambayo inakuzuka na kupitia video hizo unaweza kupata pesa kutokana na matangazo ambayo yanakuwa yanapita mara kabla ya video zako kuanza, katika ya video zako au mara baada ya video zako kuisha.

Kiujumla Ili kupata pesa kupitia YouTube unahitaji kufikisha kiwango fulani cha wafuasi wa channel yako, ikiwa pamoja na kiasi cha ujumla cha muda ambao video zako zote zimetazamwa ndani ya kipindi cha muda wa mwaka mmoja, yaani ni sawa na kusema unahitaji kiwango fulani cha views na subscriber ili kuweza kufikia hatua ya kufanya maombi ya kujiunga na Google Adsense kwa njia ya YouTube.

Jinsi ya Kupata Pesa Kupitia YouTube

Kama wewe upo Tanzania basi hii ni kwajili yako, kama unataka kupata pesa kupitia YouTube basi ni vyema kuhakikisha unatengeneza video zenye maudhui na zenye kupendwa na watazamaji zaidi. Hii ni muhimu sana hasa pale unapokuwa unaanza. YouTube huangalia zaidi video inayo tanzamwa zaidi kuliko kiasi cha subscriber, hivyo kama video zako zinaangaliwa zaidi basi nafasi ya kupata pesa kupitia YouTube ni kubwa zaidi, unaweza kusoma zaidi hapa.

Ukweli

Lakini pia hapa ni lazima nikueleze Ukweli, ili kupata views nyingi kwenye channel yako au video zako ni lazima kutumia njia halali na kutengeneza video zinazo angaliwa zaidi na zenye lugha bora ya matangazo ambayo ni Kingereza (English). Najua utakuwa umeshangaa sana lakini hapa leo inabidi nikueleze ukweli. Kama unayo video ya kiswahili yenye views nyingi au yenye uwezo wa kuangaliwa zaidi ya mara 100,000 ndani ya wiki moja basi unaweza kupata pesa kutokana na aina ya video uliyo tengeneza.

Lakini kama unayo video ya kingereza yenye uwezo wa kuangaliwa na watu wa nje ya Tanzania na kufikisha views zaidi ya 10,000 ndani ya wiki moja basi na kuhakikishia hapa unaweza kupata pesa inayo eleweka sana. Kifupi ni kwamba Video za maudhui ya Kiswahili ni ngumu sana kukubalika kimatangazo kwani kampuni nyingi sana zinazofanya kazi ya kutangaza biashara zao kupitia Google zipo nje ya Tanzania na nyingi zinatumia lugha za Kingereza.

Kwa hiyo basi kama leo hii unataka kupata pesa kupitia YouTube unaweza kujaribu kutengeneza video za Kiswahli ambazo zinaangaliwa sana, au tengeneza channel ya Kingereza yenye video zenye kuongea kwa lugha ya kingereza. Pia hakikisha unaweka video mara kwa mara hii ni muhimu sana hata kama unayo channel ya kingereza, kifupi Content is a King.

Blogger

Blogger ni mtandao ambao unaruhusu watumiaji kuweza kutengeneza tovuti ambazo zinakuwa na kiunganishi au domain za blogspot.com na zinakuwa hosted na kwenye servers za Google. Kwa upande wa kutengeneza pesa kupitia blogger, hii haina tofauti kabisa na kuwa na Channel ya YouTube kwani pia kupitia blogger unaweza kupata kiasi fulani cha pesa kutokana na matangazo ya Google unayoweza kuweka kwenye tovuti yako ya blogger.

Jinsi ya Kupata Pesa Kupitia Blogger

Sasa ili kupata pesa kupitia blogger ni vyema kujua machache yafuatayo, kupitia blogger ni lazima kuandika maudhui yenye kukubalika na jamii na yaliyopo kwenye lugha bora ya matangazo ambayo ni Kingereza. Sasa hapa zingatia neno lazima kwani kupitia blogger kama unaweka maudhui ya Kiswahili basi hutoweza kupata pesa kabisa kuitia Adsense kwani Google kupitia huduma yake ya Google Adsense bado haina lugha ya kiswahili kama lugha inayo kubaliwa na kampuni zinazotoa matangazo kupitia Google.

Ukweli

Sasa tuje kwenye ukweli, kama unafikiria kuanzisha blogger kwa lugha ya Kiswahili basi hakikisha kuwa unaondoa mawazo ya matangazo ya Google Adsense kwa sasa, kwani hadi sasa Google haikubali tovuti za Kiswahli isipokuwa tovuti maarufu sana zilizo chaguliwa na Google na ambazo pia sio kila wakati zitakuwa zinaonyesha matangazo pia tovuti hizo ni lazima ziwe hazina kiunganishi cha blogspot.com.

Google Admob

Tukija kwenye Google Admob, hii ni huduma ya Google ambayo inawaruhusu wamiliki na wabunifu wa programu mbalimbali za Android na iOS kuweza kupata pesa kupitia Programu zao. Unaweza kupata pesa kupitia matangazo ambayo yanaonekana ndani ya App husika kupitia sehemu maalum.

Jinsi ya Kupata Pesa Kupitia Admob

Tofauti na huduma nyingine, kwa upande wa Admob mambo sio marahisi lakini pia kuna afadhali kwa wabunifu wa programu wa hapa Tanzania. Kupia programu zako mbalimbali unaweza kupata pesa kwa kuweka maudhuli yanayo kubalika na jamaii iliyokuzunguka na yaliyopo kwenye lugha yoyote inayotumiwa na watu hao.

Ukweli

Sasa ili kuweza kupata pesa kwa kutumia Admob kwanza unatakiwa kuwa mbunifu mzuri wa programu za Android au iOS, pia hakikisha unapata watumiaji wengi wa programu zako pamoja na maudhui mazuri ambayo watumiaji wa programu hiyo wanaweza kupendelea. Kupitia Admob unaweza kupata pesa endapo watu wengi wanatumia programu yako au unazo programu nyingi kupitia masoko ya Play Store na App Store. Kifupi ni kuwa unahitaji kutengeneza app inayopendwa na kupakuliwa na watu wengi zaidi ili kupata pesa, angalau app itakapofikisha watumiaji zaidi ya 100,000 basi utaweza kuona matokeo mazuri zaidi kiasi.

Sasa hapa ndio hatua ya mwisho ambayo pia sio tofauti na hatua ya Blogger iliyopo hapo juu. Huduma hii ya matangazo ya google ads kupitia tovuti binafsi inatofautiana na blogger kwa sehemu ndogo kwani hutogawana kiasi kikubwa cha mapato na Google kama inavyokuwa mtu anayetumia blogspot.com.

Jinsi ya Kuapata Pesa Kupitia Google Ads (Tovuti Binafsi)

Kama unataka kupata pesa kwa kutumia tovuti binafsi basi ni muhimu kufuata vigezo na masharti ya kuandika maudhui yenye kukubalika na jamii ikiwa pamoja na lugha bora ya matangazo ambayo ni… najua unajua je unataka nikujuze zaidi…. Kingereza.

Ukweli

Kama unafikira kuwa na tovuti ya Kiswahili, yani kama Tanzania Tech, basi ni vyema kwa sasa ukasahau kuhusu matangazo ya Google Adsense kwani hadi sasa Google hawakubali tovuti zenye maudhui ya kiswahili.

Hitimisho

Sasa baada ya kusema yote hayo labda tuhitimishe kwa kusema haya, kama unayo tovuti au channel ya Youtube yenye maudhui ya kiswahili unahitaji kuhakikisha unapata waangaliaji wengi wa video zako kama ni YouTube au kama ni tovuti basi hakikisha una angalia vyanzo vingine vya mapato kama kuwa na programu kwaajili ya tovuti yako. Pia kama wewe ni blogger mawazo yangu kwako ni hayo hayo kwani ukweli ni kwamba Lugha ya Kiswahili bado mtandaoni haitumiki kwa asilimia kubwa na makampuni yenye uwezo wa kutangaza biashara mtandaoni.

Kama umefanikiwa kusoma hadi hapa badi unastahili zawadi na ukweli nakwambia umeonyesha nia ya dhati ya kuanza kufanya biashara mtandaoni, unaweza kusoma hapa kuangalia jinsi ya kuanza biashara mtandaoni kwa mtaji wa Tsh 70,000 tu. Kwa kuwa umeonyesha uaminifu mkubwa basi hii hapa ni zawadi yangu kwako.

Zawadi Yangu Kwako

Kama unafikiria kuwa na tovuti au app au YouTube Channel hapo baadae, basi pia ni vizuri kutengeneza akaunti ya Google Adsense mapema kwanza hata kama hujafikira kuweka matangazo kitu chochote. Hii ni muhimu kwani akaunti zilizotengenezwa muda mrefu huwa zina aminika zaidi kuliko akaunti ambazo zimetengenezwa na kuanza kuomba matangazo moja kwa moja hizi hua mara nyingi zinafungwa baada ya muda mfupi sana na pengine pesa kuzuiliwa.

7 comments
  1. Amani Joseph nakukubali bingwa wangu, wewe ndo kioo cha watanzania wenye ndoto hizo nikiwepo na mimi. Niko mbioni kwa shughuli dam dam kama kwasasa am studying computer languages kupitia source mbalimbali nimeanza na html you may advice me by any means….. I always appreciate you ?…..

  2. Asante sana kwa makala haya ya kufudisha jamii haswa sisi vijana wa sasa. Ningependa kukurebeshisha kwenye kipengele cha ‘google ads’ na ‘google adsense’.
    Google ads(advertiser) ni kwa ajili ya watu wanaotaka kutangaza bidhaa na huduma zao mtandaoni na ambapo Google Adsense(publisher) ni kwa ajili ya wale wanaotaka kupata kipato kupitia mtandao, yaani wanomiliki ‘blogs’ na ‘websites’.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use