Jinsi ya Kuanzisha Biashara Mtandaoni Kama Kupatana.com

Anza biashara yako mtandaoni kama ilivyo kupatana.com
Jinsi ya Kuanzisha Biashara Mtandaoni Kama Kupatana.com Jinsi ya Kuanzisha Biashara Mtandaoni Kama Kupatana.com

Kama wewe ni msomaji wa muda mrefu kidogo basi lazima utakuwa unajua kuwa hapa Tanzania Tech tunapenda kujadili mambo kadhaa ambayo yanaweza kutusaidia sisi vijana kwa namna moja ama nyingine. Kama bado hujawahi kukutana na mada kama hii basi naomba nikukaribishe sana.

Kwa siku ya leo nimekuletea njia rahisi ambayo unaweza kuitumia kwa namna moja ama nyingine kuweza kuanza biashara yako mwenyewe mtandaoni, biashara ambayo inafanana kabisa na biashara inayofanywa na tovuti maarufu hapa Tanzania ya Kupatana.com

Jinsi ya Kuanzisha Biashara Mtandaoni Kama Kupatana.com

Advertisement

Na uhakika watu wengi mnajua tovuti ya kupatana.com hivyo sitopoteza muda mwingi kuelezea hilo bali nitaenda kwenye mada moja kwa moja. Sasa kama wewe ni mmoja wa watu ambao walikuwa na ndoto za kuanzisha biashara kama ilivyo biashara ya kupatana basi nafasi hii ni yakwako.

Naitambulisha kwenu LOKO buy & Sell, Hii ni app ambayo inafanana na kupatana.com kwani inakupa nafasi ya kuweza kuanza biashara kubwa ya kuuza na kununua mtandaoni na kuwa mmiliki wake kwa asilimia 100. Kwa kununua app hii na kuifanya iwe ya kwako utaweza kuanza biashara hii ambayo na uhakika itakupa faida kama ukizingatia na kutangaza biashara yako.

Nini Unahitaji

Unachotakiwa ni kununua app hii kutoka kwetu na pale utakapo inunua tutakusaidia kuifanya iwe ya kwako kwa asilimia 100 kwa kuweka rangi yako, logo yako pamoja na jina la app yako tayari kwa wewe kuanza kuingiza pesa mtandaoni. Huna haja ya kuwa na kompyuta ili kutengeneza app hii bali sisi tutakusaidia kutengeneza kila kitu kwa ajili yako ili kurahisisha wewe kuanza biashara yako kwa haraka zaidi.

Mahitaji Mengine Muhimu

Pamoja na kununua app hii kutoka kwetu kuna mahitaji mengine ambayo ni muhimu sana ili kuweza kuanza biashara hii, mahitaji hayo ni pamoja na

 • Domain pamoja na hosting – Hivi vyote unaweza kuvipata kwa bei nafuu sana kwa takribani jumla ya shilingi 35,000 unaweza kupata domain pamoja na hosting kupitia Godaddy.
 • Unahitaji akaunti ya Google Play ili kuweka App hiyo, kama huna tunaweza kusaidia kuweka app hiyo play store kwa gharama nafuu.
 • Unahitaji kuwa na akaunti ya Google na akuanti ya Facebook
 • Unahitaji kuwa na Logo kwa ajili ya App yako (Tunaweza kutengeneza kwa gharama nafuu)
 • Na mambo mengine ya kawaida ambayo…

Uwezo wa App

Jinsi ya Kuanzisha Biashara Mtandaoni Kama Kupatana.com

Sasa kama wewe unataka kwanza kujua app hii inauwezo gani basi ngoja nikwambie angalu kwa ufupi ili kusudi ujue ni kitu gani unafikiria kununua. App hii inauwezo mkubwa zaidi ya app ya kupatana.com ambayo unaifahamu na kutumia sana, kwa kuanza hayapa hapa ni baadhi tu ya mambo hayo.

 • Unaweza kuruhudu watu kweka matangazo ya kuuza pamoja na kununua
 • Unaweza kuruhusu watu kununua vifurushi kwa njia ya simu vifurushi ambavyo vitafanya matangazo yao kuonekana kabla ya matangazo ya watu wengine.
 • Utaruhusu watu ku-upload picha za bidhaa na utaweza kuchagua idadi ya picha unazotaka watu waweke, pia picha hizo zinzuwezo wa kuwekewa alama kama ile ya kupatana.com inayokuwa katikati ya picha.
 • Utaruhusu watumiaji kuweza kutengeneza akaunti kwa kutumia Google au Facebook
 • Utaruhusu watu kuuza vitu kwa kufanya mnada yaani watu wataweza kushindania bei na atakaye toa pesa nyingi zaidi ana nunua bidhaa.
 • Na mambo mengine mengi..

Unacho takiwa kufanya unaweza kupakua app hii kupitia soko la Play Store kisha angalia vitu vyote vinavyopatikana ndani ya app hiyo ndivyo ambayo app yako itakavyokuwa.

Upatikanaji na Bei

Jinsi ya Kuanzisha Biashara Mtandaoni Kama Kupatana.com

Sasa baada ya maongezi hayo marefu habu tuje kwenye upande wa bei, Unaweza kupata app hii kwa bei mbili tofauti na zote zimeeleza kupitia hapa.

 • App pekee yenye kufanya kazi kabisa – Tsh 100,000 Hapa utapata app yenye uwezo wa kufanya kazi kwa asilimia 100 lakini itakuwa ni app pekee. (kumbuka gharama hizi hazihusiani na gharama za kununua domain, hosting au gharama nyingine zozote).
 • App pamoja na website – Tsh 200,000 Hapa utapata app pamoja na website yake na utaweza kuunganisha vyote kwa pamoja na kuanza biashara yako kwa haraka. (kumbuka gharama hizi hazihusiani na gharama za kununua domain, hosting au gharama nyingine zozote).

Baada ya kulipa pamoja na kukubaliana unaweza kupata App yako ndani ya siku moja kama utanunua app pekee na kwa wiki moja kama utanunua app pamoja na website. Kumbuka malipo yanafanyika kabla ya kazi hivyo ni vyema kufanya makubaliano kabla ya kazi kuanza. Unaweza kuwasiliana nasi hapa kama unataka app hii au kama una maswali zaidi.

6 comments
 1. Nimeona maelezo apo juu kuihusu app yenu lkn bado kuna v2 sijaelewa je kwenye kuiendesha INA hitaji watu wangapi na unanufaika je nayo?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use