Kampuni ya Google kupitia mtandao wake wa YouTube mapema leo imetangaza utaratibu mpya ambapo sasa hutoweza kuonyesha matangazo kwenye channel yako kama channel yako haijafikisha views elfu kumi (10,000) na kuendelea.
Kwa mujibu wa post iliyoko kwenye blog ya Youtube utaratibu huo mpya umekuja baada ya ongezeko la channel au akaunti zenye kuiba video kutoka channel zingine kwa lengo la kujipatia kipato kwa haraka. Hata hivyo sheria hiyo imekuja wakati kampuni hiyo ikiwa kwenye kipindi kigumu kutokana na kupata hasara kubwa baada ya baadhi ya makampuni makubwa ambayo hufanya matangazo kupitia mtandao huo kujitoa kwa kile kinacho semekana kuwa matangazo yao huonyeshwa kwenye video zisizo na maadili na zenye kuvunja haki za binadamu.
Hivyo basi kuanzia wiki ijayo kati ya Jumatano na Alhamisi channel zote za YouTube zenye views chini ya elfu kumi (10,000) zita ondolewa matangazo mpaka hapo zitakapo fikia kiwango hicho cha views, YouTube huwa inahesabu views moja (1) kila baada ya mtu anapo angalia video kwa muda wa sekunde zaidi ya thelathini (30). Vilevile YouTube imetangaza kuboresha zaidi sheria zake za (YouTube Partner Program) pale unapokuwa unaomba matangazo hivyo sasa channel yako itabidi kupitiwa kwanza mara kadhaa kabla ya kuruhusiwa kuonyesha matangazo.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.


