Jinsi ya Kujua Taarifa zako Zinazokusanywa na Facebook

Hizi hapa ndio data ambazo facebook wanakusanya kuhusu wewe
Jinsi ya Kujua Taarifa zako Zinazokusanywa na Facebook Jinsi ya Kujua Taarifa zako Zinazokusanywa na Facebook

Katika hali ya kawaida, Data au taarifa za mtu binafsi sasa ni biashara kubwa sana duniani ambayo ndio uti wa mgongo wa makampuni makubwa kama vile Google, Twitter, Facebook, Instagram, YouTube na mitandao mingine mikubwa duniani.

Hapa tuelewane, naposema “taarifa za mtu binafsi” sina maana taarifa za siri bali hapa nina maana taarifa zile za kawaida ambazo umetoa ruhusa kwa makampuni kuzichukua na kuzitumia kwa maslahi ya kibiashara.

Taarifa hizo zinaweza kuwa tofauti kulingana na biashara inayo fanywa na kampuni au mtandao husika, kwa mfano kwa Facebook taarifa zinazoweza kuchukuliwa ni pamoja na tovuti gani unatembelea zaidi au pia bidhaa gani umenunua mtandaoni pamoja na data nyingine nyingi ambazo sio za siri.

Advertisement

Sasa hivi karibuni kampuni ya Facebook imetangaza kuja na sehemu mpya kabisa ambayo itakuwa inasaidia watumiaji kujua ni data gani au taarifa gani ambazo Facebook inakusanya kutoka kwa watu binafsi nje ya mtandao wa Facebook. Yaani kwa kifupi ni sawa na kusema facebook imekuja na sehemu ambayo itakuwezesha kujua ni vitu gani facebook inajua kuhusu wewe pale unapokuwa hautumii mtandao wa Facebook. Sehemu hiyo inaitwa off-Facebook activity.

Nini Maana ya Off-Facebook Activity

Kama ulivyo sikia kwenye video hapo juu, off-facebook activity ni vile vitu unavyofanya nje ya facebook na ambavyo data zake zinakusanywa na facebook kutoka kwenye tovuti mbalimbali kwenda kwa facebook kwa ajili ya kuonyesha matangazo. Data hizo zinaweza kuwa ni vitu gani umenunua au umeangalia kwenye tovuti gani pamoja na mambo mengine kama hayo.

Jinsi ya Kujua Taarifa Hizo

Sasa kwa ufupi kabisa ili kujua taarifa hizo zinazo kusanywa na facebook kutoka kwenye tovuti mbalimbali, unatakiwa kutembelea ukurasa huu, kisha baada ya hapo hakikisha unaingia kwenye akaunti yako ya Facebook kwa kutumia username na password yako kisha bofya sehemu ya icon kama inavyo onekana kwenye picha hapo chini.

Jinsi ya Kujua Taarifa zako Zinazokusanywa na Facebook

Baada ya hapo utaweza kuona taarifa za tovuti pamoja na app ulizo tembelea ambazo facebook inafahamu, ikiwa pamoja na baadhi ya huduma ambazo umetumia kama Tigo Pesa App na huduma nyingine ambazo facebook inafahamu kuwa umetumia. Najua inashtua lakini ndio ulimwengu wa teknolojia huo….!

Jinsi ya Kujua Taarifa zako Zinazokusanywa na Facebook

Kama unavyoweza kuona hapo juu picha ya mwisho kulia, utaweza kuona app na website zote ulizo tumia kwa urahisi na haraka. Kitu kizuri ni kuwa unaweza kufuta data hizi ili kuzuia facebook kutumia data hizo kuonyesha matangazo kwenye akaunti yako ya Facebook au Instagram.

Jinsi ya Kufuta Data Zako

Ili kufuta data zako hizo unacho takiwa kufanya ni kubofya sehemu ya Clear history inayo onekana juu kwenye list ya app na website ambazo umetumia. Kumbuka kufuta data hizo hakuta zuia facebook kuonyesha matangazo bali utaweza kuona matangazo ambayo hayalingani na data zako.

Kwa sasa hayo ndio mambo ambayo kwa sasa inakuruhusu kujua kuhusu wewe, kumbuka hizi ni sehemu tu ya data au kama facebook wanavyosema hii ni “summary” ya data wanazojua kuhusu wewe. Kumbuka hatua hii imekuja baada ya sakata la Cambridge Analytica, ambapo data za watumiaji zaidi ya milioni 10 wa mtandao wa Facebook zilisemekana kuvuja na kutumia kwa ajili ya uchaguzi wa marekani mwaka 2016.

Hata hivyo Facebook imeahidi kuleta sehemu nyingine nyingi ambazo zitasaidia watumiaji kujua ni data gani ambazo facebook inakusanya ili kuweza kuonyesha matangazo kwenye mitandao yake.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use