Tumia Android Kwenye Kompyuta Bila Ku-install

Utaweza kutumia mfumo wa Android kwenye kompyuta yako ya PC
Tumia Android Kwenye Kompyuta Bila Ku-install Tumia Android Kwenye Kompyuta Bila Ku-install

Ni kweli kwamba kuna baadhi ya watu hadi sasa bado hawana simu za mfumo wa Android, hii inatokana na baadhi ya watu hao kutumia simu za mfumo wa iOS na hivyo kukosa mengi yanayo endelea kwenye mfumo wa Android.

Lakini huna haja ya kukosa chochote kwani siku ya leo nitaenda kuonyesha hatua kwa hatua jinsi ya kutumia mfumo wa Android kwenye kompyuta yako bila kuinstall mfumo huo kwenye kompyuta yako. Kitu cha muhimu ni kujua kuwa ni lazima ku-install mfumo huo pembeni tofauti na kwenye kompyuta yako ili kuweza kutumia mfumo huo pale unapo hitaji.

Mahitaji

  • Unahitaji kuwa na USB Flash angalau GB 2
  • Unahitaji kuwa na Internet angalau GB 1.5 au zaidi
  • Unahitaji kuwa na kompyuta inayotumia mfumo wa Windows, kuanzia Windows 7, 8 na 10.

Hatua za Muhimu

  • Kitu cha kwanza unacho takiwa kufanya ni kutembelea tovuti hii hapa, kisha download mfumo wa Android moja kwa moja kwenye kompyuta yako. Bofya Hapa Kudownload
  • Baada ya hapo tembelea tovuti ya Rufus kisha pakua mfumo wa rufus, mfumo huu unakusaidia kuweza kutengeneza File za mfumo ambazo zipo booted.
  • Chomeka USB Flash kisha baada ya hapo washa programu ya Rufus kama Administrator, kisha chagua USB flash uliyo chomeka kutoka kwenye kompyuta yako kwa kuchagua kwenye list ya (Device) inayo onekana juu upande wa kushoto.
  • Baada ya hapo chini kwenye (Boot selection) bofya kitufe cha Select kilichopo upande wa kulia kisha chagua mahali ulipo hifadhi file la Android ulilo pakua kwenye hatua ya kwanza. Bofya open kuweka file hilo kwenye programu ya Rufus.
  • Baada ya kuhakiki hatua zote zime enda sawa, sasa moja kwa moja bofya Start na subiri baada ya muda mfupi programu ya Rufus itakuwa imemaliza.
  • Baada ya hapo funga programu ya Rufus pia hakikisha una restart kompyuta yako na chagua boot kwa kubofya F12 au ESC kwenye kompyuta yako kisha chagua jina la Flash yako.
  • Subiria utaona mfumo wa Android utaweza kuwaka moja kwa moja kupitia kwenye Flash yako. Hongera sasa utaweza kutumia Android kwenye kompyuta yako bila kuintsall mfumo huop kwenye kompyuta yako.

Advertisement

Kama unataka kujifunza zaidi soma hapa kujua jinsi ya kutumia simu yako ya Android kwenye kompyuta kwa haraka sana. Kwa maujanja zaidi hakikisha unatembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia YouTube hapa.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use