Je nini Maana ya Fast Charging Kwenye Smartphone

Elewa zaidi kuhusu teknolojia ya Fast charing kwenye simu yako
Je nini Maana ya Fast Charging Kwenye Smartphone Je nini Maana ya Fast Charging Kwenye Smartphone

Mara kwa mara nimekuwa nikipata maswali kutoka kwa watu, Je nini maana ya Fast Charging kwenye smartphone..?. Kwa kuwa nahisi wengi wenu pia mnapenda kujua, hivyo basi leo nimeandaa makala fupi kwa ajili ya kujibu swali hili pamoja na maswali mengine kuhusu fast charging.

Kupitia makala hii utaenda kufahamu nini maana ya Fast Charging, na pia utajuaje kama simu yako inakuja na teknolojia hiyo, pia mbali na hayo nitaenda kujibu baadhi ya maswali ambayo yamekuwa yakiulizwa na watu wengi kuhusu teknolojia hii ya Fast Charging. Basi bila kupoteza muda zaidi twende moja kwa moja kwenye makala hii.

Je nini Maana ya Fast Charging Kwenye Smartphone

Advertisement

Nini Maana ya Fast Charging

Kwa ufupi kabisa, kama jina la teknolojia hii linavyo jieleza, Fast charging ni teknolojia ambayo inawezesha battery ya simu yako kujaa kwa haraka na kwa muda mfupi. Teknolojia hii huwezeshwa kwenye baadhi ya simu na vifaa vingine na ili kusudi battery ya simu yako iweze kuchajiwa kwa haraka, simu yako inatakiwa iwe imetengenezwa ikiwa na teknolojia hiyo.

Kuwa na chaja pekee yenye uwezo wa Fast charging hakuta saidia simu kujaa haraka bali simu nayo inatakiwa kuwa na teknolojia hiyo.

Chaja ya Fast Charging Inafanyaje Kazi

Mara nyingi kiasi cha umeme kinacho tolewa na chaja ya simu yako kinapimwa kwa amperage pamoja na voltage. Amperage ni kiasi cha umeme kinachotoka kwenye battery ya simu yako kwenda kwenye simu yako lakini voltage ni kiasi cha ukubwa wa umeme baina ya point mbili, sasa ukichukua kiasi cha umeme au voltage ukazidisha Amperage ndio unapata wattage, wattage ndio kipimo cha uwezo wa chaja yenye uwezo wa fast charging.

Kampuni nyingi zinazo tengeneza chaja zenye uwezo wa teknlojia ya fast charging, huongeza kiwango cha voltage ili kufanya simu iweze kujaa haraka zaidi. Mara nyingi chaja zenye uwezo wa fast charging hutoa kiasi kikubwa cha voltage kuliko chaja za kawaida, lakini pia chaja hizo huwa na uwezo wa kutoa kiasi cha kawaida cha umeme pale zinapotumika kwenye simu ambazo hazina teknolojia ya Fast Charging, Vilevile chaja hizo hutoa kiasi kikubwa cha umeme pale zinapokuwa zinatumika kwenye simu zenye teknolojia ya Fast Charing.

Je nini Maana ya Fast Charging Kwenye Smartphone

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, chaja hiyo ya Xiaomi inakuja na teknolojia ya Fast Charging hivyo inao uwezo wa kutoa kiasi cha voltage kuanzia Volt 5 ambacho hichi ni kiasi cha kawaida cha chaja yoyote ya smartphone. Kwa upande mwingine chaja hiyo pia inaweza kutoa kiasi cha voltage hadi 12, kiasi ambacho hichi ni kiwango cha chaja yenye teknolojia ya Fast Charging.

Fast Charging Inavyofanya Kazi Kwenye Simu Yako

Mbali na chaja, ni lazima pia simu yako iwe imetengenezwa kwa teknolojia ya Fast Charging. Teknolojia hii ndio inayo battery ya simu yako kuweza kupokea chaji kwa haraka kwa voltage nyingi zaidi kuliko zile za kawaida. Kwa mfano chaja za Fast Charging za Samsung huwa zimeandika 9.0v= 1.67A or 5.0v = 2.0 A hii ni sawa na kusema chaja hii inauwezo wa kutoa Volt 9.0 kwa simu zenye uwezo wa Fast Charging na Volt 5.0 kwa simu zenye uwezo wa kawaida.

Je nini Maana ya Fast Charging Kwenye Smartphone

Sasa simu yenye teknolojia ya Fast Charging ndio inayoweza kutambua kama chaja hii inaweza kutoa kiasi cha zaidi cha volt (Volt 9.0), lakini simu ambayo haina teknolojia ya Fast Charging haiwezi kutambua kama chaja inauwezo wa kutoa Volt zaidi hivyo huchajiwa kwa kutumia Volt za kawaida za chaja (Volit 5.0) ambazo pia hutolewa na chaja ya Fast Charing.

Hata hivyo ufanyaji kazi wa teknolojia ya Fast Charging hauishi hapo, wote tunajua kuwa kama kiasi kikubwa cha umeme kinapo ingia mahali basi joto huweza kuongezeka kwa kasi na kutokana na kuwa teknolojia ya Fast Charging huingiza umeme kwa kasi kwenye battery ya simu husika basi hapa ndipo utalamu mwingine hutumika ili kuepusha joto kali kwenye battery.

Mara nyingi chaja za Fast Charing huchaji simu yako kwa Volt zaidi pale simu yako inapokuwa na chaji chini ya asilimia 50 au 70, pale simu yako inapokuwa na chaji zaidi ya asilimia 50 au 70 simu yako huendelea kupokea chaji kwa voltage za kwaida (Volt 5.0) kama ilivyo simu nyingine za kawaida ambazo hazina teknolojia hiyo. Hii husaidia battery kutopata joto kali na hatimaye kulipuka.

Utajuaje Kama Simu Yako Inayo Teknolojia ya Fast Charing

Mara nyingi simu huwa haziandikwi kama zinakuja na teknolojia ya Fast Charging, njia rahisi ya kuweza kujua kama simu yako inakuja na teknolojia hiyo ni kusoma vitabu maalum vinavyokuja na simu yako au kuangalia kama chaja inayokuja na simu yako imeandika Fast Charging au Quick Charging au maneno yoyote ya kuashiria kama chaja hiyo inauwezo wa kuchaji simu yako kwa haraka. Pia wakati mwingine box la simu linakuwa limeandika.

Kwa upande wa simu za Samsung unatakiwa kuingia kwenye Settings > Divece Maintance > Bofya Battery > alafu bofya mishale mitatu juu upande wa kulia utaona sehemu ikiwa imandikwa Fast cable charging, Washa sehemu hiyo. Simu nyingine za Samsung unatakiwa kwenda Settings > Device care > Battery > More options > Settings > Fast cable charging. Kujua zaidi soma hapa.

Je nini Maana ya Fast Charging Kwenye Smartphone

Maswali Mengine

  • Je Chaja ya Fast Charging inaweza kuharibu battrey ya simu ya ambayo haina teknolojia hiyo.? – Hapana chaja ya fast charging haiwezi kuaribu simu ambayo haina teknolojia ya Fast charing kwani chaja ya mtindo huo inao uwezo wa kutoa Volt za simu yenye Fast Charing na Volit kwa simu ambayo haina Fast Charging.
  • Je ni muhimu kuwa na chaja yenye uwezo wa teknolojia ya Fast charing ili kuchaji simu yangu kwa haraka.? – Ndio ni muhimu sana kuwa na chaja yenye teknolojia ya Fast charing kwani simu yenye fast charing bila chaja yenye fast charing ni sawa na kuwa na simu ya kawaida.
  • Je ni muhimu kutumia kuwa na waya wa Fast Charing.? – Ni muhimu sana kuwa na waya unaokuja na chaja ya Fast charging kwani kuna simu nyingine ambazo hazifanyikazi kwenye upande wa fast charing bila kuwa na waya wenye uwezo wa kupitisha kiwango hicho cha umeme.
  • Je Fast charing hufanya kazi wakati simu ikiwa imewashwa au imezimwa.? – Simu nyingi hufanya kazi kwa pande zote mbili ila kama unataka simu ijae haraka zaidi hakisha unazima simu yako au unaweka Flight mode kama tulivyo onge kwenye makala iliyopita.
  • Je simu za TECNO zinayo teknolojia ya Fast charing.? – Ndio zipo baadhi ya simu za TECNO zenye teknolojia ya Fast charging, baadhi ya simu hizo ni pamoja na Tecno Phantom 8, Phantom 6 Plus, Camon CX, Phantom 6 na nyingine nyingi.

Hayo ni baadhi tu ya maswali ambayo yana ulizwa zaidi, kama unayo maswali zaidi hakikisha una uliza kupitia sehemu ya maoni hapo chini nami nakuahidi nitajibu maswali yako kwa wakati. Hadi hapo natumaini umeweza kuelewa kuhusu teknolojia ya Fast Charing, hasi siku nyingine tena endelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech ili uweze kujifunza zaidi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use