Apps Nzuri za Kudownload Nyimbo Mpya Kwenye Simu ya Android

Hii hapa ndio njia rahisi unayoweza kuitumia download nyimbo mpya
kudownload nyimbo mpya mp3 kudownload nyimbo mpya mp3

Ni mara nyingi sana watu huwa na uhitaji wa kupata nyimbo fulani, lakini sio mara zote unaweza kupata nyimbo hizi kwa kutafuta kwa kutumia Google. Kuliona hili leo nimekuletea list ya Apps nzuri ambazo unaweza kuzitumia download nyimbo mpya moja kwa moja kwenye simu yako ya Android.

Kumbuka Google hairuhusu app za namna hii kwenye soko la Play Store hivyo app hizi zote hazipo kwenye soko hilo na unaweza kudownload app hizi kwa kutumia link chini ya maelezo ya app husika. Basi baada ya kusema hayo, bila kupoteza muda let’s get to it…

Bongo Music Search

Kama wewe ni mpenzi wa nyimbo mpya na ungependa kupata nyimbo mpya kwa haraka basi app ya bongo music search ni app nzuri sana kwa ajili yako. App hii inakupa uwezo wa kutafuta nyimbo yoyote na kudownload hapo hapo bila kupoteza muda. Kingine kizuri kuhusu app hii ni kuwa haina matangazo hivyo unaweza kutumia kwa muda wowote unao hitaji, Pia unaweza kutumia tovuti hapa kama unatumia kompyuta

Advertisement

DOWNLOAD HAPA

New Pipe

New Pipe ni app nyingine nzuri ya kudownload nyimbo mpya kwa haraka, app hii inakupa uwezo wa kudownload video na audio na pia unaweza kuitumia kama app yako ya YouTube, App hii inakupa uwezo wa kufuatilia channel ya mtu bila ku-subscribe hivyo kama ulikuwa unataka hilo basi app hii ni bora sana kwako.

DOWNLOAD HAPA

Sky Tube

Skytube ni application nyingine ambayo unaweza kutumia kudownload nyimbo mpya, tofauti ya app hii na app nyingine kwenye list hii ni kuwa kupitia app hii utaweza kudownload video pekee na sio Audio kama zilivyo app nyingine zilizo tangulia. Kama unataka kudownload nyimbo mpya ambazo ni video mpya basi app hii ni nzuri sana kuwa nayo.

DOWNLOAD HAPA

SnapTube

Snaptube ni app nyingine nzuri sana kwa ajili ya kudownload nyimbo mpya, kwa kutumia app hii utaweza kudownload nyimbo mpya zikiwa kwenye mfumo wa Mp3 au Mp4. Uzuri wa app hii haina matangazo na inauwezo wa kufanya kazi kwa haraka zaidi pengine kuliko app zote kwenye list hii.

DOWNLOAD HAPA

Videoder

Videoder ni app nyingine nzuri ya kudownload nyimbo mpya kwenye simu yako ya Android. App hii inaweza kukupa uwezo wa kudownload MP3 na unaweza kudownload pia MP4. App hii ni rahisi sana kutumia na pia inaweza kudownload video kutoka kwenye tovuti nyingine mbalimbali, jaribu sasa app hii kwenye simu yako.

DOWNLOAD HAPA

Na hizo ndio app ambazo nimekuandalia kwa siku ya leo ambazo unaweza kutumia kudownload nyimbo mpya kwenye simu yako ya Android. Kumbuka apps hizi hazipo kwenye soko la Play Store hivyo ni vyema kujua vigezo na masharti ya kutumia app ambazo hazipo Play Store, pia kumbuka ni kinyume na sheria kudownload nyimbo bila kununua, kumbuka kuwa makala hii ni kwa ajili ya kujifunza hivyo ni vyema kuondoa nyimbo hizo kwenye simu yako mara baada ya kumaliza majaribio haya.

Kama unataka kujifunza zaidi na kujua apps nyingine nzuri basi unaweze kusoma makala yetu ya Apps nzuri za kusaidia kusoma meseji za mtu kwa ku-forward meseji zake kwenye simu yako, bofya hapa kuweza kujua apps hizo sasa, Pia kama unaona njia hii ya kudownload nyimbo mpya ni ngumu kwako unaweza kusoma njia nyingine hapa. Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use