Tahadhari kwa Watumiaji wa GB WhatsApp na WhatsApp Plus

Unaweza kufungiwa namba yako usipo badilisha programu hizi sasa
Tahadhari kwa Watumiaji wa GB WhatsApp na WhatsApp Plus Tahadhari kwa Watumiaji wa GB WhatsApp na WhatsApp Plus

Watumiaji wa programu za ziada za GB WhatsApp na WhatsApp Plus hivi karibuni wamepewa tahadhari juu ya utumiaji wa programu hizo kama mbadala wa programu halisi ya WhatsApp.

Kama ulikuwa hujui kuhusu programu hizo za GB WhatsApp na WhatsApp Plus, hizi ni programu ambazo zinakupa uwezo wa kutumia programu ya WhatsApp huku ikiwa na vitu zaidi ya vile vinavyopatikana kwenye programu halisi ya WhatsApp.

Programu zote za GB WhatsApp na WhatsApp Plus ni programu ambazo hazipatikani kupitia Play Store hivyo zinasemekana kuwa sio salama. Hata hivyo siku za karibuni watumiaji wengi wa programu ya WhatsApp wameonekana kutumia programu hizo ambazo zinawapa uwezo ikiwa pamoja na kubadilisha baadhi ya vitu kama rangi, Icon, kuzima last seen na vitu vingine vingi.

Advertisement

Kwa mujibu wa tovuti ya WhatsApp, WhatsApp imeanza kuchukua hatua kwa watumiaji wa programu hizo, huku ikiwataka kutumia programu halisi ya WhatsApp. Kupitia maelezo kwenye tovuti ya WhatsApp imeandikwa kuwa, kutumia programu hizo za ziada za WhatsApp kutafanya mtumiaji kufungiwa namba hiyo kwa muda pamoja na Chat au History kufutwa hata pale atakapo fanikiwa kurudi tena kutumia programu ya WhatsApp.

Hii sio mara ya kwanza kwa watumiaji wa programu za GB WhatsApp na WhatsApp Plus kufungiwa akaunti, kwani miaka ya nyuma watumiaji wa WhatsApp Plus walifungiwa namba zao na kutoruhusiwa kwa muda mrefu kutumia WhatsApp na namba zao, kitendo kilichofanya watu wengi kushindwa kutumia programu hiyo hata baada ya kurudi kutumia programu halisi ya WhatsApp.

Kwa mujibu wa maelezo ya WhatsApp, Kwa sasa kama umeshapata ujumbe wa kufungiwa akaunti yako basi unabudi kusubiri mpaka muda uliofungiwa kuisha, kisha ingia kwenye app ya GB WhatsApp, Kisha bofya More options > Chats > Back up chats. alafu ingia kwenye File manager yako tafuta file lililo andikwa GB WhatsApp, badilisha jina lake kisha andika WhatsApp.

Baada ya hapo ingia kwenye soko la Play Store kisha download app halisi ya WhatsApp, kisha baada ya ku-verify namba yako, ingia kwenye sehemu ya Restore > kisha bofya Next. Baada ya hapo chat zako zote zitarudishwa na utaendelea kutumia WhatsApp kama kawaida.

Kama bado hujafungiwa akaunti hakikisha unafanya hatua hizi na download app halisi ya WhatsApp mara moja kuepusha kufungiwa kwa muda namba yoko, kwani najua wengi wetu tunategemea app hiyo hata kwenye maswala ya biashara za kila siku.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use