Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

WhatsApp Kuja na Sehemu Mpya ya Kujua Kama Picha ni Feki

Sasa utaweza kujua kama picha uliyotumiwa ni Feki au Original
WhatsApp Kuja na Sehemu Mpya ya Kujua Kama Picha ni Feki WhatsApp Kuja na Sehemu Mpya ya Kujua Kama Picha ni Feki

WhatsApp inaendelea kufanya maboresho ya app yake kila siku, na hivi karibuni moja ya maboresho yanayo tegemewa kuja kwenye app hii ni pamoja na sehemu mpya ya kusaidia kujua picha feki ambazo huwenda umetumiwa na ndugu jamaa au marafiki.

Kwa mujibu wa tovuti ya Wabetainfo, Sehemu hii mpya ambayo sasa iko kwenye programu ya majaribio ya WhatsApp Beta, inakuwezesha kujua picha feki kwa kupeleka picha yoyote unayotumiwa moja kwa moja kwenye mtandao wa Google Image kwa ajili ya kutafuta kama picha hiyo uliyotumiwa imechukuliwa kwenye mtandao au ni picha halisi au original ya mtu huyo.

Advertisement

WhatsApp Kuja na Sehemu Mpya ya Kujua Kama Picha ni Feki

Kwa ambao walikuwa hawajui, Google image ni sehemu ya mtandao wa Google sehemu hii inakusaidia kuweza kutafuta picha yoyote kwa ku-upload picha kwenye mtandao huo na hapo hapo utapata picha zinazofanana na hiyo au picha hiyo kama imetumika kwenye tovuti mbalimbali.

Ili kutumia sehemu hiyo mpya, mtumiaji atapaswa kubofya picha yenyewe kisha chagua vidoti vitatu vya juu alafu chagua sehemu ya Search image na moja kwa moja utaletewa picha hiyo kama imetumika kwenye mitandao mingine.

Mbali na hayo sehemu nyingine inayo tarajiwa kuja kwenye programu ya WhatsApp ni pamoja na sehemu ya kivinjari ambayo hii itakuwa maalum kwa ajili ya link zinazo tumwa ndani ya WhatsApp. Kivinjari hichi kitakuwa kinafungua link mbalimbali bila kutoka kwenye programu ya WhatsApp na pia kivinjari hicho kitakuwa hakiruhusu screenshot pamoja na kurekodi video.

Mbali na hayo inasemekana kuwa, Kivinjari hicho hakina sehemu ya History hivyo watumiaji hawa takiwi kuwa na wasiwasi kwani kivinjari hicho akitakuwa kina kusanya data hata kidogo.

WhatsApp Kuja na Sehemu Mpya ya Kujua Kama Picha ni Feki

Kwa sasa sehemu hizi zote mbili zipo kwenye programu ya majaribio ya WhatsApp Beta ya Android, hakuna taarifa kamili kuhusu lini sehemu hizi zitakuja kwenye programu ya kawaida ya WhatsApp lakini pengine tutegemee kuona sehemu hizi kwa siku za karibuni.

Mbali na hayo, hivi karibuni WhatsApp imetoa onyo kali kwa watumiaji wa programu za GB WhatsApp na WhatsApp Plus huku ikitangaza kuwa watumiaji wa programu hizi watafungiwa namba zao kwa muda, Soma hapa kujua zaidi.

Kwa habari zaidi kuhusu programu ya WhatsApp hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use