Ndege Zisizo na Rubani Kuanza Kutumika na Serikali ya Tanzania

Drone zimeanza kutumika kwa njia ya tofauti hapa Tanzania
Ndege zisizo na rubani Ndege zisizo na rubani

Kwa hapa Tanzania tumesha zoea matumizi makubwa ya ndege zisizo na rubani, maarufu kama (Drone) yapo kwenye kazi ya kuchukua video pamoja na picha, lakini hili linaenda kubadilika kwani sasa ndege hizo kuanza kutumiaka kwenye shughuli za msingi za kijamii.

Kinacho thibitisha hilo, ni kusainiwa kwa makubaliano na Kampuni moja ya Marekani inayoitwa Zipline kwa ajili ya kuleta ndege 120 zisizotumia rubani (Drone) ambazo zitatumika kusambaza vifaa tiba na dawa katika maeneo yasiyofikika kwa urahisi hapa nchini Tanzania.

Hata hivyo kwa mujibu wa gazeti la nipashe, makubaliano hayo yalisainiwa jana kati ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na Kampuni ya Zipline na ndege hizo zitaanza kusambaza dawa, vifaa tiba na nyaraka muhimu kuanzia mwakani katika Mkoa wa Dodoma.

Advertisement

Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Mpoki Ulisubisya, alisema kampuni ya Zipline italeta ndege hizo 120 na zitatumika nchi nzima.

Hata hivyo Mkuu wa wizara hiyo alisema pia ndege hizo zitahudumiwa na wizara hiyo na mwanzoni zitaanza kazi katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na Mkoa wa Pwani na baadaye maeneo yote nchini.

Lakini pia Dk. Mpoki alisema kwa kufafanua zaidi kuwa mbali na kusambaza dawa, ndege hizo zitasaidia kutoa ajira kwa Watanzania ambao watafanya kazi katika kampuni hiyo hapa nchini. Kampuni ya Zipline imesha isaidia nchi ya Uganda kwa kutoa huduma kama hii na sasa imekuja hapa nchini hivyo tujiweke tayari kwa mengi mazuri kutoka kampuni hii.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.

Chanzo : US News

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use