Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Sasa Lipia Bili Yako ya Chakula KFC “China” Kwa Kutabasamu

Achana na kulipakwa simu sasa lipia bili kwa tabasamu lako
Lipia kwa Tabasamu Lipia kwa Tabasamu

Ukweli ni kuwa ulimwengu wa teknolojia unabadilika kwa kasi sana na njia zinazo tumiwa kufanya malipo mbalimbali kwenye sehemu za biashara zinaonekana kupitwa na wakati na hii kusababisha wataalam wa teknolojia kuumiza vichwa na kuleta njia mpya zenye ulizi zaidi na zenye uharaka.

Wakati Tanzania na nchi nyingi za Afrika tukiwa kwenye mifumo ya kulipa kwa kupitia mtandao ya simu, huko nchini China kunafanyika majaribio ya kulipa kwa kutumia tabasamu. Kampuni ya Ant Financial ambayo iko chini ya kampuni ya Alibaba imesema kuwa kwa sasa inafanya majaribio hayo kupitia migahawa ya KFC huko nchini china.

Advertisement

Mashine hiyo imeonyesha uwezo mkubwa wa kugundua tofauti ya mtu hata kama akibadilisha mtindo wa nywele au hata pale anapo vaa vipodozi mbalimbali hilo likidhibitisha kuwa hautaweza kuiba kwa kutumia picha au hata kwa kujiweka muonekano wa sura sawa na mwingine.

Pia huduma hiyo inakupa uwezo wa kudhibitsha zaidi kwa kuweka namba zako za simu ili kuweza kuzuia utapeli unaoweza kutokea. Najua unajiuliza je ni bure au..? kifupi ni kuwa inavyo onekana ni kuwa huduma hii itakusaudia kuacha kutembea na kadi yako ya Bank bali kila utakapo fika kwenye mashine hiyo utaweza kutumia tabasalamu lako kama udhibitisho wa kulipa na hela zitakatwa kutoka kwenye Akaunti yako.

Najua maswali ni mengi.. najua unajiuliza hivi wachina jinsi wanavyo fanana huduma hii itakuaje..? ukweli ni kuwa wataalamu hawa wanasema wame tumia teknolojia ya hali ya juu kuweza kufanikisha hili na wakiwa kwenye majaribio haya wanasema wanaimani teknolojia hii itaweza kufanikiwa na kuanza kutumika miaka ya hivi karibuni.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.

Chanzo : The Verge

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use