Wanafunzi wa Tanzania Wafanya Ubunifu wa Jembe la Sola

Wanafunzi Tanzania waendelea kufanya gunduzi za kiteknolojia
Jembe la sola Jembe la sola

Wakati hapa nchini Tanzania tukiwa kwenye hatua za awali za kuelekea kwenye Tanzania ya Viwanda, bado wananchi mbalimbali nao wanafanya harakati zao kuhakikisha Tanzania inafikia huko kwa urahisi zaidi.

Wanafunzi wa wawili wa hapa Tanzania Stephen Chacha na Naima Mohammed wamefanikiwa kufanya ubunifu wa jembe lenye uwezo wa kutumia sola. Jembe hilo ambalo limetengenezwa kwa kutumia mota maalum linao uwezo wa kupalilia shamba kwa muda mfupi sana kwa mujibu wa wanafunzi hao ambao ndio wagunduzi wa jembe hilo.

Advertisement

Jembe hilo la sola kwa sasa bado haliko kwenye hatua za kuingia sokoni na wanafunzi hao wakiwa kwenye rai ya kuomba msaada wa vyombo ambavyo pengine vinaweza kuwawezesha kutengeneza jembe hilo kuwa la kisasa na kuwa na ufanisi zaidi.

Hivi karibuni watanzania wamekua na muamko mkubwa sana wa maswala ya teknolojia kwani hivi karibuni tumeona mwanafunzi mwingine wa chuo cha mtakatifu joseph cha hapa Tanzania akiwa amefanikiwa kufanya ubunifu wa fimbo yenye kusaidia walemavu wa macho. Hizi ni kati ya juhudu chache za watanzania na serikali kupitia wizara husika na Costech kusaidia watu hawa.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.

Chanzo : BBC Swahili

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use