Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kutumia Programu Mbili kwa Wakati Mmoja Kwenye Kompyuta

Jinsi ya Kutumia Programu Mbili kwa Wakati Mmoja Kwenye Kompyuta Jinsi ya Kutumia Programu Mbili kwa Wakati Mmoja Kwenye Kompyuta

Kuna wakati ungependa kuangalia filamu huku unachat kwenye kwenye mitandao ya kijamii lakini kama tunavyojua ili kuchat kwenye kompyuta yako huku unaangalia filamu ni lazima uchati kwanza au uangalie kwanza ndio uchati kwani unapogusa kisakinishi chako kwaajili ya kuchat huwa inatokea juu ya filamu na hivyo hivyo kwa upande wa filamu, kiukweli ni kwamba imekua ni kazi sana kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja kwenye computer bila kusimamisha nyingine.

Advertisement

Lakini leo tanzania tech inawaletea njia rahisi ya kutumia ili uweze kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja hata kama ni kudownload filamu hukuna angalia nyingine chochote kile inawezekana. Kwa kutumia kompyuta yako yenye window 8 twende moja kwa moja tukajifunze namna hii rahisi sana.

Kumbuka ili njia hii iweze kufanya kazi ni lazima uwe unatumia Window 8 na kuendelea kwa wale ambao wanatumi windows 7 nazingine za zamani njia hii haita weza kufanya kazi, Basi kwa kutumia Vibonyezo vya Kompyuta yako bonyeza vitufe vifuatavyo bofya kibonyezo cha window chenye alama “WINDOW” kisha bofya “NUKTA” kisha bofya “MSHALE WA KUSHOTO AMA WA KULIA” kumbuka kubofya vibonyezo vyote hivyo kwa pamoja kisha achia kwa pamoja.

Baada ya hapo utaona window yako imeelekea upande ulio uchagua kisha bofya alama ya window tena chagua progarmu unayotaka kuangalia utaona imefunguka kwenye upande mwingine, hapo utakuwa umewezesha kompyuta yako kutumia progarmu mbili kwa wakati mmoja. Kama ungependa kuongeza saizi ya upange mmoja tumia sehemu iliyoko katikati ya progarmu hizo mbili pia ili kurudi kama awali unaweza kutumia sehemu hiyo hiyo.

Angalia video hiyo hapo juu kwa kujifunza zaidi kwa vitendo usisahu ku-comment kama haujaelewa tutafurahi kukuelewesha.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use