Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kuongeza Speed ya Internet Kwenye Simu Yako

Jinsi ya Kuongeza Speed ya Internet Kwenye Simu Yako Jinsi ya Kuongeza Speed ya Internet Kwenye Simu Yako

Kwa wengi wetu tusiokua na simu za mtandao wa 4G kuna wakati internet inakua slow sana kiasi kwamba huwezi hata kutuma meseji ya whatsapp, hii inasababishwa na mambo mengi sana ikiwemo hali ya hewa, sehemu uliyopo pamoja na mengine mengi sana ya kimtandao hata hivyo tumesha wahi kuona hapa tanzania katika vipindi mbalimbali vya mvua kuna baadhi ya mitandao inasumbua sana hasa kwenye upande wa internet.

Advertisement

Lakini kuna baadhi ya njia ambazo zinaweza kusaidia simu yako kuwa na internet yenye speed hata kwenye kipindi cha mvua ambapo internet inakua ya shida sana kutokana na matatizo ya kimtandao. Hata hivyo ili uweze kufanya moja kati ya njia hizi ni lazima ujue ni kwanini internet inasumbua kwenye simu yako ukisha gundua hilo ndipo ufuate hatua hizi, kwa leo tunaenda kufanya njia ya kubadilisha “Network mode” njia hii ni rahisi na ni ya haraka zaidi na inaonekana kuwa yenye mafanikio zaidi kuliko njia nyingine.

Ila unaweza ukawa unajiuliza Je ni kwanini tunafanya hivi.? Jibu ni kwamba tunafanya hivi kwa sababu smartphone nyingi zimetengenzwa na “network mode” zaidi ya moja ili kusaidia pale Network moja inapokosekana itumike nyingine, kwa mfano inawezekana mahali ulipo hakuna internet ya 3G au 4G hivyo simu yako moja kwa moja itabadilisha Network Mode kwenda 2G ili kukusaidia kuendela kupata internet mahali popote ulipo hata mahali ambapo hakuna network kubwa kama za 3G na 4G.

Moja kwa moja baada ya kujua hayo sasa chukua simu yako na fuata hatua hizi ili kuongeza speed ya internet katika smartphone yako. Moja kwa moja ingia katika Setting kisha bofya Connection kisha bofya More Networks alafu bofya Mobile network alfu utabofya kwenye Network mode hapo litatokea box lenye sehemu zifuatazo wcdma/gsm (auto connect), wcdma only na gsm only kama umeziona sehemu hizo basi moja kwa moja bofya sehemu ilipoandikwa wcdma only. Baada ya hapo utaona nework ya simu yako ikizima kisha kuwaka tena, ukimaliza hatua hizi jaribu kutumia internet yako hapo utaona speed ya internet kuongezeka sana.

Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kucheck video hapo juu kujifunza zaidi usisahau ku-comment kama una maoni yoyote au ushauri pia unaweza ku-like page yetu ya Tanzania tech ili kupata habari pamoja na maujanja mengine kama haya.

23 comments
    1. Asante sana Rahimu, ili kupata msaada tafadhali bofya hapo chini kwenye page yetu palipo andikwa “wasiliana nasi” kisha tuma barua pepe namna unavyotaka tukusaidia Asante.

  1. Msaada jamani please nimefungua blog yangu lakn nataka Iwe kwa kingeleza yenyewe imekuja kwa kiswahili nifanyaje naomba msaada wenu

  2. Naitwa Joyce Richard nipo Oman mm natumia Wi-Fi Ila huku nilipo inasumbua kwel had I uiweke sehemu moja ndio ishike naomba msaada kwenye android yangu jaman

    1. Joyce kusumbua kwa Wi-Fi kunatokana na upatikanaji wa huduma hiyo mahali hapo kuwa mdogo, hakuna namna ya kufanya mpaka watoa huduma hiyo waweze kuiboresha zaidi kwenye eneo ulilopo.

  3. Maoni*Tigo na pongeza kwa huduma yenu nzuri.Ila naomba msaada wenu;simu yangu haishiki facebok toka jana.

  4. Mm Nina PAGE Yangu Ya Story Ila Mara nyingi Huniandikia BOOST YOU’RE POST, Nikosema Niboost Kwa Kufata Maelekezo Yao inakataa, Naomba Mnisaidie Nifanye je Hapo Sasa,;

  5. Simu yangu ni TECNO F2 LTE na niya promosheni mtandao was vodacomu wakati nainunua niliambiwa slot 1 niweke vodacomu na slot2 niweke laini yoyote happy nitapata mtandao wa kutosha kwakweli nilifanya hivyo lakini Cha ajabu slot 2 imepigwa Pini Haina internet Sasa nifanyeje ili ipate internet maana I am 2 G tu .

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use