Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kupakua Toleo Jipya la Majaribio la Android N 7.0

Jinsi ya Kupakua Toleo Jipya la Majaribio la Android N 7.0 Jinsi ya Kupakua Toleo Jipya la Majaribio la Android N 7.0

Kwa wale ambao mnapenda kujiaribu toleo jipya la Android N 7.0 fuata njia hii ili uweze kujiaribu toleo hilo jipya, ila IKUMBUKWE toleo hili jipya bado liko kwenye matengenezo hivyo angalia usije ukaharibu kifaa chako kwa kufunga au ku-install programu hiyo. Ila kwa wale mnaotaka kujiharibu toleo hilo jipya fuata njia hizi ili uweze kufanikisha hilo.

Hatua ya kwanza hakikisha kuwa unafanya “Backup” ya simu yako kabla hujaanza hatua za kupakua na ku-install programu ya “Android 7.0 N developer preview” hii ni muhimu kwani mara nyingi progamu hizi huwa na matatizo mbalimbali ambayo yanaweza kuharibu programu za simu yako pale unapo install hivyo kwa kufanya “Backup” utaweza kurudisha simu yako kwenye hali yake ya awali.

Advertisement

Pia hakikisha sehemu maalumu ya “Backup & reset” iliyoko kwenye  simu yako imewashwa pia hakikisha ‘Back up my data’ na ‘Automatic restore’ zimewekewa tiki ikiwa na maana ya kuwa ziko ON, pia unaweza ku-backup picha zilizoko kwenye simu yako kwa kuunganisha simu yako na kompyuta kisha ingia kwenye file za simu yako na copy file zako na uziweke kwenye kompyuta yako.

Ukiwa umemaliza kufanya Backup ya simu yako sasa unaweza ukapakua programu hiyo ya “Android 7.0 N developer preview” moja kwa moja nenda katika website hii ya Google Android N Developer Preview Page ili kupata habari zote zinazo husu toleo hilo. Pia page hiyo ya Google itakupa habari kamili zinazohusu programu hiyo ya Android N Developer Preview pia itakupa stepu moja moja za namna “Android 7.0 N developer preview” itakavyokua ikitoka hakikisha unasoma ukurasa huo kwa makini.

Baada ya kusoma na kuelewa namna programu hiyo itakavyotoka na ni vitu gani utakavyo pata pale utakapo fanikiwa kuweka programu hii kwenye simu yako, moja kwa moja nenda kwenye page hii ya Android Beta Program ingia kwa akaunti yako ya google iliyopo na simu yako, baada ya kufanikiwa kuingia utaona listi ya simu zote ambazo zinaweza kuinstall program hiyo ya Android N kama kivaa chako kipo katika list hiyo bofya ‘Enroll Device’ kama hapo kwenye picha.

eligable

Hakikisha Akaunti yako ya Google unayotumia ni sawa na ile unayotumia kwenye simu yako hiyo ya Android, baada ya hapo utaona simu yako ikipata toleo hilo jipya la “Android 7.0 N developer preview” akikisha una bando la kutosha kupakua toleo hilo.

Baada ya kujiaribu na kama unataka kurudi katika toleo lako la zamani la Android 6.0 ingia tena katika website ya Android Beta Program kisha bofya ‘Unenroll device’ KUMBUKA kwa kufanya hatua hii utapoteza vitu vyote vilivyopo kwenye simu yako hivyo ni vizuri ukiwa umefanya backup hapo mwanzoni.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use