Namna ya Ku-Copy Picha Zote Kwenye Account ya Instagram

Namna ya Ku-Copy Picha Zote Kwenye Account ya Instagram Namna ya Ku-Copy Picha Zote Kwenye Account ya Instagram

Jinsi inavyojulikana ni kwamba si rahisi kucopy picha zote kwenye account ya Instagram pale ambapo zinakua tayari zipo kwenye account hiyo, watu wengi hutumia njia ya kufanya screenshot au ku-repost ilikuweza kupata picha flani kutoka kwenye account ya Instagram. Lakini inakuaje nikikwambia kuwa kuna njia rahisi yaku-copy picha za mtu yoyote kutoka kwenye account ya Instagram ?, kwa kutumia njia hii unaweza kupata picha zote za profile yako au ya mtu yeyote unae taka kwa muda usio zidi dakika moja tu.

Kwa kuanza basi kumbuka njia hii inaweza kufanyika pale mtu unapokua na computer tu na sio vinginevyo kama unatka kujifunza namna ya kucopy picha kwa kutumia simu bado watalamu wetu wanaendelea kushulikia hilo pale watakapo kua tayari tutawaletea njia hizo hapahapa Tanzania tech blog moja kwa moja twende tukajifunze namna ya ku-copy picha zote za instagram kutoka katika account ya mtu yeyote.

Advertisement

Hatua ya kwanza hakikisha unaingia kwenye website ya instagram ambayo inapatikana hapa http://instagram.com kisha baada ya hapo login kwenye account yako ya instagram kwa kutumia jina lako na password yako au unaweza kutumia facebook kuingia katika account yako.

Hatua ya pili chagua profile ya mtu au kama ni yakwako fungua profile yako alfu sogea mpaka chini kidogo utaona kitufe kimeandikwa “Load More” kibonyeza na subiri mpaka picha zote zionekane.

Hatua ya tatu baada ya picha zote kuoekana chagua picha yoyote kwenye profile hiyo kisha right click na kisha bonyeza save as subiri file limalize kupakua.

Hatua ya nne baada ya file kumaliza kupakua fungua file hilo hakikisha unafungua kama folder yani usifungua file hilo pekee, kwa kifupi fungua mahali ilo folder lilipo pakuliwa kisha tafuta Folder lenye jina la profile yako ama mtu uliechukua picha zake, hapo utakuta picha zote zilizowekwa zikiwa na Quality nzuri kabisa.

Kama unataka kujifunza hatua kwa hatua angalia video hapo juu usisahau ku-comment kama kuna mahali umekwama tutakusaidi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use