Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Movie Nzuri za Kuangalia Christmas Hii Mwaka 2018

Wakati huu wa Christmas furahia movie hizi nzuri za Teknolojia
Hizi Hapa Movie Nzuri za Kuangalia Christmas Hii Mwaka 2018 Hizi Hapa Movie Nzuri za Kuangalia Christmas Hii Mwaka 2018

Christmas ni kipindi kizuri cha kujumuika na ndugu, jamaa, na marafiki ikiwa pamoja na ku-enjoy siku yenyewe kwani ni kweli wote kwa ujumla tunakila haki ya kufurahi na kushukuru kwani Mwenyezi Mungu amatupa tena kibali cha kuona Christmas nyingine tena.

Najua kila mtu anayo namna yake ya kusherekea siku hii lakini kwa wenzangu na mimi mnao penda Movie basi kama kawaida leo nimewaletea list yangu ya Movie nzuri za kuangalia kipindi hiki cha msimu wa sikukuu hasa Christmas. Kama kawaida mimi napenda teknolojia sana, hivyo kwenye list hii movie nyingi kama sio zote zitakuwa ni movie za kiteknolojia zaidi hivyo kama wewe ni mpenzi wa teknolojia basi na uhakika utapenda movie hizi kwa asilimia 100. Ok let’s get to it..

Advertisement

9. Unfriended Dark Web (2018)

Dark Web ni movie inayo husiana na jamaa mmoja ambaye alichukua laptop isiyokuwa yake kutoka kwenye maduka yanayotoa huduma za Internet na alipo fika nyumbani na kufanikiwa kuifungua alikutana na video zilizokuwa zinaonyesha mauaji ya kutisha sana. Baadae mwenye laptop alikuja kumpata jamaa huyo kupitia Facebook na nadhani unahitaji kuangalia Movie hii kujua kilicho endelea.

Download Unfriended Dark Web (2018)

8. Searching (2018)

Searching ni movie nyingine nzuri sana ya kuangalia msimu huu, Movie inahusu baba na mtoto wake wa kike ambaye alipotea kwenye mazingira ya kutatanisha. Hatimaye baba alianza kutumia kompyuta ya mwanae kuweza kujua mwanae yuko wapi na hatimaye baadae baba aligundua mambo mengi sana ambayo mwanae alikuwa akifanya bila hata yeye kujua.

Download Searching 2018

7. Pacific Rim Uprising (2018)

Pacific Rim Uprising ni sehemu ya pili ya movie nzuri sana ya Pacific Rim, Kama unapenda movie kama Transformer na movie za mtindo huo basi ni lazima utapenda Movie Hii. Movie hii inahusu kijana ambaye baba yake alikuwa mtu mashuhuru kwenye sehemu ya kwanza ya Movie hii, kijana huyo alikuwa na uwezo mkubwa wa kuendesha robot lakini kwa bahati mbaya alishindwa kuchaguliwa na jeshi kutokana na tabia yake. Baadae nchi ilivamiwa na viumbe wa ajabu na ilibidi kijana huyo apate nafasi ya kuendesha robot hizo za jeshi.

Download Pacific Rim Uprising (2018)

6. Upgrade (2018)

Upgrade ni movie nzuri sana kwa wanaopenda movie za Action, Movie hii inahusu jamaa mmoja aliyekuwa anaishi maisha mazuri na mkewe aliyekuwa akifanya kazi kwenye sekta nyeti ya kiteknolojia. Baadae wakiwa njiani walivamiwa na mke wa jamaa ali uwawa na jamaa nae alipigwa risasi lakini alifanikiwa kupona na kuwa kilema, baadae jamaa alikukutana na jamaa mmoja ambaye ni mtaalam wa teknolojia na jamaa huyo alimuwekea chip ambayo ilimpa nafasi ya kuweza kutembea tena. Baadae jamaa alikuja kujua chip hiyo ilikuwa inamuendesha yeye na sio yeye anaenesha chip hiyo iliyokuwa ndani ya kichwa chake.

Download Upgrade (2018)

5. The Predator (2018)

The Predator 2018 ni movie nzuri sana ambayo ni mwendelezo wa movie za predator ambazo zimeanza kutoka toka mwaka 90. Predator ya mwaka huu 2018 inahusu viumbe hao ambao walikuja kutoka sayari nyingine kwa ajili ya kuwinda viumbe vingine kama hivyo ambavyo navyo vilikuja duniani. Movie inakuwa nzuri zaidi baada ya waalifu wa kivita kuwa ingilia kwenye vita hivyo baada ya mmoja wao kuchukua baadhi ya vifaa vya viumbe hivyo.

Download The Predator (2018)

4. Black Panther (2018)

Black Panther ni movie nzuri sana kama bado hujangalia Movie hii, Kama umesikia neno wakanda basi ujue neno hilo linatoka kwenye movie hii. Movie hii inatoka Marvel na inahusiana na jamaa mmoja ambaye ni Chief kwenye kabila moja la wakanda hapa Afrika. Jamaa nataumia teknolojia kuweza kulinda kijiji chake pamoja na kupigana na adui ambao ni watu wa karibu yake pamoja na ndugu yake ambaye amekulia kwenye maisha ya uhalifu.

Download Black Panther

3. Anon (2018)

Anon ni movie inayo husiana na sehemu ambayo ilikuwa haina uhalifu kabisa lakini polisi mmoja anakutana na mdukuaji (Hacker) mmoja amabye ni mwanadada mwenye ana uwezo wa ku-hack watu. Dada huyo ana hack kituo cha polisi pamoja na mitambo mingine mbalimbali ya kiteknolojia.

Download Anon (2018)

2. Johnny English Strikes Again (2018)

Kama unafahamu Movie za Mr Bean za zamani hii ni tofauti kabisa, Johnny English Strikes Again ni movie ambayo inahusu Mr Bean ambaye alikuwa ni polisi anaetafuta wahalifu akiwa undercover, na baadae alijikuta anajitokeza kwa sababu ya uhalifu wa mtandaoni (cyber-attack) uliotokea na kuanza kumtafuta muhalifu aliye fanya udukuzi huo. Kama unapenda movie za kuchekesha na Action basi hii ni movie kwa ajili yako Christmas hii.

Download Johnny English Strikes Again (2018)

1. Venom 2018

Kama wewe ni mpenzi wa movie za kisayansi na kiteknolojia basi unaweza kuangalia Movie hii, Movie inahusu jamaa mmoja ambaye alikuwa ni mwandishi wa habari aliyefanikiwa.. Kama Millard Ayo hivi hahaha anyway jamaa alikuwa na rafiki yake wa kike aliyekuwa akifanya kazi kwenye kampuni ya uchunguzi ya maswala ya anga, kampuni ambayo inaleta viumbe wapya kutoka sayari nyingine na kuanza kufanya uchunguzi kwa kuweka viumbe hao kwa binadamu. Mtangazaji huyo baadae anakuwa ni mmoja wa walioekewa viumbo hao kwa bahati mbaya na kuanza kubadilika na kuwa kiumbe cha ajabu.

Download Venom (2018)

That’s it Guys hii ndio list ya Movie ambazo ukweli unaweza kuziangalia na kufurahia kama unapenda maswala mazima ya teknolojia. Unaweza kuangalia movie hizi au unaweza kuzpakua kupitia link nime kuwekea hapo chini kwenye video. Kama unataka kudownload movie hizi kupitia simu yako ya Mkononi unaweza kufuata njia hizi hapa. Au pia unaweza kutumia apps hizi nzuri za kudownload Movie. Nakutakia mapumziko mema na Christmas Njema, kama kuna link yoyote haifanyi kazi unaweza ku-comment hapo chini.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use