Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Tigo Mbioni Kumiliki Mtandao wa Simu wa Zantel

Inasemekana Toka mwaka 2015 Tigo inamiliki asilimia 85 ya hisa za Zantel
Tigo mbioni kumuliki Zantel Tigo mbioni kumuliki Zantel
<a href="http://www.kajunason.com/2014/12/wateja-wa-tigo-na-zantel-sasa-kufurahia.html" rel="nofollow" target="_blank"><span style="font-size: x-small;">Photo via Kajunason</span></a>

Kwa mujibu wa habari kutoka tovuti ya The Citizen, Tigo iko mbioni kumiliki mtandao wa Zantel kutokana na kampuni hiyo kumiliki asilimia kubwa za hisa za kampuni ya Zantel. Kwa mujibu wa The Citizen, Karibu miaka mitatu na miezi sita tangu Millicom International Cellular (Mic) au Tigo ilipata asilimia 85 ya sehemu ya mtandao wa Zanzibar Telecom (Zantel) kutoka kwa kampuni kampuni mama ya Zantel ya Umoja wa Falme za Kiarabu inayoitwa Etisalat Group.

Kwa mujibu wa Citizen, Mic Tanzania au Tigo Tanzania kwa sasa inataka kumiliki asilimia zote za mtandao huo na inasemekana imesha andika barua kwa Fair Competition Commission (FCC) kwa ajili ya kuomba kibali cha kuchuka asimia zote za hisa za kampuni ya mawasiliano ya Zanzibar Telecom au (Zantel).

Advertisement

Hata hivyo, inasemekana kuwa bado Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inamiliki asilimia 15 ya hisa za mtandao wa Zantel, lakini kwa mujibu wa gazeti ambalo halikutajwa inasemekana kuwa hisa hizo zitahamishiwa ili kufanya umiliki huo kuweza kukamilika na kufanya kampuni ya Mic Tanzania kuwa na asilimia 99.9 za hisa za kampuni hiyo ya Zanzibar Telecom (Zantel).

Kwa sasa kwa mujibu wa sehemu ya taarifa iliyo wekwa kwenye tovuti ya The Citizen, “FCC inafanya upelelezi huku ikiwataka wote ambao wanajiona kuwa na maslahi ya kutosha katika ushirikiano huu kufaili na kusajili maslahi hayo au kuandika maelezo kwa njia ya maandishi kwa FCC ndani ya siku 14, “sehemu ya taarifa hiyo iliandika.

Kwa mujibu wa data kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Zantel ilikuwa na jumla ya wanachama (Subscribers) 1,071,586 wakati Tigo ilikuwa na jumla ya wanachama (Subscribers) 12,006,568 mwezi June mwaka 2018. Hii inaonyesha kuwa, endapo Tigo ikifanikiwa kumiliki kampuni ya Zantel itakuwa na jumla ya wanachama (Subscribers) 13,078,154, ambapo itakuwa imeikaribia kidogo kampuni ya Vodacom Tanzania ambayo inasemekana kuwa na wanachama (Subscribers) zaidi ya 13,277,574.

Kwa upande wa Mobile Money, Tigo na Zantel zote kwa ujumla zina kadiriwa kuwa na jumla ya watumiaji 7,286,907 mwezi june mwaka 2018 na hii ikiwa ni zaidi ya watumiaji wa huduma ya M-Pesa ambao wanakadiriwa kufikia 1,355,355 ndani ya kipindi hicho.

Yote haya yana onyesha endapo Tigo itafanikiwa kumiliki matandao wa Zantel, itakuwa imefanikiwa kumiliki asilimia nyingi zaidi za watumiaji milioni 41.8 wa huduma za sauti hapa Tanzania na asilimia nyingi za watumiaji milioni 20.8 wa huduma za Mobile Money.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use