Ripoti : Android Oreo Bado Sana Sasa Inatumika kwa Asilimia 4.6%

Haya ndio matumizi ya mifumo ya Android kwa Aprili 2018
android-oreo-nougat android-oreo-nougat

Google imekuwa ikitoa ripoti mbalimbali kuhusu matumizi ya mifumo yake ya Android, mwaka huu Google imetoa ripoti hiyo mpya ambayo inaonyesha kuwa mfumo wa Android Oreo unakuwa kwa kasi ndogo sana kwani mpaka sasa mfumo huo unatumika kwa asilimia 4.6% tu kati ya mifumo yote.

Kwa hapa Tanzania na uhakika mambo yatakuwa ni tofauti zaidi kwani ni wazi kuwa, watu wengi hutumia simu za zamani kidogo kuliko wale wanaotumia simu za kisasa. Hata hivyo kampuni nyingi zimekuwa haziweki mfumo mpya wa uendeshaji kwenye simu za zamani hii ni ili kulazimisha wateja kununua simu mpya au kutokana na sababu ya simu hizo kutokuwa na uwezo au sifa za kuimili mfumo huo mpya. Hata hivyo matumizi ya mfumo wa Android Nougat yana onekana kukuwa na kufikia asilimia 28.5% kwa Aprili mwaka huu 2018.

Hii inaonyesha kuwa simu nyingi zimekuwa zikiwezeshwa kupata mfumo wa Android 7 au Android Nougat lakini ni wazi kuwa ni simu chache sana zinazo tumia mfumo huo hadi sasa zitakuwa na uwezo wa kutumia mfumo mpya wa Android Oreo kwa siku za karibuni.

Advertisement

Lakini pamoja na hayo bado matumizi ya mifumo ya zamani yapo tena sana kwani kulingana na chat hiyo, unaweza kuona mfumo wa Android Marshmallow ndio ulio chukuwa nafasi kubwa kwa kuchukua asilimia 26.0% ya mifumo yote ya Android. Lakini pia bado watu wengi wanatumia simu zenye mifumo mingine ya zamani kama vile inavyo onekana kwenye chat hapo juu.

  • Nini Ufanye Kupata Mfumo Mpya wa Android

Sasa nini kifanyike kuhakikisha unakuwa unapata mfumo mpya kwenye simu yako unayo nunua sasa..? Swali hili majibu yake ni magumu kidogo kutokana na kuwa kampuni nyingi ziko kibiashara zaidi hivyo kuzuia watumiaji kupata mfumo mpya ili kuwafanya wanunue simu mpya zinazotoka.

Lakini pia kuna kitu kimoja kikubwa ambacho unaweza kufanya. Kitu chenyewe ni kuhakikisha kuwa unanunua simu yenye RAM kubwa yaani hakikisha unakuwa na simu yenye RAM angalau kuanzia GB 4 na kuendelea, hii ni kutokana na kuwa simu nyingi zinashindwa kupata mfumo mpya kutokana na udogo wa RAM inayo patikana kwenye simu hizo.

Kwa mfano, ukiangalia simu nyingi mpya za sasa zinakuja na RAM kuanzia GB 3 na kuendelea hivyo basi, ili kuhakikisha simu yako inaendelea kupata mfumo mpya basi ni lazima kuhakikisha simu hiyo inakuwa hatua moja mbele kwa kuwa na RAM angalau GB 4. Kwa kufuata njia hii utakuwa umejiweka kwenye hatua nzuri za kuhakikisha unapata mfumo mpya wa Android kwenye simu yako pale unapo patikana.

Kwa wale wanaoshirki shindano la kushinda Vocha usisahau, kutembelea kurasa hapa kuchukua pointi zako za Bonus za kila siku, hizi zitakuzaidia kuchukua ushindi kwa urahisi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use