Samsung Hatarini Kupitwa na Tecno Mauzo ya Simu Afrika

Samsung inaongoza kwa mauzo kwa kuuza nakala 3.4 robo ya kwanza 2018
Samsung Hatarini Kupitwa na Tecno Mauzo ya Simu Afrika Samsung Hatarini Kupitwa na Tecno Mauzo ya Simu Afrika

Kwa mujibu wa ripoti za utafiti uliofanyika na Canalys, Samsung bado inaongoza kwa mauzo ya simu Afrika kwenye robo ya kwanza ya mwaka huu 2018. Pamoja na Samsung kuongoza kwenye robo hiyo ya kwanza ya mwaka inayo anzia January 1 mpaka March 31, Kampuni za kuuza simu za China nazo zinaonekana kutawala soko la simu kwa nchi za Afrika huku zikionyesha tishio kwa kampuni ya Samsung.

Kwa mujibu wa ripoti za utafiti huo, Kampuni ya Tecno inaonyesha kupambana na Samsung na uhenda pengine kwenye nusu ya kwanza ya mwaka huu kampuni hiyo inaweza kuongoza kwenye mauzo ya simu kwa Afrika nzima. Utafiti huo unaonyesha Tecno imeshika nafasi ya pili mwaka huu 2018 kwa kuuza nakala milioni 2.8 ikiwa chini ya Samsung ambayo inaongoza kwa kuuza nakala milioni 3.4 kwa nchi za Afrika.

Kampuni ya China ya iTel inaonekana kushika nafasi ya tatu kwa kuuza nakala milioni 2.0, huku Huawei ikifatia kwenye nafasi ya nne yenyewe ikiwa imefanikiwa kuuza nakala milioni 1.1 kwenye robo hiyo ya kwanza ya mwaka 2018. Nafasi ya tano kama unavyo ona kwenye chati hapo juu ni kampuni ya Infinix ambayo imeuza nakala milioni 1.0 kwenye robo ya kwanza ya mwaka huu 2018.

Advertisement

Aidha ripoti za utafiti huo zinaonyesha, Samsung imekuwa kwenye soko la mauzo kwa asilimia 42% mwaka 2018, kutoka kuuza nakala milioni 2.4 kwenye robo ya kwanza ya mwaka jana 2017, hadi kuuza nakala milioni 3.4 kwenye robo ya kwanza ya mwaka huu 2018. Kifupi ni kwamba japokuwa Samsung inaongoza kwenye utafiti huo, lakini bado haijafikia kampuni kama Tecno na Infinix ambazo zenyewe zina angalia soko la Afrika kwa kutoa simu ambazo ni za bei nafuu kwaajili ya watumiaji wa kipato cha kawaida.

Kuona ripoti hiyo nadhani ni wakati sasa kwa Samsung kuamka na kuanza kutengeneza simu za bei nafuu kwaajili ya watu wa kipato cha kawaida, bila hivyo pengine kwenye robo ya kwanza ya mwaka kesho 2019 Samsung inaweza kuondoka kwenye nafasi yake ambayo imeshikilia kwa muda mrefu. Tuambie maoni yako wewe unaonaje kuhusu hili..? Tuambie kwenye maoni hapo chini.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use