Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Sababu za Watumiaji Kubadilika Kutoka Android Kwenda iOS

Hizi hapa ndio sababu kwanini watu wengi uhama kutoa Android kwenda iOS
Kuhama Android kwenda iOS Kuhama Android kwenda iOS

Japokuwa kichwa cha habari kinasema Android kwenda iOS lakini ni kweli kuwa wapo pia watu wengi wanaobadilika kutoka kwenye iOS kwenda kwenye Android na zifuatazo ndio sababu ambazo zimeainishwa kwenye utafiti uliofanyka hivi karibuni.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka mtandao wa PCMag, ambao ulifanya utafiti uliohusisha watumiaji wa simu mbalimbali zaidi ya 2500, Asilimia 47 ya watu hao walisema wamehama kutoka Android kwenda kwenye iOS na sababu ilikuwa ni ubora na urahisi binafsi wa kutumia simu hizo. Hata hivyo asilimia 30 ya watu hao walihama kutoka iOS kwenda Android kwa kigezo hicho hicho.

Advertisement

Hata hivyo kupitia utafiti huo inaonekana kama watu wengi sana wanahama kutoka Android kwenda iOS kutokana na urahisi na ubora binafsi kwenye matumizi ya simu hizo za mfumo wa iOS. Vilevile asilimia kubwa ya wanaohama kutoka kwenye simu za iOS kwenda Android wengi walikuwa wakisema sababu kubwa ni bei ya simu hizo ukilinganisha na Android.

Sababu nyingine ambazo zilitajwa kwenye utafiti huo ni pamoja na urahisi wa kutumia app nyingi kwenye simu za Android, pia pamoja na usasishaji (update) wa haraka wa matoleo mapya ya mfumo wa uendeshaji wa simu za Android.

Mbali ya utafiti huo, kipindi cha nyuma hapa Tanzania Tech tulisha wahi kuongelea kuhusu ni simu gani ununue kati ya Android au iOS na kama hujasoma makala hiyo, tuliongelea sana urahisi wa mtumiaji na nilisema kuwa mara nyingi watu wanaotumia simu za Android ni watu wenye kutaka zaidi yaani mtu anataka App zaidi, anataka uwezo zaidi na pia anataka bei pungufu zaidi na mengine mengi..

Kwa upande wa watumiaji wa simu za iOS hapa watu wengi wenye simu hizi huwa wanaridhika na wanachopata. Yaani watu wengi wanaotumia simu za iOS huwa wanapenda ile hali ya kuwa na simu yenye kufanya mambo ya muhimu kwao tu na sio zaidi ya hapo.

Kwa mfano nahakika kila anaetumia simu za iOS anasababu kwanini anaendelea kutumia simu hiyo na pengine bei ya simu hizo ni kubwa lakini unakuta kuna kitu binafsi mtu anakipenda kwenye simu hiyo kiasi kwamba anashindwa kuacha kutumia simu za iOS japo kuwa bei yake ni kubwa zaidi.

Kwa watumiaji wa Android haiko hivyo kwani kila siku mtu anataka zaidi, utakuta mtu anataka simu yenye wireless charging, kesho anataka simu yenye Radio, kesho anataka simu yenye kamera nzuri zaidi, yaani unakuta mtu hawezi kutumia simu moja kwa muda mrefu sana kutokana na kutaka zaidi.

Kwa mtumiaji wa iOS mwenyewe hata kama simu ikibadilika bado yeye anaendelea kuipenda simu hiyo sababu ya kitu chake kile kimefanyiwa maboresho zaidi au kimekuwa rahisi kutumia. Hivyo moja kati ya sababu ambayo mimi nadhani ndio sababu kubwa ya watu kuhama kutoka Android kwenda iOS ni ile hali ya mtu kufikia hatua ya kutaka simu yenye kufanya anacho kipenda yeye na sio kuwa na simu yenye kufanya zaidi.

Ndio maana mara nyingi mtu akishaanza kutumia iOS basi anashindwa kuhama tena kutokana na kuridhika. Lakini vilevile kama sio mtu wa kuridhika basi ni lazima atarudi kwenye Android kwa sababu mbalimbali na utamsikia akisema, bora android inafanya kitu fulani…

Wewe unaonaje..? Unadhani nini sababu ya watu kuhama kutoka Android kwenda iOS..?, Kama wewe ni mmoja wa watu waliohama kutoka Android kwenda iOS hebu share na sisi sababu zako kubwa zilikuwa ni nini..? Pia vilevile kama ulihama kutoka iOS kwenda Android pia tuambie sababu yako ilikuwa ni nini… pengine hiyo itasaidia na wengine wanaotaka kununua simu za aina hizi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use