Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mambo ya Kujua Kabla ya Kununua Laptop ya MacBook

Njia hizi zitakusaidia kupata laptop bora ya macbook hasa kwa hapa Tanzania
Mambo ya Kujua Kabla ya Kununua Laptop ya MacBook Mambo ya Kujua Kabla ya Kununua Laptop ya MacBook

Kama wewe ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii ni wazi utakuwa umeshakutana na matangazo mengi sana ya wauzaji wa laptop za MacBook. Pengine hii inachangiwa na kushuka kwa bei kwa laptop nyingi za zamani za Apple hivyo kufanya laptop hizo kupatikana kwa bei rahisi.

Sasa kabla ya wewe kuamua kununua laptop ya MacBook ni vyema unipe muda mfupi kwani kupitia makala hii nitaenda kujuza mambo ya muhimu kufahamu kabla ya kununua laptop yoyote ya MacBook. Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye makala hii.

Advertisement

Usinunue MacBook za Zamani

Kama wewe ni mtumiaji wa laptop za MacBook au kama wewe ndio unaingia kwa mara ya kwanza kwenye mfumo wa macOS basi ni vyema ufahamu hili. Kama unataka laptop bora ya MacBook Air usinunue MacBook Air ya nyuma ya mwaka 2018. Japokua hii ni bei ghali kidogo lakini utafurahia zaidi matumizi yake na uwezo wake.

Mambo ya Kujua Kabla ya Kununua Laptop ya MacBook
MacBook Air ya Zamani

Kama unataka kununua MacBook Pro ya zamani hakikisha unanua MacBook Pro ya kuanzia mwaka 2019 na kuendelea jitahidi sana usinunue MacBook ya nyuma ya hapo. Kama mtumiaji wa MacBook Pro naweza kukwambia utapata urahisi zaidi kutumia laptop hizi na kudumu nazo kwa muda endapo utafuata hatua hizi.

Hakikisha RAM Kabla ya Kununua

Kabla ya kununua laptop ya MacBook ni vyema kuhakikisha RAM na kujua kama inaweza kuendana na matumizi yako. Hii ni muhimu kwani laptop nyingi za Mac (Kuanzia Mwaka 2012) hazina sehemu ya kubadilisha au kuongeza RAM, hii ni kwa sababu RAM zake zimetengenezwa ndani ya Motherboard moja kwa moja.

Mambo ya Kujua Kabla ya Kununua Laptop ya MacBook
Muonekano wa RAM ya Ndani ya MacBook

Hii ni muhimu kwa kuwa utakapo nunua laptop hii hutoweza kubadilisha au kuongeza RAM hivyo ni vyema kuchagua laptop yenye RAM ya kutosha kwa ajili ya matumizi yako ya kilasiku.

Angalia Keyboard Kabla ya Kununua

Kwa hapa Tanzania ni wazi kuwa laptop nyingi ambazo unaziona zinauzwa kwenye mitandao ya kijamii hasa za zamani zina kuja zikiwa zimesha tumika (Refurbished) hivyo kama unataka kununua MacBook za kuanzia mwaka 2016 hadi 2018, hakikisha unakuwa makini kwa kuchunguza vizuri keyboard kabla ya kununua.

Mambo ya Kujua Kabla ya Kununua Laptop ya MacBook

Hii ni kwa sababu laptop nyingi za kuanzia mwaka 2016 hadi 2018 zinakuja na keyboard ya butterfly keyboard ambayo inajulikana kuwa na matatizo mengi kulingana na ripoti za watumiaji wengi. MacBook za kuanzia mwaka 2019 na kuendelea nyingi hazina matatizo hayo ila sio vibaya kuhakikisha una angalia kwanza kabla ya kununua.

Angalia Afya ya Battery (Battery Healthy)

Kama unafikira kununua MacBook za zamani hii ni muhimu zaidi kwako (Hata kwa anaye nunua matoleo mapya ya Refurbished) kwani itakusaidia sana kutumia laptop yako kwa muda mrefu bila kuchaji kila mara. Soma zaidi hapo chini.

Mambo ya Kujua Kabla ya Kununua Laptop ya MacBook
Muonekano wa Menu ya Kuangalia Battery Healthy

Battery Health Bora: Kama unataka kununua MacBook ya zamani hakikisha battery healthy inakuwa kuanzia asilimia 80% au zaidi. Kwa hapa battery ya laptop inaweza kuimili kukaa na chaji kwa muda kulingana na aina ya kazi unayofanya kwenye laptop yako.

Battery Health ya Kati: Battery health ya kati ni kuanzia asilimia kati ya 70% na 80%. Hapa utaweza kuendelea kutumia laptop yako lakini utagundua kuwa inaisha chaji haraka na mara nyingine inaweza kuzima ghafla kulingana na kazi unayofanya.

Battery Health Mbaya: Kama kwa namna yoyote ukiangalia battery healthy na ukaona inaonekana kuanzia asilimia chini ya 70% basi usinunue laptop hiyo. Kwenye stage hii  hautaweza kutumia laptop hiyo kwa muda mrefu bila kuchomeka kwenye chaji, pia mara nyingi laptop hizi zinakuwa na matatizo mengine tofauti  na battery.

Jinsi ya Kuangalia Battery Healthy MacBook

Kama unataka kuangalia battery healthy kwenye laptop ya MacBook unayotaka kununua unaweza kufuata hatua hizi rahisi.

  1. Bofya sehemu ya Menu (Kwenye Logo ya Apple Juu Kushoto) kisha chagua “System Settings”.
  2. Kisha upande wa kushoto angalia Menu iliyo funguka na kisha angalia sehemu iliyoandikwa “Battery”.
  3. Baada ya hapo bofya sehemu ya “Battery Healthy” ambayo ni sehemu ya pili kwenye menu hiyo, kisha bofya sehemu ya ⓘ kujua zaidi kuhusu afya ya battery ya laptop yako na kuona asilimia.

Mbali ya kutumia njia hii, kama una uwezo wa kuinstall program kwenye kompyuta ya MacBook basi unaweza kupakua app ya “coconutBattery 3“. Unaweza kutafuta app hii kuptia Google na install kwenye kompyuta yako na itaweza kukupa taarifa zaidi kuhusu battery ya kompyuta yako.

Mambo ya Kujua Kabla ya Kununua Laptop ya MacBook
Programu ya coconutBattery 3

Angalia Mfumo wa Uendeshaji

Unapo nunua MacBook ni vyema ujue kuhusu programu utakazo tumia, kama unataka kuhakikisha kuwa unatumia programu mpya na zamani bila usumbufu na kuhakikisha usalama wa laptop yako basi ni vyema kuangalia haya.

Mambo ya Kujua Kabla ya Kununua Laptop ya MacBook
Muonekano wa Mfumo wa maOS Sonoma (14)

MacBook zenye macOS hizi ni za kuepuka: Epuka MacBook ambazo zimekwama kwenye macOS High Sierra (10.13) au toleo lolote la nyuma ya hapa, kwani hazina usalama wa kisasa na hazipokei update na  programu za kisasa.

MacBook zenye macOS hizi ni za kawaida: MacBook zenye macOS Mojave (10.14) na Catalina (10.15) bado zinaweza kutumika lakini zina karibia mwisho wa kipindi cha usaidizi na update.

MacBook zenye macOS hizi ni nzuri: MacBook zenye macOS Big Sur (11) na Monterey (12) ni chaguo bora kwa mtu anaeangalia MacBook ya zamani upande wa mfumo wa uendeshaji.

MacBook zenye macOS bora zaidi: MacBook zenye macOS Ventura (13) na Sonoma (14) ni matoleo bora zaidi, kwani yanahakikisha usaidizi na uwezo wa kupata update kwa muda mrefu zaidi na utendaji bora kwa mashine ya zamani.

Angalia Umbo na Ubora wa Laptop

Mwisho kabisa kama wewe ni mtumiaji wa laptop mara kwa mara basi ni vyema kuangalia laptop yenye umbo kulingana na matumizi yako. Laptop nyingi za zamani za MacBook Air ni bora kwa kazi za kawaida na kazi ambazo hazitumi uwezo mkubwa wa processor, chaji na RAM.

Mambo ya Kujua Kabla ya Kununua Laptop ya MacBook
Muonekano wa MacBook Air (Kushoto) na MacBook Pro (Kulia)

Unaweza kuchagua laptop nyembamba yenye kuweza kutumika mahali popote kwa haraka hasa kama kazi zako sio kazi kubwa.

Kwa wale wenzangu na mimi ambao tunatumia laptop kufanya kazi ngumu kama za uandishi wa program (Developer) au hata Graphics designer ni vyema kuchagua laptop ambayo ina uwezo zaidi wa kupunguza joto kwani bila hivyo ni lazima laptop yako itakuwa slow na kuzidiwa na joto. Kwa hapa ni wazi unahitaji MacBook Pro ambazo hizi huwa na umbo kubwa kidogo.

Hitimisho

Najua nimesema maneno mengi kidogo lakini ni wazi vipo vitu vingi sana vya kuangalia kabla ya kununua laptop ya MacBook, haya niliyo weza kuandika hapa ni yale ya muhimu na yanayo endana na watumiaji wa kazi zote.

Makala hii pengine ingekuwa ndefu zaidi pale ambapo ningandika kulingana na aina ya kazi ambayo unataka kufanya na laptop yako. Hivyo kama kuna point ya muhimu ambayo nimeacha kuandika unaweza kuongeza kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kama wewe ni Windows fun unaweza kusoma hapa kujua mambo ya kuangalia kabla ya kununua laptops za Windows.

Kwa makala zaidi kama hizi hakikisha una tembelea Tanzania Tech kila siku, pia hakikisha una kaa karibu na sisi kupata habari zaidi za Teknolojia kupitia Tanzania Tech App.

Baada ya kupakua app ili kusoma makala za kiswahili bofya Menu upande wa juu kushoto kisha chagua “Swahili Site” kisha chagua kiswahili na kisha funga na fungua app na utakuwa unasoma makala za kiswahili tu bila kubadilisha kwa mara nyingine.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use