Fahamu Yote ya Muhimu Kuhusu Mfumo Mpya wa macOS 10.15

Mfumo huu unakuja na maboresho machache lakini ya muhimu
Fahamu Yote ya Muhimu Kuhusu Mfumo Mpya wa macOS 10.15 Fahamu Yote ya Muhimu Kuhusu Mfumo Mpya wa macOS 10.15

Kampuni ya Apple hapo jana kupitia mkutano wa WWDC, imezindua mfumo mpya wa macOS 10.15 Catalina, mfumo huu mpya wa macOS unakuja na mabadiliko kadhaa ambayo yanagusa zaidi wabunifu wa programu mbalimbali.

Kupitia makala hii tutaenda kuongelea yote ya muhimu kuhusu mfumo mpya wa macOS Catalina pamoja na mambo mengine machache yaliyo badilika kutoka kwenye mfumo uliopita wa macOS mojave.

Project Catalyst

Kama wewe ni mbunifu wa programu za iPad basi habari njema kwako kwani Apple imetangaza ujio wa project catalyst, sehemu hii itakuwa inakupa uwezo wewe mbunifu kubadilisha programu zako za kawaida za iPad na kuweza kufanya kazi kwenye kompyuta zote zinazotumia mfumo wa macOS Catalina.

Advertisement

Kwa mujibu wa Apple, Twitter imepanga kuleta app yake ya ipad kwenye kompyuta zenye mfumo huo, pia kampuni nyingine kama Atlassian nayo pia inategemea kuleta programu zake kwenye mfumo huo mpya wa macOS. Kwa sasa bado haija julikana ni wabunifu wangapi wataleta programu zao kwenye mfumo huo, ila Apple inaonekana kushawishi wabunifu mbalimbali kuleta programu zao kwenye mfumo huo mpya wa macOS.

App za Apple Music, Podcasts, na Apple TV

Kama ulisoma makala iliyopita nadhani utakuwa unajua kuwa Apple imesitisha programu ya iTunes na badala yake imekuja na programu tatu mpya ambazo zitafanya kazi ambayo iTunes ilikuwa inafanya. Tofauti na mwanzo kama unataka kuweka muziki kutoka kwenye kompyuta ya Mac yenye mfumo huo mpya sasa utatumia programu mpya ambayo iko ndani ya mfumo mpya wa macOS.

Kwa upande wa Apple TV yenyewe imeboreshwa na kuwekewa sehemu ya mpya ya 4K HDR yenye HDR 10, Dolby Vision, pamoja na Dolby Atmos.

Kutumia iPad kama Kioo Cha Mac

Pamoja na yote Apple imeleta uwezo mpya wa kutumia iPad kama kioo cha pili cha kwenye kompyuta yenye mfumo wa macOS Catalina. Kama kompyuta yako itakuwa ina mfumo huo, utaweza kuunganisha kompyuta yako na iPad yako moja kwa moja huku ukiwa na uwezo wa kutumia kalamu ya Apple.

Kutumia Kompyuta ya Mac kwa Sauti

Kwenye mfumo mpya wa macOS Catalina, Apple imeleta sehemu mpya ambayo itakuwezesha kutumia kompyuta hiyo kwa maneno. Sehemu hii mpya itakuwa msaada mkubwa wa watu wenye ulemavu wa mikono.

Njia Mpya ya Kulinda Kompyuta Yako

Kama ilivyo kwenye mfumo wa iOS 13, kupitia mfumo mpya wa macOS Catalina pia utaweza kutumia app mpya ya Find My ambayo inawezesha mtu kupata laptop yake hata kama imezimwa. unaweza kusoma hapa kujua zaidi kuhusu sehemu hiyo ambayo inachanganya programu za awali za Find My Friends na Find My iPhone.

Na hayo ndio mabadiliko makubwa ya mfumo wa macOS 15.10, mfumo ambao umepewa jina la macOS Catalina. Kama unataka kujua zaidi kuhusu mkutano wa WWDC 2019 tembelea ukurasa wetu wa #WWDC 2019 hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use