Pesa ya Mtandaoni ya Facebook Kuitwa Libra na Itazinduliwa 2020

Pesa hiyo ya kimtandao haito milikiwa na Facebook kwa asilimia 100
Pesa ya Mtandaoni ya Facebook Kuitwa Libra na Itazinduliwa 2020 Pesa ya Mtandaoni ya Facebook Kuitwa Libra na Itazinduliwa 2020

Kama siku za karibuni ulisikia tetesi kuwa Facebook inajiandaa kuja na pesa yake ya mtandaoni, basi ningependa ujue kuwa hizo kwa sasa sio tetesi tena. Kwa mujibu wa tovuti ya The verge pesa hiyo imetambulishwa na msemaji wa Facebook kwa jina la Libra.

Kwa mujibu wa msemaji huyo, Libra inategemewa kuwa pesa ya kimtandao ambayo watumiaji wote duniani wataweza kuitumia kufanya malipo mbalimbali ya kimtandao au hata yela ambayo sio ya kimtandao. Vilevile kwa mujibu wa tovuti ya The Verge, pesa hiyo ya Facebook kwa sasa inategenezwa kwa ushirikiano wa kundi la kampuni 27 ambazo kwa pamoja zimetengeneza Libra Association, umoja huo ambao utakaokuwa sio wa kifedha (Non Profit) ndio utakuwa unahakikisha pesa hiyo inaendeshwa bila tatizo pamoja na kuwa na thamani halisi kama ilivyo dollar.

Baadhi ya makampuni hayo ni pamoja na Coinbase, Mastercard, Visa, eBay, PayPal, Stripe, Spotify, Uber, Lyft, Vodafone na kampuni nyingine kubwa za nchini marekani.

Advertisement

Pesa ya Mtandaoni ya Facebook Kuitwa Libra na Itazinduliwa 2020

Kwa mujibu wa Dante Disparte, ambaye ni mkuu mpya wa sera na mawasiliano wa Libra Association alisema kuwa “lengo ni kuboresha huduma za kifedha na kufanya uhamisho wa thamani na malipo kuwa mrahisi zaidi, kama jinsi internet inavyofanya kwenye uhamisho wa mawasiliano na habari”. Hata hivyo kwa mujibu wa The Verge, umoja huo unategemewa kuwa na wawakilishi dunia nzima huku makao makuu ya umoja huo yakitarajiwa kuwa huko Geneva, Uswisi.

Hata hivyo inasemekana kuwa, Facebook inategemea kutengeneza biashara mpya kabisa kupitia pesa hiyo ya mtandao ambapo Facebook inatarajia kuanzisha kampuni mpya ya inayoitwa Calibra.

Pesa ya Mtandaoni ya Facebook Kuitwa Libra na Itazinduliwa 2020

Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Facebook, Calibra itakuwa ni kampuni iliyopo chini ya Facebook ambayo itakuwa inasimamia pesa hiyo ya Libra ndani ya mitandao yake ya Facebook Messenger pamoja na WhatsApp. Kupitia pesa hiyo Facebook inatarajia kuanzisha wallet ya kidigitali ndani ya mitandao yake wallet ambayo pia itakuwa inaitwa jina hilo hilo la Calibra.

Mbali ya kuwa ndani ya mitandao ya Facebook, Calibra pia itakuwa na apps za kujitegemea ambazo zitapatikana kwenye mifumo yote ya Android pamoja na iOS. Facebook imeeleza kuwa apps hizo zitasaidia watu kuweza kutuma na kupokea Libra kwa urahisi kama ilivyo pesa nyingine za kidigital.

Pesa ya Mtandaoni ya Facebook Kuitwa Libra na Itazinduliwa 2020

Kwa sasa inasemekana kuwa umoja huo wa Libra Association unataka kuungana na makampuni zaidi ili kuongeza ufanisi wa pesa hiyo pamoja na mitandao yake ya kiteknolojia inayotumika kuhifadhi pesa hiyo, huku msemaji wake akisema kuwa, kupitia pesa hiyo pamoja na mifumo yake ya kifedha ingependa kufanya kazi na mabenki kuliko kuwa kama washindani wa kibiashara.

Kama unavyojua, seketa ya benki kwa sasa imekuwa ikibadilika kutokana na ujio wa teknolojia nyingi za kifedha za kidigital, teknolojia ambazo zinalazimisha benki hizo kubadilika na kufuata mfumo wa kidigital ambao unahitaji mteja kuwa na uwezo wa kutuma na kupokea pesa kwa urahisi kwa kutumia simu ya mkononi bila kwenda kwenye ofisi za benki au ATM.

Ni wazi kuwa kama mfumo huu wa kipesa wa Facebook ukifanikiwa, basi kila benki ina haja ya kuwezesha teknolojia hii kwani wote tunajua kwa sasa watu wengi zaidi wanahitaji urahisi wa kutuma na kupokea pesa kwa urahisi bila kukatwa makato makubwa kama ilivyo tabia ya pesa nyingi za kidigital.

Hata hivyo kwa sababu teknolojia ya pesa hiyo haimilikiwi na kampuni yoyote, Facebook imesema inatoa files za programu hiyo (Libra blockchain Technology) kupitia leseni ya Apache 2.0, ambapo mtu yoyote anaweza kutumia files hizo kuweza kutengeneza mfumo ambao utakuwa unaweza kupokea au kutuma pesa hiyo mpya ya kidigital ya Libra.

Kwa ufupi hayo ndio machache kuhusu pesa ya kimtandao ya Facebook, Kama unataka kujua zaidi kuhusu mambo mengine ya muhimu kuhusu Libra pamoja na Calibra, unaweza kusoma makala ya Techcrunch imeeleza kwa undani zaidi. (Kwa wavivu wa kusoma Makala hiyo ni ndefu kidogo).

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use