Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Uber Kunyimwa Leseni ya Kufanya Kazi Kwenye Miji ya London

Hii ni baada ya kushindwa kufuata baadhi ya vigezo na mashari nchini humo
Leseni ya Uber London Leseni ya Uber London

Mamlaka ya mawasiliano nchini London imetangaza kuwa kuanzia tarehe 30 ya mwezi huu, kampuni maarufu kwa usafirishaji wa abiria ya Uber haita ruhusuwa kufanya kazi kwenye viunga vya miji ya London.

Hata hivyo habari hizo ambazo zimetoka hivi karibuni zinasema kuwa, mamlaka hiyo ya usafirishaji imechukua hatua hiyo baada ya kampuni hiyo kushndwa kufuata, vile inayodaiwa kuwa ni vingezo na masharti ya leseni ya kufanya biashara ya usafirishaji wa abiria kama kampuni binafsi nchini humo.

Advertisement

Katika kauli ya maandishi iliyotolewa na mamlaka hiyo kupitia mtandao wa Twitter inasema kuwa, uber haina vigezo vyote vinavyo takiwa kufanya kazi ya usafirishaji wa abiria kama kampuni binafsi nchini humo na vilevile kampuni hiyo haina njia na mwenendo mzuri na imekuwa ikishndwa kusimamia mambo kadhaa ya kiusalama kwa abiria na waendeshaji wake.

Aidha kwa mujibu wa tweet kutoka mamlaka hiyo kampuni Uber imepewa siku ishirini na moja (21) za kupinga hoja hiyo ya kufutiwa leseni yake ya usafirishaji binafsi na kwa kipindi chote hicho madereva wa kampuni hiyo wana ruhusiwa kuendelea kufanya kazi kama kawaida kwenye miji ya London.

Meneja wa kampuni hiyo ya Uber nchini London Tom Elvidge, amesema kuwa kampuni hiyo itaenda mahakamani haraka iwezekanavyo kupinga hoja hiyo ya mamlaka ya usafirisha ya nchini London, kwani imekuwa ikufuata mashart yote yalio wekwa na mamlaka hiyo ikiwa pamoja na mifumo yote iliyoweka na mamlaka ya usafirishaji nchini humo.

Hata hivyo msemaji mwingine wa kampuni hiyo amesema kuwa sehemu ya kampuni hiyo ambayo inatumika kusambaza chakula nchini humo inayoitwa UberEATS haita adhiriwa na ufutwaji wa leseni hiyo na itaendelea kufanya kazi kama kawaida.

Kupata habari zaidi kuhusu sakata hili, endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video

Chanzo : The Guardian

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use