Hizi Hapa Laptop Nzuri za Kununua kwa Mwanafunzi

Laptop hizi za mwaka 2019 lakini ni bora kununua kwa sasa kutokana na bei na sifa
Laptop Bora Kwa Wanafunzi Laptop Bora Kwa Wanafunzi

Kwa sasa ni kipindi cha kuanza kujiandaa kuingia kwenye semiter mpya na kwa wengine ni kipindi cha kujiandaa kuingia kwenye masomo ya elimu ya juu, pamoja na yote hayo kuwa na laptop ni kitu cha msingi sana kwa wanafunzi ndio maana leo Tanzania Tech tunakuletea laptop bora kwaajili ya wanafunzi kwa sasa. Laptop hizi zimepangwa kwa kuzingatia ubora wa laptop ambayo mwanafunzi anahitaji na angeweza kununua.

 • Asus Zenbook UX305

Sifa za Asus Zenbook UX305

 • CPU: 6th generation Intel Core m3 – Core m5 |
 • Graphics: Intel HD Graphics 515 – 5300
 • RAM: 8GB
 • Screen: 13.3-inch FHD (1,920 x 1,080) – QHD+ (3,200 x 1,800)
 • Storage: 256GB – 512GB SSD

Laptop hii ni bora kutokana na ubora wake bei pamoja na urahisi wake wa kutumia laptop hii inauwezo wa teknolojia ya full HD screen ama hakika laptop hii ni bora sana kuwa nayo wewe mwanafunzi.

Advertisement

 • HP Chromebook 14

Sifa za HP Chromebook 14

 • CPU: 6th generation Intel Celeron
 • Graphics: Intel HD Graphics
 • RAM: 2GB – 4GB
 • Screen: 14-inch HD (1366 x 768) – FHD (1,920 x 1,080)
 • Storage: 16GB – 32GB eMMC

Kama unatafuta laptop yenye kutumia Android ukiwa na uwezo wa kuinstall app kutoka play store basi laptop hii ni bora sana kwako wewe mwanafunzi kwani kupiti play store utapata programu nyingi za kukusadia kurahisisha masomo pamoja na kuhifadhi data zako kwa urahisi.

 • Apple MacBook Pro (13-inch 2016)

Sifa za Apple MacBook Pro (13-inch 2016)

 • CPU: 6th generation Intel Core i5 – Core i7
 • Graphics: Intel Iris Graphics 540
 • RAM: 8GB – 16GB
 • Screen: 13.3-inch WQXGA (2,560 x 1,600)
 • Storage: 256GB – 1TB SSD

Hakuna asie ijua kompyuta hii kwani kompyuta hii ni bora sana na inakupa uwezo wa kuhifadhi mafile yako ya shule kwa kiwango kikubwa, pia laptop hii inaonekana kukaa na chaji sana hivyo ni laptop bora sana kuwa nayo wewe mwanafunzi.

 • Acer Chromebook 15

Sifa za Acer Chromebook 15

 • CPU: 5th generation Intel Celeron – Core i5
 • Graphics: Intel HD Graphics
 • RAM: 2GB – 4GB
 • Screen: 15.6-inch HD (1,366 x 768) – FHD (1,920 x 1,080)
 • Storage: 16GB – 32GB SSD

Kama unatafuta laptop yenye kukaa na chaji pamoja na kufanya kazi kwa haraka basi latop hii ni bora sana kwako, vile vile laptop hii inatumia Android hivyo inakupa uwezo wa kupata programu kibao za ku-kurahisishia maisha yako utakapo kuwa masomoni.

 • 13-inch MacBook Air

Sifa za MacBook Air 13-inch 

 • CPU: 5th generation Intel Core i5; Core i7
 • Graphics: Intel HD Graphics 6000
 • RAM: 8GB
 • Screen: 13.3-inch WXGA+ (1,440 x 900)
 • Storage: 128GB – 512GB SSD

Laptop hii ni moja kati ya laptop zenye nguvu na zenye kufanya kazi kwa haraka iwe unafanya kazi zaidi ya moja au unatumia laptop hiyo kwa muda mrefu MacBook Air 13-inch itakupa uhakika wa kudumu na chaji kila siku.

 • Lenovo IdeaPad Y700

Sifa za Lenovo IdeaPad Y700

 • CPU: 6th generation Intel Core i5 – Core i7
 • Graphics: Nvidia GeForce GTX 960M (2GB – 4GB)
 • RAM: 8GB – 16GB
 • Screen: 15.6-inch FHD IPS (1,920 x 1,080)
 • Storage: 500GB HDD – 1TB HDD + 512GB SSD

Bali na ubora wake pamoja na uwezo wake wa kudumu na chaji laptop hii pia ina muonekano mzuri sana ambao unavuti na ambao unakufanya utumia laptop yako kila saa hivyo kama unapenda laptop bora na yenye muonekano bora basi hii ni laptop yako.

 • Dell XPS 13

Sifa za Dell XPS 13

 • CPU: 7th generation Intel Core i3 – i7
 • Graphics: Intel HD Graphics 620
 • RAM: 4GB – 16GB
 • Screen: 13.3-inch FHD (1,920 x 1,080) – QHD+ (3,200 x 1,800) InfinityEdge
 • Storage: 128GB – 512GB SSD

Sina haja ya kusema sana kuhusu laptop hii mbali na kuwa ni bora kwa wanafunzi laptop hii inafaa kwa matumizi karibia ya aina zote hivyo kama unataka kilicho bora Dell XPS 13 ni laptop bora sana kwaajili yako.

 • Asus ZenBook Flip UX360

Sifa za Asus ZenBook Flip UX360

 • CPU: Intel Core m-6Y30 – Intel Core m-6Y75
 • Graphics: Intel HD Graphics 515
 • RAM: 4GB
 • Screen: 13.3-inch FHD (1,920 x 1,080)
 • Storage: 128GB – 512GB SSD

Kama unatafuta laptop nyembamba na yenye uwezo wa kudumu na chaji karibia siku nzima basi laptop hii ni bora sana kwako, laptop hii imetengenezwa kisasa uku ikikuwezesha kufanya kazi zako bila wasiwasi wa chaji.

 • Microsoft Surface Pro 4

Sifa za Microsoft Surface Pro 4

 • CPU: 6th generation Intel Core m3 – Core i7
 • Graphics: Intel HD Graphics 515 – Iris Graphics
 • RAM: 4GB – 16GB
 • Screen: 12.3-inch PixelSense (2,736 x 1,824)
 • Storage: 128GB – 1TB SSD

Kama unatafuta tablet ambayo inauwezo wa kufanya kazi za laptop basi tablet hii ni kwaajili yako, tablet hii inauwezo mkubwa sana pamoja na uwezo wa kudumu na chaji kwa muda mrefu sana huku ikikuwezesha kufnaya kazi zako zote bila wasiwasi.

 • Samsung Notebook 7 Spin

Sifa za Samsung Notebook 7 Spin

 • CPU: 2.5GHz Intel Core i7-6500U
 • Graphics: Nvidia GeForce 940MX (2GB DDR3L); Intel HD Graphics 520
 • RAM: 12GB – 16GB
 • Screen: 15.6-inch Full HD (1,920 x 1,080) LED with touch panel
 • Storage: 1 TB HDD – 1TB HDD; 128GB SSD

Pamoja na kuwa latop ya mwisho kwenye listi hii laptop hii inauwezo mkubwa sana huku ikikupa nafasi ya kuweza kuhifadhi data zako kwa wingi zaidi pamoja na kukupa uwezo wa kufanya kazi zako za chuo bila wasiwasi wowote.

Na hizo ndio laptop bora zinazofaa kwa mwanafunzi kwa mwaka huu, kama unataka kujua kuhusu laptop nyingine unaweza kuangalia list ya laptop bora za kununua mwaka. Pia usisahau kudownloafd app ya Tanzania Tech kama unataka kupata habari zote kwa haraka, pia unaweza kujinga na channel yetu kupitia Youtube ili kujifunza na kupata habari zote za teknolojia.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use