Jinsi ya Kuzuia Simu Yako Kuibiwa Android au iPhone

Fuata njia hizi kama unataka kuzuia simu yako kuibiwa au kupotea
Jinsi ya Kuzuia Simu Yako Kuibiwa Android au iPhone Jinsi ya Kuzuia Simu Yako Kuibiwa Android au iPhone

Ni kweli kwamba tunatumia pesa nyingi sana kuweza kununua simu nzuri za kukidhi mahitaji yetu ya kila siku, lakini wote tunajua kuwa sio wakati wote maisha yana haki, kwani kuna baadhi ya watu ambao wapo kuweza kuturudisha nyuma kwa namna moja ama nyingine.

Kuliona hili leo nimekuletea njia za kusaidia kuzuia simu yako ya Android au iOS kuibiwa au kupotea kwa namna moja ama nyingine. Kumbuka njia hizi ni hatua za awali hivyo unahitajika kuzifanya mapema kabla simu yako haija ibiwa au kupotea. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie njia hizi.

Hifadhi IMEI Namba ya Simu Yako

Mara nyingi mtu unapo nunua simu mpya huwa mawazo yapo kwenye kuweka laini na kuanza kutumia, lakini pengine mawazo yako yanatakiwa kuwepo kwenye njia za kufanya simu yako kuwa salama na kutoku potea kwa namna moja ama nyingine.

Advertisement

Sasa moja kati ya njia ya muhimu na ya awali sana unayotakiwa kufanya ni kuandika pembeni namba ya utambulisho wa simu yako yaani IMEI Namba.

Jinsi ya Kuzuia Simu Yako Kuibiwa Android au iPhone

Mara nyingi namba hii ndio hutumika kuweza kusaidia kupata simu yako au kuzuia simu yako kutumika na mwizi au mtu atakaye iokota.

Kama umenunua simu yako mpya hakikisha unatumia box la simu yako kuhifadhi au kuandika IMEI namba ya simu yako kisha hifadhi box hilo nyumbani sehemu salama.

Kuna simu nyingine kuja na IMEI namba za ziada ndani ya box, hizi zipo kama stika kama ulikua unajiuliza kazi ya stika hizo basi hiyo ndio kazi yake unatakiwa kubandika mahali salama ambapo unaweza kuona baadae kwa urahisi na haraka.

Washa Programu ya Find My Device

Kama wewe ni mtumiaji wa simu ya Android hii ni muhimu sana kwako, Unapo nunua simu yako basi moja kwa moja wakati una download programu zingine basi hakikisha una install programu ya Google inayoitwa Find My Device.

Programu hii mara nyingi inakuja na simu lakini kama imetokea hujaiona basi Install programu hiyo kupitia link hapo chini.

Jinsi ya Kuzuia Simu Yako Kuibiwa Android au iPhone

Google Find My Device

Kwa watumiaji wa iPhone pia unaweza kuwasha programu ya Find my Phone inayopatikana kwenye simu zote za iPhone. Ili kuwasha programu hiyo ingia kwenye Settings > [Jina la Akaunti yako] > iCloud.

Kama simu yako inatumia mfumo wa iOS 10.2 au zaidi basi bofya, Settings > iCloud, baada ya kufika kwenye sehemu hiyo bofya kuwasha sehemu hiyo. Unaweza kupata maelezo zaidi hapa.

Jinsi ya Kuzuia Simu Yako Kuibiwa Android au iPhone

Sehemu hizi zitakusaidia sana kujua simu yako ilipo pale inapo potea au kuibiwa, hakikisha unafanya hatua hizi mapema baada tu ya kununua simu yako.

Washa Sehemu ya Secure Start-Up (Android)

Kama wewe ni mtumiaji wa simu ya Android basi inawezekana hujui kuhusu sehemu ya Secure Startup, sehemu hii inapatikana kwenye simu nyingi za Android zenye mfumo kuanzia Android 7 Nougat na kuendelea.

Sehemu hii husaidia kila mara unapozima simu yako na kuwasha kabla simu yako haijawaka moja kwa moja itakuwa inataka password, kumbuka hii sio lock screen bali hii huzuia kabisa simu yako kuwaka hadi hapo hutakapo ingiza password.

Jinsi ya Kuzuia Simu Yako Kuibiwa Android au iPhone

Mara nyingi sehemu hii hupatikana kwenye ukurasa wa Settings > Lock screen and security > Secure startup. Kama simu yako ipo tofauti kidogo utapata sehemu kwenye ukurasa wa Security.

Tumia Apps za Ziada Kuongeza Ulinzi

Kama wewe unatumia simu ya Android basi unaweza kufaidika zaidi kwa kuongeza ulinzi wa simu yako kwa kutumia Apps mbalimbali, zipo apps nyingi sana ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza kukusaidia kuongeza ulinzi kwenye simu yako ya Android, Baadhi ya Apps hizo ni pamoja na-

Wheres My Droid
Price: Free
Find My Phone
Price: To be announced
Anti-theft alarm
Price: Free

Na Apps nyingine nyingi, unaweza kujaribu moja kati ya apps hizo kisha angalia kama zinaweza kukidhi haja ya matumizi yako na moja kwa moja tumia app hiyo kama ulinzi wa ziada kwenye simu yako.

Kuwa Muangalifu

Ushauri wangu wa mwisho ambao napenda kukupa ni kuwa muangalifu, ukweli ni kwamba kuna baadhi ya mambo hutokea bila wenyewe kujua lakini kuna baadhi ya mambo hutokea kwa kujitakia au kwa kuwa wazembe.

Ukweli ni kwamba kama unajua umenunua simu yako ya gharama basi sio mbaya kuwa muangalifu zaidi hasa pale unapokuwa unatumia simu yako, unaweza kufanya baadhi ya mambo haya ili kuongeza usalama wa simu yako.

  • Kuwa na simu ndogo ya ziada

Hii husaidia pale unapokuwa unaenda sehemu zenye mkusanyiko wa watu au sehemu ambayo huiamini kama vile club au sehemu nyingi za starehe.

  • Tumia simu yako kwa mikono miwili

Unapokuwa njiani pendelea kutumia simu yako kwa mikono miwili kwani hii hupunguza hatari ya kunyakuliwa simu yako hasa unapokuwa unatembea ( lakini pia kuwa muangalifu usinguke kwenye hii hukunyima balance).

  • Tumia simu upande wa Pili wa sikio kama Unatembea Barabarani

Kama unatembea barabarani na unaongea na simiu basi hakikisha upande sikio ambao sio wa barabara ndio upande unao tumia kuongelea na sio vingine, hii itapunguza urahisi wa kunyakuliwa simu.

  • Weka kava la Mpira kwenye simu yako lisilo teleza

Kama unaenda sehemu yenye watu wengi hakikisha unaweza simu yako kwenye kava la mpira kabla ya kuweka mfukoni wako wa jeans, hii husaidia simu yako kushikana na nguo hivyo sio rahisi mtu kuchomoa

  • Kama Upo Kwenye Dalala Tanguliza Mguu ulio na Mfuko wenye simu Mbele

Kama kwa namna yoyote unapanda usafiri wenye mkusanyiko wa watu wengi na umeweka simu yako mfukoni na umesimama, hakikisha kwa namna yoyote unatanguliza mguu wenye mfuko wa simu mbele hii husaidia mfuko kubana na husaidia pia mwizi kushindwa kuchukua simu.

Na hizo ndio baadhi tu ya njia ambazo unaweza kutumia kuweza kulinda simu yako kupotea au kuibiwa. Kama kwa namna yoyote umekwama unaweza kutujulisha kupitia kwenye sehemu ya maoni ya hapo chini. Kwa maujanja zaidi hakikisha unasoma hapa.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use