Fanya Mahesabu Muhimu ya Kila Siku Kwa Kutumia Njia Hii

Utaweza kufanya hesabu za kila siku za maisha kwa urahisi na haraka
Fanya Mahesabu Muhimu ya Kila Siku Kwa Kutumia Njia Hii Fanya Mahesabu Muhimu ya Kila Siku Kwa Kutumia Njia Hii

Ni kweli kwamba hesabu ni sehemu ya maisha yetu, ukubali au usikubali ni lazima hesabu itausika kwenye maisha yetu kila siku.

Kwa mfano kama wewe ni mlipa kodi ni lazima ujue mahesabu ya asilimia, au kama wewe ni mtu anaejihusha na maswala ya pesa za kigeni ni lazima ujue viwango vya kubadilisha fedha na mahesabu mengine.

Kuliona hili leo nimekuletea njia rahisi sana ambayo itakuwezesha kufanya mahesabu marahisi ya kila siku kwa haraka zaidi bila kupoteza muda kufikiria kanuni mbalimbali.

Advertisement

Njia hii ni bora na kwa ushauri wangu kila tu anahitaji hii uwe wewe ni mtu ambae unajihusisha na maswala ya hesabu au hata kama wewe ni mfanyabiashara au mfanyakazi wa kuajiriwa, unahitaji njia hii kwa asilimia 100.

Basi bila kuendelea kupoteza muda zaidi moja kwa moja twende nikuonyeshe njia hii ambayo najua lazima utaipenda kwa asilimia 100.

Unachotakiwa kufanya, bofya app hapo chini kisha pakua app hiyo kwenye simu yako. Baada ya kupakua app hii moja kwa moja fungua app hiyo.

Download Hapa

Baada ya kudownload app hii fungua na moja kwa moja utaweza kuona Menu upande wa kushoto juu bofya hapo na utaweza kuona aina mbalimbali za vikokoti kwaajili ya mahesabu ya kila siku.

Fanya Mahesabu Muhimu ya Kila Siku Kwa Kutumia Njia Hii

Kama unavyoweza kuna kunazo calculators za aina mbalimbali kama vile Calculator ya GPA, Loan au mkopo na aina nyingine mbalimbali za calculator ambazo unahitaji kwenye maisha yako ya kila siku. Ukweli ni kwamba app hii ni muhimu sana kwa kila mtu hebu jaribu alafu tuambie kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

Bila shaka kwa kutumia njia hii utaweza kufanya hesabu za kila siku kwa kutumia simu yako kwa urahisi na haraka. Kama unataka kujua zaidi unaweza kusoma hapa jinsi ya kufanya mahesabu magumu kwa urahisi. Au unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kupata majibu ya maswali ya hesbu kwa kupiga picha maswali.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use