Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kudivert SMS za Kawaida Kupitia Telegram

Sasa utaweza kupokea SMS zako zote kupitia programu yako ya Telegram
Jinsi ya Kudivert SMS za Kawaida Kupitia Telegram Jinsi ya Kudivert SMS za Kawaida Kupitia Telegram

Katika ulimwengu huu wa sasa ambapo tunatumia zaidi mitandao ya kijamii pamoja na programu za mawasiliano kama Telegram na WhatsApp ni wazi kuwa umuhimu wa SMS bado upo pale pale.

Hii inatokana na huduma nyingi za muhimu kutumia SMS kama njia ya biashara pamoja na mawasiliano. Kuliona hili leo nimekuletea njia fupi sana ambayo itaweza kusaidia sana kwa namna moja ama nyingine. Kupitia makala hii tunajifunza jinsi ya kudivert SMS ya kawaida kwenda kwenye programu ya telegram.

Advertisement

Njia hii inaweza kuwa msaada kwa wafanya biashara kwani unaweza kutumia njia hii kuweza kuunganisha na simu yako na kila meseji inayoingia kwenye simu yako na utaweza kupata SMS zako zote kupitia programu yako ya Telegram. Basi bila kuendelea kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye maujanja haya.

Kwa kuanza unatakiwa kuwa na simu ya Android kwani njia imethibitshwa kufanya kazi kwenye simu za Android, lakini pia hakikisha unayo app ya Telegram kwenye simu yako hiyo hiyo.

Kama tayari unayo simu ya Android pamoja na app ya Telegram, basi moja kwa moja unachotakiwa ni kupakua app ya SMSQ inayopatikana kwenye link hapo chini. App hii haipatikani kwenye soko la Play Store lakini unaweza kupata kupitia link hapo chini.

Download App ya SMSQ Hapa

Baada ya kupakua app hii na kuinstall kwenye simu yako moja kwa moja washa app hii na utaweza kuona app hiyo ikihitaji ruhusa ya kupokea SMS zako, bofya OK kama inavyo onekana kwenye picha hapo chini.

Jinsi ya Kudivert SMS za Kawaida Kupitia Telegram

Baada ya hapo moja kwa moja Sasa bofya Start sehemu ya kwanza kabisa kwenye option zinazo onekana mara baada ya kufanya hatua iliyopita.

Jinsi ya Kudivert SMS za Kawaida Kupitia Telegram

Baada ya hapo utaona tena sehemu ya permission ikitokea kuuliza kama unataka kuruhusu app hii iweze kutuma SMS zako, kupitia sehemu hiyo utabofya Allow.

Jinsi ya Kudivert SMS za Kawaida Kupitia Telegram

Baada ya hapo sasa utaletewa sehemu maalum ambayo unatakiwa kuunganisha programu yako ya Telegram na app hii, unatakiwa kuchagua app yako ya telegram kisha chagua akaunti yako kama unayo akaunti zaidi ya moja kisha bofya OK.

Jinsi ya Kudivert SMS za Kawaida Kupitia Telegram

Baada ya hapo utakuwa umemaliza kufanya setup na kila wakati ambapo utakuwa unatumiwa SMS kwenye simu hii baso moja kwa moja unaweza kuona meseji hiyo kupitia akaunti yako ya telegram.

Jinsi ya Kudivert SMS za Kawaida Kupitia Telegram

Kupitia ujumbe huo utaweza kuona namba ya simu iliyo tuma SMS hiyo, ikiwa pamoja na muda na tarehe bila kusahau na ujumbe wenyewe.

Natumaini hadi hapo utakuwa umeweza kupokea SMS ya kawaida kupitia app ya Telegram, kama kuna mahali ambapo umekwama unaweza kuandika swali lako kupitia sehemu ya maoni hapo chini, Pia kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa jinsi ya ku-forward SMS kutoka simu moja kwenda simu nyingine kwa urahisi na haraka.

1 comments
  1. Samahani nilikua naomba msaada jinsi ya kuremove permission restriction kwenye account ya Instagram ili niendelee kufanya promotion

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use