Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi Kupokea au Kukata Simu Bila Kuishika (Android)

Utaweza kupokea simu yako kwa urahisi na haraka hata kama upo bize
Jinsi Kupokea au Kukata Simu Bila Kuishika (Android) Jinsi Kupokea au Kukata Simu Bila Kuishika (Android)

Kutokana na kuwa bize na maisha ya kila siku kuna wakati unatamani kupokea simu yako bila kuishika, iwe wewe ni mpishi au mtu yoyote ambaye anafanya kazi za kutumia mikono zaidi lazima umekuwa ukihitaji njia hii.

Kupitia makala hii nitaenda kukuonyesha njia mpya na rahisi ambayo unaweza kuitumia ili kuweza kupokea simu yako kwa kutumia maneno “Yes” ili kupokea na “No” ili kukata simu.

Advertisement

Uzuri wa njia hii ni kuwa pale unapo pokea simu kwa kutumia njia hizi basi moja kwa moja simu yako itajiweka loudspeaker, hivyo huna haja ya kushika simu yako kwa namna yoyote ile, pia huna haja ya kutumia maneno ya “Yes” au “No” bali unaweza kuweka maneno yoyote yale ili kupokea au kukata simu yako kwa namna unayo ijua mwenyewe.

Jinsi Kupokea au Kukata Simu Bila Kuishika (Android)

Basi bila kupoteza muda, moja kwa moja tukangalie njia hii. Hatua ya kwanza unatakiwa kupakua app hiyo hapo chini, Baada ya kupakua moja kwa moja install kwenye simu yako na endelea kwenye hatua hapo chini.

Download App Hapa

Baada ya kupakua app hiyo hakikisha una install vizuri kwenye simu yako ya Android kisha endelea kwenye hatua zinazofuata.

Baada ya kufungua app hiyo bofya Skip kisha Bofya Start ili kuwasha App hiyo, kwa kubofya Start utapelekwa kwenye ukurasa ambao unatakiwa kuruhusu app hiyo bofya Allow Permission kuruhusu App hiyo.

Baada ya hapo sasa Unatakiwa kuruhusu App hiyo kwenye permission mbalimbali, hakikisha unasoma na kukubali permission hizo kisha endelea kwenye hatua inayofuta.

Sasa unatakiwa kuruhusu App hiyo kwenye sehemu ya Accessibility bofya sehemu yoyote kwenye screen ya simu yako kisha washa application ya Vani kupitia ukurasa huo wa Accessibility, Soma maelezo kisha Bofya Allow kuruhusu.

Baada ya hapo bofya kitufe cha Back kwenye simu yako kisha utapelekwa kwenye uwanja wa kuseti neno unalotaka ili kupokea simu yako au kukata pale unapo pigiwa.

Kama unataka, unaweza kutumia Maneno yaliyopo ambayo ni Hello kwa kupokea simu na kukata utasema No. Pia unaweza kusema speaker kuweka au kuzima loudspeaker. Kumbuka maneno yote hayo yanaweza kubadilishwa.

Ili kubadilisha maneno hayo kwenye uwanja uliopo sasa, bofya sehemu ya Mic iliyopo upande wa kulia kwenye kila neno kisha sema neno unalotala liwe maalum kupokea au kukata simu yako, fanya hivyo kwa vipengele vyote.

Baada ya hapo utakuwa umemaliza na sasa utaweza kupokea simu yako kwa kusema maneno uliyo yachagua, kumbuka njia hii ni nzuri sana kwa watu waliopo bizee kama unaendesha gari pia njia hii inaweza kukusaidia sana.

That’s it.. hiyo ndio njia ambayo unaweza kutumia kupokea au kukata simu yako kwa urahisi bila kuishika simu yako. Kama unataka kujifunza zaidi hakikisha unajiunga nasi kupitia YouTube Channel yetu hapa, kwani huko huwa tunajifunza kwa vitendo. Kwa maujanja zaidi hakikisha unasoma hapa kujua jinsi ya kutumia simu yako ya Android kwenye kompyuta.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use