Tengeneza Video za Mitandao ya Kijamii Bila Kuwa na Ujuzi

Badilisha makala yoyote ya maandishi kuwa video kwa urahisi na haraka
Tengeneza Video za Mitandao ya Kijamii Bila Kuwa na Ujuzi Tengeneza Video za Mitandao ya Kijamii Bila Kuwa na Ujuzi

Ukweli ni kwamba kwa sasa video zinayo nafasi kubwa sana pengine kuliko blogs, vitabu pamoja na magazeti au majarida mbalimbali ambayo yanakuwa kwenye mfumo wa maandishi.

Hii inasababishwa na urahisi wa kuangalia video na kuweza kujifuza kwa haraka kuliko kusoma maandishi mengi ambayo sio watu wote ambao wanapenda sana siku hizi. Kuliona hili leo nimekuleta njia mpya ya kutengeneza video za mitandao ya kijamii bila kuwa na ujuzi.

Njia hii ni rahisi sana na inaweza kusaidia mtu yoyote kutengeneza video za mitandao yake ya kijamii kwa urahisi na haraka. Unaweza kuangalia mfano wa video nilio tengeneza kwa njia hii hapo chini.

Advertisement

Kwa kuanza moja kwa moja unachotakiwa kufanya ni kuwa na Internet kwenye simu yako au kompyuta na kama unayo moja kwa moja tembelea tovuti ya lumen5.com hapa.

Baada ya hapo tengeneza akaunti kwa kubofya kitufe cha signup free kisha moja kwa moja endelea kwa kujaza data zako kwenye fomu husika, au unaweza kutumia mtandao wa facebook kuweza kujisajili kwa haraka bila kujaza fomu.

Tengeneza Video za Mitandao ya Kijamii Bila Kuwa na Ujuzi

Baada ya hapo utaletewa sehemu ambayo itakuapa urahisi wa kutengeneza video yako ya kwanza, utaweza kuchagua mfano wa video unayotaka na kisha utaweza ku-copy video hiyo na kutengeneza video yako kwa urahisi.

Tengeneza Video za Mitandao ya Kijamii Bila Kuwa na Ujuzi

Baada ya kuchagua video bofya Continue iliyopo chini mwisho upande wa kulia baada ya hapo sasa endelea kwenye hatua inayofuata ambapo sasa utaweza kubadilisha maandishi kuwa video kwa kutumia script kama unayo au kwa kutumia blog yako.

Tengeneza Video za Mitandao ya Kijamii Bila Kuwa na Ujuzi

Kama unayo website unaweka domain ya website yako au weka link ya makala unayotaka kubadilisha kuwa video. Baada ya hapo bofya Go, kama unayo script ambayo umesha andika chagua script kisha ukimaliza utaendelea kwenye hatua inayofuata.

Pia unaweza kuweka video zako au kurekodi video zako kwa kutumia kompyuta au simu yako kwa kubofya sehemu ya Record webcam or upload a file.

Tengeneza Video za Mitandao ya Kijamii Bila Kuwa na Ujuzi

Baada ya hapo sasa chagua format ya video unayotaka, unaweza kuchagua video kwa ajili ya mtandao wowote yaani Instagram, YouTube, Facebook, Twitter na mitandao mingine yote ya kijamii.

Baada ya hapo chagua mfumo wa video kisha endelea kwa kuedit video yako, kama uliweka link utaweza kuona link imebadilishwa na kuwa video na utaweza kuona video hiyo ikiwa tayari, hapo sasa unaweza kuendelea kwa kuongeza video hiyo au kupunguza.

Tengeneza Video za Mitandao ya Kijamii Bila Kuwa na Ujuzi

Ukimaliza unaweza kudownload video yako na kuweka video yako kwenye mitandao yako ya kijamii kulingana na aina ya format uliyokuwa umechagua hapo awali. Unaweza kuongeza video yako kwa kuongeza vitu mbalimbali kupitia sehemu ya kuongeza upande wa kushoto.

Mpaka hapo natumaini umeweza kutengeneza video zako kwa ajili ya mitandao yako ya kijamii. Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kutembelea channel yetu ya YouTube hapa, na pia unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kubadilisha WhatsApp Voice Message kuwa meseji ya maandishi.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use