in

Njia za Uhakika za Kufanya Biashara Mtandaoni ili Kuongeza Kipato

Fuata hatua hizi kama unataka kuongeza kipato kwa kufanya biashara mtandaoni

Biashara Mtandaoni

Hivi sasa teknolojia imekua ndio kila kitu hakuna mahali unapitia pasipo kutumia teknolojia, hiyo inadhirisha kuwa uwezekano wa kufanya biashara mtandaoni ni mkubwa sana cha msingi ni kujua ni vitu gani vya kufanya ili kuweza kuongeza kipato chako.

Kwa kuanza basi ni vyema nikwambie kabisa kuwa kama unataka kufanya biashara hizi mtandaoni, kama zilivyo biashara nyingine zinaitajika uwe mvumilivu na uwe unapenda kitu unachofanya tena ni vyema kutokufikiria pesa kwanza fanya kwanza unachokifanya kisha pesa itakuja baadae, kwa njia hiyo utaweza kufanya kitu hicho kwa uhakikia na bila kusimama au kuacha.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Fungua Blog au Tovuti

Katika swala zima la kufungua blog au tovuti hapa ni mahali muhimu sana pakuzingatia kwani watu wengi huanzisha blog na baadae kuacha sababu tu mambo yamekua magumu au muda umekua mchache wakati mwingine unakuta mtu alifungua blog ya kitu asichokipenda au sababu aliona mtu mwingine alifungua blog ya aina flani na akafanikiwa. Cha msingi hapa ni kutafuta kitu ambacho unakipenda kwa asilimia 100 na ukifanye bila kutegemea chochote kile kwani matokeo hua badae kabisa na inategemea na kitu unachokifanya na jinsi unavyo kifanya.

  • Fungua Youtube Channel

Youtube ni mtandao ambao kujiunga ni bure kabisa, lakini pia ni sehemu ya kutengenezea pesa kama utakua unafanya kitu chenye mvuto kwa jamii pamoja na watu unaotaka kuwagusa kutokana na aina ya channel ambayo umefikiria kutengeneza. Kwa hapa Tanzania kifupi ni kwamba watumiaji wa mtandao huo hawako wengi sana hivyo ni vizuri kufanya kitu ambacho ni bora kwa watu na kitavutia jamii kwa asilimia 100, hii pia inategemea na aina ya kitu unachofanya pamoja na ubora wa kitu unachofanya kumbuka pesa huja baadae hivyo fanya hivi kwa subira.

  • Fanya Biashara ya Kutafuta Masoko (Online Marketing)

Kuna watu wengi sana wanafanya au wanafikiria kufanya matangazo kupitia Instagram, Facebook, Twitter, Google pamoja na Youtube watu hao wengi wao hawajui cha kufanya hivyo ukianzisha biashara ya mtandaoni ambayo itakuwa inahusika na kufanya matangazo kwenye sehemu hizo basi hakika utafanikiwa kwa namna moja ama nyingine. Kufanya biashara hii unatakiwa kujitengenezea jina zuri pamoja na kuonyesha kwanini watu wakuchague wewe, hivyo ni vizuri kutumia muda wako kujijengea jina kwanza kabla ya kuanza kufanya biashara hii kwa hiyo pia biashara hii inaitaji subira.

  • Fanya Kazi ya Kutafutia Kampuni Wateja (Affiliate)

Affiliate ni njia inayofahamika sana ya kufanya biashara mtandaoni kuna kampuni nyingi mtandaoni ziko tayari kutoa asilimia flani kutokana na wewe kumleta mteja mmoja, kuna mpaka kampuni zingine zinatoa asilimia 40 ya kipato kinacho patikana kwa mteja ulio mleta. Kufanya biashara hii unaitajika kuwa mtaalamu kidogo wa masoko na uwe na mtandao mkubwa wa watu ambao utaweza kuwa shawishi kununua bidhaa hizo ili kusababisha wewe kupata kamisheni.

  • Tengeneza Akaunti za Mitandao ya Kijamii

Una njia imeingia sasa hasa kwenye mtandao wa Instagram njia ni yakutuma matangazo mbalimbali ya biashara kwenye akaunti mbalimbali, njia hii ni nzuri kama utakuwa umetengeneza akaunti ya kitu ambacho unakipenda na uhakikishe una weka makala mpya kila siku ili kuvutia follower wengi kwenye akaunti zako. Hakikisha ununui follower kwa namna yoyote ile acha watu wakufuate wenyewe kwani akaunti nyingi zilizo nunua follower unakuta mtu ana post picha wana like watu 1000 wakati akaunti hiyo ina follower zaidi ya watu laki mbili, hapo unakuta hao 1000 ndio wenye kufuata page yako kutokana na kitu unachokifanya. Hivyo ni muhimu kufanya kitu unachokipenda na acha watu wakufollow wenyewe hapo utapata wateja wengi.

  • Nunua na Uza Vitu Mtandaoni (Buy and Sell)

Kuna mitandao mingi hivi sasa ya kukupa uwezo wa kuuza vitu, unaweza kununua kitu kipya kisha ukakiuza kwenye mtandao au kama una kompyuta, simu au kitu chochote ambacho unaona huna matumizi nacho unaweza ukaanza kwa kukiuza kisha ukanunua tena na kuuza kwa faida. Njia hii ni njia rahisi na inahitaji kuwa makini pale unapo nunua usije kununua kitu kibovu kwani biashara yako ndio inayotegemea, kuwa mvumilivu na hakikisha unafanya kwa umakini na ustarabu mkubwa sana ili kuongeza wateja kwenye biashara yako, pia hakikisha utafuti faida kubwa kwani hiyo itawafanya watu kuona ni bora waende dukani kuliko kununua kitu hicho kwako.

Hizo ni baadhi ya njia ambazo ukweli zinaweza kukusaidia kupata kipato na ukifuata kwa umakini utafanikiwa kwa asilimia 100, ukweli ni kwamba ukifanya unachokipenda lazima pesa na mafanikio yatakuja kwani utakifanya kwa ustarabu na umakini wa hali ya juu kwa sababu unakipenda utaki kuona kitu hicho kipo ovyo. Hakikisha unafuata ndoto zako na anza kufanya sasa…..

Kwa habari zaidi za teknolojia download App ya Tanzania Tech au tufuate kwenye channel yetu ya Tanzania Tech kupitia mtandao wa Youtube ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia.

Njia za Uhakika za Kufanya Biashara Mtandaoni ili Kuongeza Kipato
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

11 Comments