in

Jinsi ya Kuroot Simu Yoyote ya Tecno Bila Kutumia Kompyuta

Njia ya bora ya ku-root simu yoyote ya tecno bila kutumia kompyuta

Ku-root Tecno

Hivi karibuni tumepata maswali mengi sana yanayouliza jinsi ya ku-root simu za android za tecno, hivyo basi leo nakuletea makala hii mpya ambayo itakusaidia kufanya hivyo bila kutumia kabisa kompyuta.

Kabla ya kuanza ni vyema ukajua nini maana ya ku-root simu, ku-root simu ni neno linalotumika kwa watumiaji wa simu za android likiwa lina maana kuwa, hii ni njia ambayo inatumika kufanya simu za android kuwa na uwezo wa kuona au ku-xpose file zinazo hifadhi mfumo wa uendeshaji wa Android ili kuipa simu yako uwezo zaidi. Lakini kumbuka kwa kuroot simu yako utakuwa umevunja vigezo na masharti yanayokuja na mkataba wako wa warrant pale unapo nunua simu yako, hivyo kuwa makini na usifanye hivi kama hujui unachokifanya.

Basi moja kwa moja twende tukanze somo letu la leo, kumbuka kwa kufanya hivi unaweza kuharibu simu yako hivyo ni vyema kuwa makini sana na utakapo haribu simu yako hatuto husika kwa namna yoyote ile hivyo tafadhali kuwa makini na fanya hivi kwa kukumbuka mambo hayo ya muhimu.

Jinsi ya Kuongeza Uwezo wa RAM kwenye Windows PC

Kwa kuanza basi unatakiwa kudownload App ya Framaroot Hapa kisha install moja kwa moja kwenye simu yako, baada ya hapo fungua App hiyo kisha chagua Superuser au SuperSU. Kisha endelea mbele kwa kuchagua Boromir, baada ya hapo kama umefuata hatua zote utaona meseji ikitokea inayo kwambia umefanikiwa ku-root simu yako, kama umefika hapo usiwe na haraka bali kinachofuata unatakiwa ku-restart simu yako fanya hivyo kisha kwa kubofya OK.

Baada ya kufanya hivyo utakuwa umefanikiwa kuroot simu yako ya Tecno bila kutumia kompyuta, njia hii imeonekana kusaidia watu wengi sana wenye simu za tecno hivyo natumaini hata wewe itakusaidia. Kama utakuwa umekwama mahali usisite kutuandikia kwenye maoni hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

33 Comments

  1. Asante,

    Kuna misemo watu husema kuwa ikiwa simu itakuwa chini ya 50% za charge kwamba simu itaharibika hili likoje?
    Na j kwa kufanya rooting wengine husema wakati una weka apps upya utakayo sahau kuweka haitapatika tena ni sahihi?

  2. Kaka mm nimetumia app nyengine isiyokuwa hii nimefanikiwa kuroot na sasa natumia simu kwa kujisikia app ambayo imenisaidia inaitwa kingroot ambapo kwenye play store haipo ila kwenye app inayoitwa uptodown app unaweza kuipata bila tatizo lolote.Simu niliyo tumia app hii ni sony xperia c245

  3. Maoni*jamani natumia TECNO T430 lakini nikifungua internet inakubali lakini kunamda inafika inazima na kuwaka yenyewe baada ya sekunde kadhaa sijui tatizo nini afu pia nikituma txt delivery report inaniandikia fail ila unakuta twt imefika kwa nimtumiaye sasa jamani msaada wenu please!